Mh. Rais, Mkuu wa Wilaya na OCD Lindi 'wamemuua' ANGEL KESSY Mwanafunzi wa PCB

Status
Not open for further replies.

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,369
Mh Rais, mimi ni raia wa Tanzania na ni mwananchi wako mwema.

Naomba kwa masikitiko makubwa tena makubwa nikujulishe tu ya kuwa:

Juzi nilipigiwa simu na Mkuu wa Wilaya ya Lindi akinijulisha kuhusu KIFO cha mwanafunzi ANGEL HONEST KESSY.

Kwanza nilishangaaa kuona Mkuu wa Wilaya akinipa taarifa ya kifo cha mtoto ambae mimi ndo nilimfikisha hapo shuleni WIKI MBILI ZILIZOPITA.

PILI NILIUMIA mpaka nikazimia na kulazwa hosptali ya Bugando maana mwananu wakati anaumwa sikuambiwa lolote, siku alipofariki ndo napigiwa simu na Mkuu wa Wilaya kwa kuungana na OCD wa Wilaya Lindi. MKUU WA WILAYA ALITUMIA NO HII AMBAYO NO NI YA OCD WA LINDI KUWASILIANA NA MIMI 0659888632

Mh, Rais sisi wazazi tunaomba mambo yafatayo yafanyike:

Mkuu wa Wilaya: Nilimwambia huyo ni mwanangu asimlete kwangu mpaka mimi nifike hapo, ALIKATAAA. JE, KWANINI ALIKATAA?

PILI: Kwanini kifo cha mwanangu kiripotiwe na Mkuu wa Wilaya BADALA YA MGANGA MFAWIDHI?

MWANANGU ANILIPIGIA SIKU MOJA KABLA YA KIFO CHAKE AKIOMBA PESA YA MATIBABU, NILITUMA KWANINI BAADA YA KUTUMA PESA KWENYE NAMBA YA MATRONI HAKUPOKEA SIMU TENA?

Mh. Rais, mimi sina mtoto nje ya marehemu ANGEL.

Bado najiuliza, KWANINI MKUU WA WILAYA ALILAZIMISHA MWILI KUPAKIWA KULETWA DAR HOPSTALI YA TEMEKE PASIPO RIDHAA YA MAANDISHI (KUTOKA LINDI KUJA DAR)?

Mhe. Rais, natarajia kumzika mwanangu siku ya Jumatatu, naomba sana mwili wa mwanangu kabla haujazikwa ufanyiwe postmotamu.

Mkuu wa Shule, Mkuu wa Wilaya ma OCD nawaona kama wahusika wa kifo cha mwanangu wa pekee.

Soma pia hapa: Kwanini nawahusisha Mkuu wa Wilaya na OCD Lindi kwenye kifo cha mtoto wangu...
 
Tulianza na
  1. Handeni mjamzito kufariki kwa kukosa Tsh 150K
  2. Mgonjwa kutakiwa kulipa Tsh 86K ili asomewe cd ya vipimo vyake
  3. Leo kifo chenye utata Lindi
 
mkuu... mimi nakushauri muache mtoto apumzike. unaweza ukafanyika uchunguzi lakini haitobadilisha ukweli kuwa hivi sasa tunaomboleza.

hivyo ni vigumu mtu yeyote kukubali kirahisi ràhisi kupokea kifo cha mpendwa wake. ila ninacho kushauri liache hilo lipite Muda utaleta jibu...!​
 
Fuatilia vema,ujue kifo kimesababishwa na nini,usije ukawa unawatuhumu polisi tu.Fuatilia na pole sana.Polisi wapo wema na wapo wabaya pia,lakini tusiwe tunawalaumu kwa ujumlajumla.
 
mkuu... mimi nakushauri muache mtoto apumzike. unaweza ukafanyika uchunguzi lakini haitobadilisha ukweli kuwa hivi sasa tunaomboleza.

hivyo ni vigumu mtu yeyote kukubali kirahisi ràhisi kupokea kifo cha mpendwa wake. ila ninacho kushauri liache hilo lipite Muda utaleta jibu...!​
Samahani mkuu, kwanza nikuulize tu kama una mtoto??
Maana nisje nikakuonea bure kumbe haujui hata uchungu wa mtoto kwa mzazi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom