Mkuu wa Shule akamatwe kwa mauji

Mkuu wa Shule akamatwe kwa mauji

7ecccb96872951815825eaeb6de9f5bb.jpg
 
Tena inasemekana ilitakiwa magari matatu lakini yeye akaforce moja
Jamani kuweni na akili. Na kama huna taarifa kaa kimya. Magari yameenda Matata. Dereva wa kwanza alifikisha gari salama la pili ndo hilo la tatu halikupata ajali unataka mkuu ashtakiwe pumbafuuu.
Waliokufa ni 33 waliopona 3 hiyo 40 unaitoa wapi. Mbona wanafiki mnatupotezea muda!
 
Jamani kuweni na akili. Na kama huna taarifa kaa kimya. Magari yameenda Matata. Dereva wa kwanza alifikisha gari salama la pili ndo hilo la tatu halikupata ajali unataka mkuu ashtakiwe pumbafuuu.
Waliokufa ni 33 waliopona 3 hiyo 40 unaitoa wapi. Mbona wanafiki mnatupotezea muda!
Ndo kazi iliyobaki mkuu kwa sasa kwetu sisi waTz uongo kila mtu ni mchambuzi wa mambo.
Fitina
Majungu
Uongo
Unafiki
Ndo vimejatujaa
 
Mkuu acha ushabiki usokuwa na maana ajali aijasababishwa kwa wingi wa wanafunzi na idadi aikuwa 40 kama unavyotaka kuaminisha umma
 
Naona yote yaishe..chukulia mfano wa mwendokasi..inaruhusiwa kubeba watu wangapi ila huwa zinabeba mara 4 ya abiria wanaotakiwa level seat..kama ni kuzuia tatizo tuanze na dala dala zetu akiwemo baba yao mkuu mwendokasi..ndio tutaponya tatizo
 
Wa.tz tuache dhana ya unafiki...mtoa maada anza na dala dala na mwendokasi...
 
Huu ulioandika ni upumbavu unaonyesha huna uchungu hata kidogo na yaliotokea bali furaha yako ni ubaya kwa ubaya,gari zilikuwa 3 na wasimamizi na waratibu walikuwa ni waalimu husika, ningekuona unaakili ungeniambia askari wa usalama barabarani waliokuwepo zamu ambapo gari lilipita wawajibike kutokagua gari, hata hivyo hii ni ajali imetokea bahati mbaya hakuna wa kumlaumu Bali ni vema tuchukue tahadhari juu ya ukaguzi wa magari yanayobeba watoto mengi huwa ni mabovu sana kwa vile hayakaguliwi na ysmepigwa rangi kuonekana mazuri
 
Dereva ndio ana maamuzi ya mwisho kuhusu chombo chake. Ndiye mwenye leseni na anawajibika kwa yaliyotokea.

Mkuu wa shule au mmiliki hawahusiki moja kwa moja
 
Huu msiba umetuumiza watu wote hasahasa ndungu wa karibu lakini kuanza kulaumu watu pasipo uthibitisho kwamba wametolewa kafara sijui free mason sijui mkuu wa shule hii haisaidi bali itajenga chuki na kuzidisha machungu kwa waliofiwa ambayo labda ingeepukika kama watu wangekaa kimya na kuomboza juu ya hawa watoto
 
Mtoa post jaribu kufikiri. majinja bus nayo iliua watu wengi tu. utamlaumu mwenye gari au readily. Tuwaombee wanetu
 
Mkuu wa shule hana makosa. kumbuka waleni watoto siti za watu wazima wanaweza kaa ata wa3. Ishu ata mkimshitaki au kumfunga watoto wamehsapoteza maisha.

Nafikili ata dereva alijitahidi ila ikamshinda maana ajali nyingi dereva huwa anapona.
Uchakavu wa magari kwa shule zetu nao pia unachangiwa kama shule ya St.Mary Mbagara kuna gari ya aina ya mchina yaani gari ni bovu kabisa na lilegari linabeba watoto wengi mno. Wajifunze jamani kwa haya yaliyotokea inauma sana.
 
Mtoa hoja ukisema ivo unakosea sana katika kipindi hiki kigumu kwani kipindi hiki sio cha kulaumiana,bado tupo katika dimbwi LA mojanzi
 
Mkuu wa shule ya Lucky Vincent ashitakiwe kwa kosa LA kusababisha mauaji baada ya kuruhusu Gari ya kubeba abiria 28 ibebe abiria 40. Bila uzembe wa Huyu Mkuu, idadi ya marehemu ingekuwa ni ndogo. Polisi wamshughulikie kikamilifu
Sasa hapo wewe ndiyo wa kwanza kuona hili tukio kwa macho mapana, wengi wetu baada ya pole tunakimbilia ya ajabu kama kwenda kwa babu, mungu kapenda, mungu kataka n.k.
Ajali karibu zote hapa nchini zasababishwa kabisa na sisi wenyewe, kubeba watu au mizigo zaidi, ulevi, kwenda kasi, barabara mbovu au zisizo na kinga pembeni, kutokuwa na ishara muhimu barabarani, madereva kutokupenda kutii sheria huku wakishangiliwa na kuachwa wafanye watakalo na abiria, hata kama wanavunja sheria zote hizi..
TUBADILIKE, SIO KILA AJALI MUNGU KAPENDA AU KUTAKA, TUJIANGALIE KAMA TWAFATA SHERIA ZA BARABARANI, SISI NA WAHUSIKA...PERIOD
 
Mkuu wa shule ya Lucky Vincent ashitakiwe kwa kosa LA kusababisha mauaji baada ya kuruhusu Gari ya kubeba abiria 28 ibebe abiria 40. Bila uzembe wa Huyu Mkuu, idadi ya marehemu ingekuwa ni ndogo. Polisi wamshughulikie kikamilifu


Vilevile askari wa usalama barabarani wote waliokuwa kwenye hiyo njia nao wanahusika
 
Basi na trafick nao wakamatwe kwa kushindwa kuwazuia barabarani. Sioni kosa kwa mkuu wa shule
 
Mkuu wa shule ya Lucky Vincent ashitakiwe kwa kosa LA kusababisha mauaji baada ya kuruhusu Gari ya kubeba abiria 28 ibebe abiria 40. Bila uzembe wa Huyu Mkuu, idadi ya marehemu ingekuwa ni ndogo. Polisi wamshughulikie kikamilifu
hakuna criminal responsibility hapo mkuu labda ungesema dereva ambaye tayari ameukumiwa na ajari.
 
Huyo mkuu wa shule ndo aliruhusu abiria 40 wapande basi yenye uwezo wa kubeba abiria 28?

Na kama idadi ya abiria si sababu ya hiyo ajali, kwa nini akamatwe?
Gari hilo inasemekana, viti vyake havikuwa na mikanda(Sijalidhibitisha hili nasubiri taarifa kamili).
 
Back
Top Bottom