Mkuu wa Mkoa wa Tanga afunga maduka na masoko!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuu wa Mkoa wa Tanga afunga maduka na masoko!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dark City, Apr 16, 2011.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ndugu wana JF,

  Katika safari zangu za kutembelea jiji la Tanga, nimekumbana na kitu ambacho sijakielewa kabisa. Nilipokuwa nazunguka mjini leo asubuhi, nimeshangaa kuona maduka yote na sehemu muhimu za huduma kama masoko zikiwa zimefungwa. Nilipouliza nikaambiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mej Mstaafu Said Kalembo ametoa amri (kupitia barua ambayo sikubahatika kuiona) kwamba sehemu zote hizo zifungwe siku ya leo (16 Aprili 2011) kuanzia asubuhi hadi saa 6.00 mchana ili watu wafanye usafi wa maeneo yao. Hata maduka ya dawa nayo pia yamefungwa.

  Naomba wajuzi wa sheria na mambo ya utawala waniambie kama Mkuu wa mkoa anayo mamlaka kama hayo kisheria. Nimeongea na wakili mmoja wa hapa Tanga akanambia kuwa kuna kitu kama by-laws kimetumika ila akakikiri kuwa hajaiona hiyo sheria ndogo wala kupata undani wake. Pia jamaa mmoja aliyekuwa amekwazwa kama mimi kampigia simu mwanasheria wa jiji ambaye kajibu kuwa mkuu wa mkoa ametumia penal code (sina hakika na spellings) au kanuni za adhabu kutoa amri hiyo.

  Ndugu zangu nimekwazika sana na hali hii na naomba mnisaidie kwa michango yenu.

  DC
   
 2. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yule jamaa na mbabe sana lkn waache watu wa tanga wanapenda sana ccm. Hayo ndio mafao yao. Achana nao wale huwawezi hata ukiwafahamisha hawaelewi.
   
 3. K

  KWELIMT Member

  #3
  Apr 16, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mi sioni tatizo kama nia ya RC ni nzuri,walifunga hvyo hivyo enzi za chama kimeshka hatamu sembuse leo?ACHA WAFANYE USAFI MAANA KIPINDUPINDU NI HATARI KULIKO HUKO KUFUNGWA KWA MUDA.
  Pia sisi watz hadi tusimamiwe kwani maeneo hayo najua kuna diwani kwa nini wananchi wasimbane ili nae aibane halmashauri? Vilele RC alitakiwa afuate ngazi za kiutawala,eneo hilo lina DC,Mkurugenzi na Diwani hata serikali ya mtaa.KWANINI HAJAWA CHUKULIA HATUA HAO VIONGOZI ILI WAWAJIBIKE?
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  wafanye usafi bana , kikpiga kipindupidu hapao si watu watatafutana
   
 5. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  DC ,

  Nothing wrong with that Sir!!

  Can you tell me what is the alternative way to make people clearn their own compouds ...in our local streets!!?
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Nashukuru sana mkuu.

  Binafsi sina tatizo na nia ya RC. Tatizo langu ni kama sheria inampa mamlaka ya kufanya hilo alilolifanya. Kwani tukiendekeza mambo ya nia nzuri tunaweza kuleta mtafaruku siku moja. Hivi siku moja akiamua kuwa wanaume wakorofi wanyang'anywe wake zao utakubaliana naye?
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kwani usafi usingeweza kufanyika bila kufunga maduka?
   
 8. TONGONI

  TONGONI JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 1,027
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hiyo ya watu wa-Tanga wanapenda chama gani haihusu, hapa tuna hoji uhalali wa mkuu wa mkoa kutoa amri ya kufunga maduka
  na uhalali wa kuitekeleza amri yake,na hata kama watu wa Tanga ni ccm tusiwachukie na kuwatenga kwa kauli za "achana nao" kama lengo ni kuwakomboa wa-Tanzania mikononi mwa madhalimu basi tutafute namna ya kuwashawishi na kuwafanya wakubali sera za chama ukitakacho. Tukitengana kwa vyama,tutatengana kwa dini,makabila nk then hatutokaa salama....Yalikwisha semwa JF sio kwa ajili ya watu fulani ni kwa ajili ya wote kikubwa tufuate maadili na tupendane.
   
 9. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #9
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,823
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Ni sawa kabisa kufanya hivo na RC ana mamlaka yote kama ilivyoainishwa kwenye katiba,,kuna sheria ndogo ndogo ( by laws) zinatungwa katika maeneo husika hizo zina nguvu sawa kama sheria mama katika suala husika ila zikipingana na sheria mama ndio kuna tatizo...usafi mhimu
   
 10. Big One

  Big One JF-Expert Member

  #10
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 759
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  dah hcho kidingi kitemi hakina lolote we usafiiiii kwann hawawez kufanya maduka yakiwa waz achen hzo sheria sheria mama na sheria baba ipo wap?mnatetea ujinga kama m2 anafanya bidhaa za kuoza apate hasara yan aliyemteua kachemka saaannaaaah
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Safi sana Mkuu,

  Hiyo ndo hoja yangu haswa! Hatuwezi kuendesha nchi kwa hisia na utashi binafsi. Lazima tufuate taratibu na sheria. Mimi bado nasubiri watu wanipatie ufafanuzi unaosimama katika sheria na si ushabiki au chuki!
   
 12. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Tunaomba ututendee haki kwa kutupatia vifungu vya katiba vinavyompa mamlaka RC kusimamisha shughuli za raia kwa muda wa zaidi ya masaa 6. Pia utatundea haki zaidi ukitumabia kama hizo by-laws zipo pale Tanga na ikiwezekana ukaweza nakala hapa.
   
 13. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu sio bidhaa za watu kuoza tu, bali amesimamisha na kukwamisha shughuli za watu kwa kiasi ambacho labda kikikotolewa hasara yake haiwezi kulingana na gharama za huo usafi. Hebu fikiria kama kuna mtu angekuwa amesafiri kuja Tanga kununua bidhaa ili aweze kuwahi gulioni leo. Huyo mtu hawezi tena kwani hadi saa 6 maduka mengi ya wahindi na wafanyabiashara yatakuwa yamefungwa na labda hayatafunguliwa tena hadi Jumatatu. Hasara aliyopata huyu mtu itafidiwa na nani? Pia loss aliyopata huyo mfanyabiashara ambaye hakufungua duka itafidiwaje?
   
Loading...