Mkuu wa Mkoa wa Mbeya atangaza Dau la Mil. 5 kwa atakayempata Esther Noah Mwanyilu

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Sep 13, 2020
3,166
4,581
1687518265978.png

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera ametangaza dau la milioni tano kwa yeyote atakaye fanikisha kupatikana kwa mwanafuunzi wa kidato cha tano Esther Noah Mwanyilu wa shule ya Sekondari ya Pandahill aliyetoweka shuleni Mei 18/2023

Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya waziri Mkuu Kasimu Majaliwa kuiagiza ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kufuatilia sakata la kupotea kwa Mwanafunzi huyo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Joseph Kusaga amesema juhudi za kumtafuta zinaendelea ikiwa ni pamoja na kuwahoji wale wote aliwataja kwenye ujumbe aliocha kabla ya kuondoka.

Pia soma: Mkuu wa Mkoa Mbeya, Juma Homera: Kama kuna mtu yupo na mwanafunzi wa shule ya Pandahill, Ester Noah Mwanyilu ni vyema akamuachia
 
Hadi anatangaza dau hili maanayake juhudi za kumtafuta zimegonga mwamba, wakati yeye ndie mkuu wa ulinzi na usalama mkoani....🤨
By the way, hiyo pesa imetoka kwenye fungu gani la RC...🙄
Achana na habari ya Fungu zingatia umuhimu wa kupatikana binti, Ingekuwa ni Mtoto wako ungeuliza hili swali?
 
Achana na habari ya Fungu zingatia umuhimu wa kupatikana binti, Ingekuwa ni Mtoto wako ungeuliza hili swali?
RC ndio mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama hapo mkoani, yeye anapo tangaza hili dau kwetu sisi makapuku tunaelewa nini??
Yes, mimi ni mzazi na kweli inaumiza sana panapo tokea mambo kama hizi kwenye familia.
 
Back
Top Bottom