Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Malawi atengua Amri ya Rais Banda ya kufuta Matokeo ya Urais

Mahakama za bongo zina uzalendo kama za hawa jamaa?

Ninachoona hapa ni kwamba Mahakama itasimama upande wa CCM na kukandamiza upinzani
 
Kwa nn hataki kukubali matokeo? Bila shaka kuna madudu aliyo yafanya.people's power.na hivi ndivyo itakavyo kuwa kwa Shemeji yetu.tujiandae
 
Dakika chache Zilizopita,Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Malawi Justice Mbendera amekaidi Amri ya Rais Banda ya kufuta matokeo ya uchaguzi.

Mbendera amewaagiza maofisa wa tume ya uchaguzi kuendelea na zoezi la kuhesabu kura na kuomba ushirikiano wao wa dhati katika kipindi hiki kigumu.

Amesema Rais hana mamlaka ya kuingilia tume ya uchaguzi ambayo inafanya kazi kikatiba na kisheria.

Pia Rais Wa chama cha wanasheria wa Malawi (MLS) na Pia Mwanasheria Mkuu wa Zamani wa Malawi wameongea na Vyombo vya Habari Mud Mfupi uliopita na kusema ibara aliyoitaja Rais haimpi mamlaka ya kufuta uchaguzi..

Wamesema kifungu cha 5 cha sheria ya uchaguzi wa Bunge na Rais kinaipa Mamlaka Jukumu lote tume ya uchaguzi kusimamia mchakato wa Uchaguzi. Pia kifungu cha 100 cha sheria hiyo kinatoa haki ya chama au mgombea kulalamika kwa tume kuhusu ukiukwaji wa Mwenendo wa Uchaguzi na kama ndani ya masaa 48 hali hiyo isiporekebishwa kwa kiwango cha kuridhishwa basi kifungu namba 113 cha sheria hiyo hiyo kitatumika kupeleka mashtaka Mahakama Kuu.

Hata hivyo Mwanasheria mkuu akizungumzia Amri hiyo ya Rais leo hii amesema "Kuna Mtu anafanya uhaini hapa sasa" na kuendelea kudai kuwa Rais amefanya uhaini kwa kukiuka ibara ya 88 ya katiba ya nchi kutoa "Presidential Decree" bila sababu yoyote ya msingi inayozingatia katiba na mamlaka ya kisheria .
 
Hata mimi jana nililiona hilo ndiyo maaana nikaweka bandiko hili hapa JF. Sama hapa tumepisha na vifungu wao wametumia cha tano nami nimetumia cha saba

Mama Joyce Banda kachemka....katiba ya Malawi (2006) hairuhusu mtu yeyote kuingilia TUME YA UCHAGUZI kwenye shughuli zake...sehemu ya Saba ya katiba ya Malawi inayohusu Uchaguzi inasomeka hivi:

"Powers and functions 76
: ........

3. Any person who has petitioned or complained to the Electoral Commission shall have a right to appeal to the High Court against determinations made under subsections (2) (c) and (2) (d).

4. The Electoral Commission shall exercise its powers, functions and duties under this section independent of any direction or interference by other authority or any person.


............................."

https://www.jamiiforums.com/interna...arudiwa-ndani-ya-siku-90-a-4.html#post9623723
 
Pamoja na msimamo mzuri wa mwenyekiti wa tume lakini bado kuna kasoro zimejitokeza katika maeneo mbalimbali kwa watu kupiga kura zaidi ya mara moja mfano kuna sehemu panaitwa Mangoshi imeonekana kwamba waliojiandikisha ni watu 39,000 lakini waliopiga kura ni laki moja hivi, hivyo tume inaangalia uwezekano wa kuhesabu kura moja moja tena. Source; Amka na BBC leo saa 12 alfajiri mtangazaji Baruani Muhuza
 
Sina shaka Justice Mbendera anaongozwa na Mungu, majaji wote Duniani wanapashwa kuwa na morals na integrity ya hali ya JUU- ni matumaini yangu kwamba Wenzetu Watanzania wata emulate mfano mzuri wa kuhugwa wa MZALENDO wa kweli wa Nchi ya MALAWI one "Justice Mdendera" Mungu akuongezee hakima kama za Mfalme SELEIMAN.
 
Nilitaka kushangaa hawa jamaa wanasheria za aina gani kama mgombea anauwezo wa kuahirisha uchaguzi. La kuhama chama ukiwa rais lilinishangaza hili la huyu mama nalo liliniacha hoi.

kwa Africa inawezekana sana, basi tu amechemka ukilinganisha na ma-dictators wengine, wangevuruga uchaguzi in their favour tangu mwanzo. mtu kama Kagame au Mzee wa Zimbabwe ungemwambia nini, eti tume? what is tume by the way.
 
Back
Top Bottom