Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Malawi atengua Amri ya Rais Banda ya kufuta Matokeo ya Urais

Tuliwahi kuimba enzi zetu" ti lutye pamozi ndi mtima u mozi,ti lutye pamozi ndi mtima u moziiii! Nyerere tie,tie pamozi,tie,tie pamozi tuende pamozi ndi mtima u moziii!. Samahani wengine mlikua hamjazaliwa!
 
Wenzetu wana mahakama, wana mwanasheria mkuu wa serikali, wana tume ya uchaguzi. Jumamosi sio siku ya kazi lakini wameweza kulipa jambo hili uzito unaostahili na kufungua mahakama na kutoa amri, Mwanasheria wa serikali hakupeleka pingamizi kupinga hayo maombi kama hapa na mahakama haikutaka kupendelea serikali.

HAPA KWETU ISINGETOKEKA ASILANI.

Tumejifunza na ofisi ya mwanasheria wa serikali nadhani imefanya hivyo na tume ya uchaguzi imeborrow a leaf.

Sina uhakika na polisi na jeshi la malawi wako upande gani
 
  • Thanks
Reactions: BAK
URAIS mtamu jamani duh!Yaani unavunja hata sheria mradi ushinde tu.Sasa anauhakika gani akirudia mara ya pili atashinda?Inawezekana hata zile alizopata asizipate kabisa.Afrika kazi tunayo.
 
Bongo tume zetu zingekuwa hivi , wanasheria wangeheshimika saana na utawala bora ungewezekana, nafikiri manadiliko ya katiba yaangalie kama vifungu hivyo vipo

Hawa wanasimamia taaluma na sheria inavyotaka! Hawana professional Dishonesty, kama wale aliowaita Jaji Mzee J S Warioba. Ukisimamia FACTS na ueledi kama taaluma yako ilivyokuelekeza huwezi kupindisha mambo kishabiki shabiki tu! Mfano mkubwa wa Professional Dishonesty hapa Tanzania ni ule wa wasomi wetu kukana maandiko yao, wabobez wa sheria KUTETEA tena kwa kutokwa misuli eti KURA YA WAZI, wakati kitaalam wanajua ni UPOTOFU.
 
Haya maamuzi ya Raisi Joyce Banda iwe ni angalizo kwa magamba kulazimisha wanawake kushika nafasi za juu kwenye uongozi wajue sio nafasi zote wanamudu wanaweza kutoa maamuzi yasiyo na tija kwa Taifa.
 
mweheee shemeji yetu pamoja na kupewa kimemo cha jinsi ya kuiba kura hakija msaidia au mkwele kamwingiza mjini
 
I think it indirectly happened here in 2010! Mkithubutu 2015,maana dalili zinaonesha, mtapata cha moto!
 
Unachosema ni kweli kabisa lakini hapa kwetu wanasheria wananunulika sana na vyombo vya dola ni vitengo maalum vya MACCM katika kuhakikisha MACCM wanatimiza dhamira yao ya kuitawala nchi milele. Nadhani unakumbuka vitisho vilivyotolewa vya "jeshi kuchukua nchi" pindi katiba mpya ikiruhusu Serikali tatu. Demokrasi nchini haipo, angalia UKAWA jinsi inavyonyanyaswa katika mikoa mbali mbali kwa kunyimwa ruhusa ya kufanya mikutano ya hadhara, bado tuna safari ndefu sana.

Bongo tume zetu zingekuwa hivi , wanasheria wangeheshimika saana na utawala bora ungewezekana, nafikiri manadiliko ya katiba yaangalie kama vifungu hivyo vipo
 
MEC wanatoa statement ya kuendelea na kazi muda huu hadi hapo High Court itakapo amua otherwise na vote recount is on the way!!!! Kazi ipo

Anaongea tena saa nne na nusu Hii, chanell ya MBC
 
...mmmh! Matokeo ya Urais Malawi hadi jana jioni
yalikuwa hivi:,

1:prof.Peter Mutharika wa DPP 1,789,364 ,


2:Lazarus Chakwera wa MCP 1,388,500,


3:Joyce Banda wa PP 1,042,686,


4:Atupele Muluzi wa UDF 665,519



*********
Updates tafadhari...
**********
 
Back
Top Bottom