Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Malawi atengua Amri ya Rais Banda ya kufuta Matokeo ya Urais

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,840
2,000
Kwani Nabii hakumweleza matokeo ya uchaguzi?

Dakika chache Zilizopita,Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Malawi Justice Mbendera amekaidi Amri ya Rais Banda ya kufuta matokeo ya uchaguzi. Mbendera amewaagiza maofisa wa tume ya uchaguzi kuendelea na zoezi la kuhesabu kura na kuomba ushirikiano wao wa dhati katika kipindi hiki kigumu.

Amesema Rais hana mamlaka ya kuingilia tume ya uchaguzi ambayo inafanya kazi kikatiba na kisheria. Pia Rais Wa chama cha wanasheria wa Malawi (MLS) na Pia Mwanasheria Mkuu wa Zamani wa Malawi wameongea na Vyombo vya Habari Mud Mfupi uliopita na kusema ibara aliyoitaja Rais haimpi mamlaka ya kufuta uchaguzi..

Wamesema kifungu cha 5 cha sheria ya uchaguzi wa Bunge na Rais kinaipa Mamlaka Jukumu lote tume ya uchaguzi kusimamia mchakato wa Uchaguzi. Pia kifungu cha 100 cha sheria hiyo kinatoa haki ya chama au mgombea kulalamika kwa tume kuhusu ukiukwaji wa Mwenendo wa Uchaguzi na kama ndani ya masaa 48 hali hiyo isiporekebishwa kwa kiwango cha kuridhishwa basi kifungu namba 113 cha sheria hiyo hiyo kitatumika kupeleka mashtaka Mahakama Kuu.

Hata hivyo Mwanasheria mkuu akizungumzia Amri hiyo ya Rais leo hii amesema "Kuna Mtu anafanya uhaini hapa sasa" na kuendelea kudai kuwa Rais amefanya uhaini kwa kukiuka ibara ya 88 ya katiba ya nchi kutoa "Presidential Decree" bila sababu yoyote ya msingi inayozingatia katiba na mamlaka ya kisheria
 

Ben Saanane

Verified Member
Jan 18, 2007
14,595
2,000
Haya Dramma inaendelea Malawi...

Rais Joyce Banda muda mfupi uliopita ameatoa Amri kwa Tume ya Uchaguzi ya Malawi(MEC) Kuacha mara moja kutangaza matokeo na kufuta uchaguzi ambao vyama viwili vya Upinzani vilikua vikiongoza.Ametaka uchaguzi uitishwe kwa kipindi cha Siku 90 zijazo

Chama cha Wanasheria Malawi nacho kimesema Rais hana Mamlaka ya kisheria/kikatiba kusitisha mchakato wa kutangaza Matokeo ya uchaguzi

Kama nilivotabiri tangu juzi kuwa kuna kila Dalili ya Mama huyu kutia Aibu nyingine kwa Taifa lake na Afrika Kwa Ujumla

-Alipoona Peter Mutharika anaongoza alituma jeshi na pia polisi nyumbani kwake

-Naibu waziri wake aliposhindwa Ubunge alijipiga risasi na kujiua

-Chama chake kilivituhumu vyombo vya habari kwa kupendelea upinzani

-Jana alipeleka Pingamizi mahakamani kuzuia matokeo kutangazwa na kukituhumu chama cha upinzani kufanya wizi wa kura.Mahakama ilitupilia mbali pingamizi hilo kwa hoja kuwa halina msingi

-Jana hiyo hiyo mkuu wa idara ya habari na Matangazo alifukuzwa kazi kwa kukiuka Amri ya Serikali ya kusitisha matangazo ya matokeo ya uchaguzi.Chama cha Wanasheria Malawi kikasema kuwa kilichofanyika ni uonevu mkubwa.

Hawa ndio madikteta wa Afrika wasiotaka kushindwa uchaguzi

Roodney alipoandika "People's Power ,No Dictator" alisema kuwa "Madikteta wanajikweza na pia kuinuliwa na watu.Wanajiona wako juu ya Watu,Taasisi na oganization Zote.Wanainuliwa na kutukuzwa na watu,taasisi,viongozi wa Dini na viongozi wa Kimila".Hii ndio picha halisi ya viongozi wa Afrika

Sasa anachotafuta Joyce Banda ni Vurugu ili atangaze hali ya Hatari na afanye Suspension ya Katiba in order to assume fully dictatorial power.

Jumuiya ya Kimataifa hasa SADC,COMESA,AU na UN hazitakiwi kuruhusu hali iliyojitokeza Nigeria Mwaka 1993 ya Dikteta Ibrahim Babangida kufanya nullification ya Matokeo ya Urais yaliyokua yamempa Ushindi Chifu Mashoud Abiola na baadae Abiola kuwekwa ndani akiwa President Elect hadi miaka 5 ilipopita na kufanyiwa hujuma akiwa Gereni pia chini ya Utawala wa Mtawala wa kijeshi Dikteta Sani Abacha. Chifu Abiola alikufa kifo cha Kutatanisha baadae kabla Olusegun Obasanjo hajaachiwa Kutoka Gerezani na kuongoza mageuzi ya kisiasa kwa msaada wa jumuiya ya kimataifa baada pia ya kifo cha ghafla cha dikteta Sani Abacha.

We must cherish the values of Democracy.Kama AU inakata Mapinduzi (Coup d'etat) dhidi ya Tawala zilizochaguliwa Kidemokrasia,kwanini turuhusu watawala kupindua matakwa ya umma kupitia sanduku la kura(Coup d'Civillien)?

Hili halitakiwi kuachwa hata kidogo karne hii

Upinzani Tanzania tujiandae kukabiliana na hali hii Mwakani.Naamini Upinzani Malawi Utasimama kidete bila kuyumba kukabiliana na udikteta huu.Tume ya Uchaguzi ya Malawi hadi sasa imeonyesha Msimamo bila woga.

Matokeo ya Urais Malawi hadi jana jioni yalikuwa hivi:,

1:prof.Peter Mutharika wa DPP 1,789,364 ,

2:Lazarus Chakwera wa MCP 1,388,500,

3:Joyce Banda wa PP 1,042,686,

4:Atupele Muluzi wa UDF 665,519

*********
Updates
**********

Dakika chache Zilizopita,Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Malawi Justice Mbendera amekaidi Amri ya Rais Banda ya kufuta matokeo ya uchaguzi.

Mbendera amewaagiza maofisa wa tume ya uchaguzi kuendelea na zoezi la kuhesabu kura na kuomba ushirikiano wao wa dhati katika kipindi hiki kigumu.

Amesema Rais hana mamlaka ya kuingilia tume ya uchaguzi ambayo inafanya kazi kikatiba na kisheria.

Pia Rais Wa chama cha wanasheria wa Malawi (MLS) na Pia Mwanasheria Mkuu wa Zamani wa Malawi wameongea na Vyombo vya Habari Mud Mfupi uliopita na kusema ibara aliyoitaja Rais haimpi mamlaka ya kufuta uchaguzi..

Wamesema kifungu cha 5 cha sheria ya uchaguzi wa Bunge na Rais kinaipa Mamlaka Jukumu lote tume ya uchaguzi kusimamia mchakato wa Uchaguzi. Pia kifungu cha 100 cha sheria hiyo kinatoa haki ya chama au mgombea kulalamika kwa tume kuhusu ukiukwaji wa Mwenendo wa Uchaguzi na kama ndani ya masaa 48 hali hiyo isiporekebishwa kwa kiwango cha kuridhishwa basi kifungu namba 113 cha sheria hiyo hiyo kitatumika kupeleka mashtaka Mahakama Kuu.

Hata hivyo Mwanasheria mkuu akizungumzia Amri hiyo ya Rais leo hii amesema "Kuna Mtu anafanya uhaini hapa sasa" na kuendelea kudai kuwa Rais amefanya uhaini kwa kukiuka ibara ya 88 ya katiba ya nchi kutoa "Presidential Decree" bila sababu yoyote ya msingi inayozingatia katiba na mamlaka ya kisheria .

*****Updates***

Mgombea Urais wa Chama cha DPP kinachoongoza katika matokeo ya Urais yasio Rasmi Prof. Peter Mutharika amesema Rais Joyce Banda hana mamlaka ya kisheria kufuta matokeo ya uchaguzi na kumtaka atumie muda wake uliosalia madarakani kulinda amani na utulivu hadi atakapondoka ikulu.

Pia Muda mfupi uliopita Mahakama Kuu imetupilia pembeni Amri ya Rais Joyce Banda ya Kufuta Matokeo ya Uchaguzi na kuamuru Tume ya Uchaguzi kuendelea na Zoezi la Kuhesabu kura.
 

Mhabarishaji

JF-Expert Member
Oct 5, 2010
1,005
2,000
Mahakama Kuu ya Malawi imetengua agizo la Rais Joyce Banda la kusimamisha matokeo ya Uchaguzi Mkuu. Muda mfupi baada ya Rais Banda kutangaza kwamba Uchaguzi huo utarudiwa baada ya miezi mitatu, Mwanasheria Noel Chalamanda akiwakilisha Malawi Electoral Commission (MEC), na Mwanasheria Patrick Mpaka wa Malawi Law Society, walikimbilia Mahakamani. Mahakama Kuu imesema kulingana na Katiba ya Malawi, Rais Banda hana mamlaka ya kutengua Uchaguzi Mkuu, na imeitaka MEC kuendelea kutoa matokeo ya Uchaguzi Mkuu.
 

Zamaulid

JF-Expert Member
May 25, 2009
17,883
2,000
aiss!soon wanaweza anza kunyukana,inabidi tu mama akubali yaishe hata kuwa wa kwanza kupoteza!!
 

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,745
2,000
Nilitaka kushangaa hawa jamaa wanasheria za aina gani kama mgombea anauwezo wa kuahirisha uchaguzi. La kuhama chama ukiwa rais lilinishangaza hili la huyu mama nalo liliniacha hoi.
 

Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,534
2,000
Nilitaka kushangaa hawa jamaa wanasheria za aina gani kama mgombea anauwezo wa kuahirisha uchaguzi. La kuhama chama ukiwa rais lilinishangaza hili la huyu mama nalo liliniacha hoi.

Huyu mama sijui u dokta wake ninwa nini..hana akili kabisa...yaani ni kama udokta wa mrema au maji marefu
 

RockSpider

JF-Expert Member
Feb 16, 2014
6,865
1,500
Mahakama Kuu ya Malawi imetengua agizo la Rais Joyce Banda la kusimamisha matokeo ya Uchaguzi Mkuu. Muda mfupi baada ya Rais Banda kutangaza kwamba Uchaguzi huo utarudiwa baada ya miezi mitatu, Mwanasheria Noel Chalamanda akiwakilisha Malawi Electoral Commission (MEC), na Mwanasheria Patrick Mpaka wa Malawi Law Society, walikimbilia Mahakamani. Mahakama Kuu imesema kulingana na Katiba ya Malawi, Rais Banda hana mamlaka ya kutengua Uchaguzi Mkuu, na imeitaka MEC kuendelea kutoa matokeo ya Uchaguzi Mkuu.
Nilimuona Mama Joy akipewa ki-note cha kwenda kumuona Mzee Kingunge siku ile ya Military Showcase 26/04/2014!!! kwa haraka haraka sikuweza kukonnect dot!... kazi imeanza...
 

Mhabarishaji

JF-Expert Member
Oct 5, 2010
1,005
2,000
Saafi sanaaaaaaaa

Mahakama Kuu ya Malawi ni Mahakama iliyo huru kwelikweli. Tume ya Uchaguzi ya Malawi (MEC), nayo ni Tume huru kwelikweli. Lini Tanzania tutafikia kuwa na Mahakama huru, na Tume huru kiasi hiki? Safari bado ni ndefu!!! Mungu ikumbuke Tanzania!
 

Mto

Senior Member
Sep 6, 2011
170
170
Viongozi wengi wa kisiasa Afrika ambao wapo madarakani wanapoingia katika uchaguzi huwa wanafikiria jambo moja tu, kushinda. Wengi hawajiandai kisaikolojia wakijua kuwa kuna kushinda au kushindwa. Ikitokea wakashindwa ndo hivi, wengine wanaamua kujiua, wengine wanakufa kwa presha, na wengine ndiyo hivi kama huyu mama wanatapatapa kuukataa ukweli kuwa wameshindwa katika uchaguzi husika. Wanasiasa jiandaeni kisaikolojia mnapoenda kwenye chaguzi; jueni kuwa kuna kushinda na kushindwa!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom