Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,563
- 21,665
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, ameagiza kurudiwa upya kwa zoezi la uhakiki la kubaini watumishi hewa katika mkoa wa Mwanza, ikiwa ni mpango wa kubaini wale wote wanao lipwa mishahara bila kufanya kazi.
Mongella ameunda kamati ya watu saba katika kila halmashauri ambao watahakiki watumishi ambao wapo kazini pamoja na kupitia 'payrol' za wafanyakazi, zoezi lililo fanyika awali mkoa huo ulibainika kuwa na watumishi hewa wapatao 334.
”Tunataka kwenda kufanya uhakiki wa mtu kwa mtu (physical), popote pale walipo warudi wahakikiwe labda kama yupo masomoni nje ya nchi."
Ameagiza wale wote walioko masomoni, likizo au safari warudi mara moja kwenye vituo vyao vya kazi kwa ajili ya zoezi la uhakiki, huku akiwataka wote watakao kwenda kwa ajili ya kuhakikiwa waende wakiwa na picha tatu za passport size, ambapo taratibu zakuweka kumbukumbu sahihi zitafanyika
Tunataka zoezi hili lichukue muda wa siku saba tu na baada ya hapo tutatoa ripoti kamili, tusishangae kuona idadi hiyo ikiongezeka au kupungua kwani katika uhakiki huu naamini tutapata majibu sahihi " alisema Mongella.
Aidha Mongella amewataka waandishi wa habari kumpa ushirikiano ili waweze kuufanya mkoa wa Mwanza kuwa sehemu nzuri kiuchumi na kitalii na kimaendeleo.