Ukistaajabia ya musa utayaona ya filauni,sasa nimeanza kuamini usemi huu! Jamani tanzania nchi yangu ina vituko vilivyo pitiliza! Mkuu wa shule ya sekondari ya kata iitwayo ndalibo sekondari anaeitwa lucas masanzu anawaumiza vichwa viongozi wa elimu walayani kongwa mkoani dodoma kwa mambo yake yafuatayo!habari za kuamini kutoka kwa wasamalia wema eneo inapopatikana shule na nilizozithibitisha mimi kwanjia zangu na pia zisha andikwa gazetini mwezi mmoja uoputa zinatiririka kama ifuatavyo!!!kwanza kabisa alikula pesa za wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka wa jana ilingulika baada ya matokeo kutoka kwa mara ya kwanza kabla ya kufutwa na serikali,baadhi ya wanafunz waliandamana hadi shuleni wakiwa na wazazi wao,alipobanwa sana alikri makosa na kuahidi kulipa fedha hizo baraza la mitihani tena na faini juu kwa mujibu wa baraza la mitihani pindi matokeo yanapo kuwa yametoka!huyo mkuu wa shule alilipa na matokeo yakatoka!! Kali kuliko yote iliyonifanya nilete huu uzi ni hii hapa!viongozi wa elimu walipo fanya utafiti waligundua kuwa amekula tena pesa za ada za kidato cha nne wa mwaka wanaotarajia kufanya mtihani safari. hii amekula na wale wa kidato cha pili alipoulizwa alijibu kama alivyotaka tena kwa ujasiri! Chakushangaza zaidi alipo letewa barua ya kuondolewa ukuu wa shule aligoma na kukataa kukabidhi ofisi kwa mkuu mpya,wiki iliyopita viongozi wa elimu mara mbili walienda shuleni hapo bila ya mafanikio tena wakiwa na mkuu mpya!raia wanajiuliza anategemea nini kama anaweza kufanya hivyo mkuu huyo mwenye diploma tu ya ualimu?pia viongozi watafanyaje tena?wataenda tena kumtoa au ndo wameshindwa na mtu huyo anaeweza kumjibu mwajiri wake apendavyo!NAIPENDA NCHI YANGU TANZANIA NAWACHUKIA VIONGOZI WEZI!!