Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 958
- 1,978
Baraza la Mawaziri la Israel limeadhimia kumfuta kazi Mkuu wa Usalama wa Taifa hilo Ronen Bar huku wananchi jijini Tel Aviv wakiandamana kupinga uamuzi huo.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliwasilisha pendekezo hilo kwenye baraza la mawaziri kwa madai kuwa Bar amekuwa akiendesha mambo ya kiusalama kwa maslahi binafsi.
Duru zinaeleza kuwa wawili hao wamekuwa wakizozana kwa miezi kadhaa huku Bar akimtuhumu Netanyahu kwa kile alichodai rushwa ya uchaguzi.
Bar anasema kuwa amefutwa kazi ili kufichwa ukweli kwa matukio ya awali kabla operesheni za kijeshi zilizofanywa Gaza tarehe 7 Oktoba 2023.