Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,703
- 218,247
Taarifa zilizoibuliwa leo nje ya Mahakama kutoka kwa Mawakili waliopeleka kesi ya Mkataba mbovu wa Bandari , wamemtaja wazi wazi Mkuu wa Mkoa huo Juma Homera kwamba hafai kuongoza Mkoa wa Mbeya kwa vile anaamini Ushirikina.
Wamesema kitendo cha RC huyo kuwataka machifu na Waganga wa Mbeya kuwaloga Wanasheria wanaosimamia kesi hiyo kinachoenda sambamba na RCO wa Mbeya kuwakamata atakavyo na kuwadhalilisha Wazalendo wote wanaopambania Rasilimali za Nchi hakipaswi kufumbiwa macho maana kinaweza kuleta Maafa.
Wanashangaa kwanini Homera anaachwa pamoja na kwamba ameanza ushirikina siku nyingi tangu akiwa Katavi, ambapo kumbukumbu zinaonyesha kwamba, Wakati wa Ugonjwa wa Korona alikusanya Waganga na Wachawi Ofisini kwake akiwalazimisha watengeneze dawa ya Korona ili yeye apate sifa kutoka kwa Magufuli.
Binafsi kama mtu wa Mbeya naunga mkono RC huyo kung'olewa kwa vile anatia aibu , Mbeya inahitaji RC wa kisasa anayeamini katika Sayansi badala ya uchawi wa kuloga watu , muda wa kuamini uchawi ulishapita na ni Aibu kwa kijana kama Homera kudhani ushirikina utamsaidia chochote.