Mkuu wa Wilaya Arusha na mbwembwe za misafara

Kijana anatenda kama kijana na mzee anatenda kama mzee,...kama wewe ni mzee usione ya vijana hayana maana utakuwa unaingilia uumbaji wa mungu
Heshima sana wanajamvi,

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini ni kijana mdogo lakini mwenye mbwembwe nyingi na vituko vya ujana uliopitiliza. Katika siku za karibuni amekuwa na tabia ya kusindikizwa na gari la Polisi ikiambatana na ving'ora vingi pengine ungefikiri kuna mgonjwa wa COVID 19 anakimbizwa Hospitali kuwahi huduma za kitabibu.

Mwezi uliopita kama kumbukumbu zangu zipo sana alizindua mradi mdogo {mradi uchwara} wa kufyatua matofali wa halmashauri ya Jiji la Arusha. Huo msafari ungefikiri anakwenda kuzindia kinu cha Nyuklia gari zilikuwa zinakimbizwa,ving'ora na taa za magari yote zikiwashwa full light.T

utakae tukubali Vijana wakipewa madaraka kidogo wanaharibu sana, wanaumiza wananchi sana, wanatumia madaraka vibaya sana bahati mbaya Mkuu wa Wilaya ya Arusha anaingia katika kundi hilo.

Mwaka jana alishiriki zoezi la kuwachapa viboko wafanyabiashara kwa madai ya kununua thamani za shule. DC kawa mpelelezi, akajivika ujaji na mwisho wa siku akamalizia kudhalilisha wananchi pasipo uchunguzi wa haki.
 
Back
Top Bottom