Mkuu wa Wilaya Arusha na mbwembwe za misafara

Acha wivu, tafuta shughuli ufanye. kukosa kwako shughuli ndo kunakufanya uwaonee wanaume wenzio wivu na kuanza kupika majungu. Nakushauri nenda kauze hata njugu hutopata muda wa kuleta umbea humu.
W
Huyo ni mmoja wa ma DC wajinga sana walioteuliwa na mwendazake.

Sifa yake kubwa ilikuwa nadhiri ya kuondoa uhai wa Zitto.
 
Unafikiri mama hamjui huyu dogo wa kucharaza viboko watu? Anamjua sana, na wengine mafaili yao yapo wazi kwake, shida tu mama anawastahi na kuwapa second chance watu wa Mwendazake. Sina uhakika kama Ali Happi atatoboa kwenye huu utawala
Alipata uteuzi kwa kutaka
Unafikiri mama hamjui huyu dogo wa kucharaza viboko watu? Anamjua sana, na wengine mafaili yao yapo wazi kwake, shida tu mama anawastahi na kuwapa second chance watu wa Mwendazake. Sina uhakika kama Ali Happi atatoboa kwenye huu utawala

Alipata uteuzi baada ya kutamka hadharani kuwa Mbunge aliyeshawishi Benki ya Dunia kusimamisha mkopo kwa nchi yetu anastahili kuuwawa! Hizo ndizo roho zilizokuwa zinatakiwa katika uongozi wa nchi! Swali je, kijana mdogo hivi akiachishwa uongozi anakwenda wapi? Vijana wajifunze kujiendeleza kimaisha kabla ya kuingia siasa.
 
Kale kakijana mbina kanaonekana kastaarabu, kwani naye kichwa ishaanza ota pembe!!!
 
Sema katika viongozi vijana hapa Arusha ambao naona Wana afadhali ni huyu Kihongosi ,anajitahidi kuchapa kazi,kusimamia na kutatua kero za wananchi kwa upande wangu naona hana noma ni mtu poa hata ukikaa nae.
 
Heshima sana wanajamvi,

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini ni kijana mdogo lakini mwenye mbwembwe nyingi na vituko vya ujana uliopitiliza.Katika siku za karibu amekuwa na tabia ya kusindikizwa na gari la polisi ikiambatana na ving'ora vingi pengine ungefikiri kuna mgonjwa wa Covid 19 anakimbizwa Hospital kuwahi huduma za kitabibu.

Mwezi uliopita kama kumbukumbu zangu zipo sana alizindua mradi mdogo {mradi uchwara} wa kufyatua matofali wa halmashauri ya Jiji la Arusha.Huo msafari ungefikiri anakwenda kuzindia kinu cha Nyuklia gari zilikuwa zinakimbizwa,ving'ora na taa za magari yote zikiwashwa full light.Tutakae tukubali Vijana wakipewa madaraka kidogo wanaharibu sana,wanaumiza wananchi sana,wanatumia madaraka vibaya sana bahati mbaya Mkuu wa Wilaya ya Arusha yumo katika kundi hilo.

Mwaka jana alishiriki zoezi la kuwachapa viboko wafanyabiashara kwa madai ya kununua thamani za shule.DC kawa mpelelezi,akajivika ujaji na mwisho wa siku akamalizia kudhalilisha wananchi pasipo uchunguzi wa haki.

Naye ni mmoja kati ya wale wa miaka ya 80?
 
Kwakweli huyu mkuu wa wilaya ya Arusha simjui vizuri ila ni mtu poa sana.

Nakumbuka mwishoni mwa mwaka jana alitusaidia kupata mafao yetu NSSF baada ya kusumbuliwa karibia mwaka mzima.
Nnachokumbuka tulimfata siku moja tuna akatuambia turudi baada ya siku 3, na tulivyorudi aliondoka na sisi hadi kwenye ofisi za nssf pale Arusha na akaingia na sisi hadi ndani, akakagua computer za pale kwa sababu tulimweleza namna tunavyopigwa danadana muda mrefu bila majibu ya kueleweka....
Meneja alijitahidi kujitetea kwa uongo mwingi lakini kupitia mkuu huyu wa wilaya tulipata mafao yetu bila kuchelewa.

Kumbuka tulikua wengi hivyo alitusaidia sana
Namkubali sana maana amesaidia watu wengi kuanzia waliodhulumiwa maeneo yao, migogoro ya kifamilia na mengine mengi... Kwakweli nilimkubali hadi nikawa nahudhuria kwenye ziara zake za kusikiliza kero za wananchi.

Yule aliyekuwepo kabla yake tulimfata akatufukuza na maneno mbovumbovu bahati nzuri hakumaliza mwezi akaondolewa ndio akaletwa aliyepo sasa.
System vs personalities
 
Back
Top Bottom