#COVID19 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya amesema Chanjo itakwenda nyumba kwa nyumba

K
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera ametangaza kuanza utoaji wa chanjo ya Uviko 19 nyumba kwa nyumba, kitanda kwa kitanda na katika nyumba za ibada kuazia kesho Jumamosi Septemba 25, 2021.

Homera ametoa msimamo huo leo Ijumaa Septemba 24, 2021 kwenye kikao cha wadau cha uhamasishaji wa chanjo kwa wananchi mkoani Mbeya.

Amesema wamefikia uamuzi huo kwa sababu Mkoa ulipokea chanjo 50,000 lakini mpaka sasa waliopata chanjo ni 10,000 jambo ambalo halikubaliki huku Serikali ikiwa imetumia gharama kubwa kwa lengo la kuokoa uhai wa Watanzania

"Zoezi la utoaji chanjo ya Uviko 19 ni nyumba kwa nyumba ,kitanda kwa kitanda kwa kuwashirikisha watendaji wa ngazi za kata na vijijini kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa na jamii kupata chanjo dhidi ya ugonjwa wa uviko 19 ingawa sio lazima lakini itabidi iwe hivyo,"amesema.

Mwakilishi wa Wizara ya Afya, Dk Baraka Nzobo amesema jamii inapaswa kutambua chanjo hiyo haina madhara kwa binadamu na kwamba inasaidia kupunguza vifo na maambukizi ya Uviko 19.

"Ni hofu tu imejengeka miongoni mwa jamii na tafsiri tofauti juu ya kinga hiyo hivyo niungane na mkuu wa mkoa kwa kuanza kwa zoezi la nyumba kwa nyumba ,kitanda kwa kitanda ili kufikia malengo ya serikali ya chanjo zikizotolewa katika kila mkoa."amesema.

Mkazi wa Forest, Saada Abdalla amesema msimamo huo wa Homera ni sahihi kwani jamii imekuwa ikiona chanjo hiyo ni kama sumu jambo ambalo linachangia kuwepo kwa vifo vitokanavyo na Uviko 19 na kuwepo kwa changamoto ya vifaa hususan oksijeni kwenye hosptali zetu nchini.

Mwananchi
Kwa hiyo sio hiyari tena?Huyu mkuu wa mkoa ,INA maana ya hiyari haijui?
 
I wonder. Hili ni wazo la serikali au mtu binafsi.
1. Kama ni wazo la serikali Je serikali inalazimishaje kitu ambacho ime declare kutokuwa responsible Kwa any side effects.

2. Kama ni wazo la Mtu binafsi yaani wazo lake namshauri Mh azingatie kipengele hicho juu atabaki salama.

3. Pia hao washauri wa mkoa. Mshaurini upya Mh. Kuhusu hili suala, it's not all about data kwamba eti mkoa wako umechanja wangapi. Fuateni Maelekezo ya serikali, hamasisheni watu wakachanje Kwa hiyari until further government instructions.

4. Pia hao watendaji wasikurupuke, wacheki na mkurugenzi wao ikishindikana hata tamisemi. Wapate written document ya Maelekezo kutoka serikalini kwamba Sasa chanjo ni lazima na ikiwa na Maelekezo watakaokaidi wachukuliwe hatua gani, ili kila Mtendaji Sasa Apime uzito na aamue mwenyewe. Wazingatie hii ni serious issue inayohusu afya za watu sio Jambo la kukurupuka namna hiyo na wakumbuke Maelekezo yaliyopo kwenye maandishi sasa kutoka serikalini ni Kuwa chanjo ni hiyari. Hivyo wajue likitokea lolote wataulizwa walitenda Kwa Maelekezo ya maandishi kutoka serikali ipi.

Narudia tena hao watendaji wazingatie hili. Nadhani wapo humu watasoma.
 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera ametangaza kuanza utoaji wa chanjo ya Uviko 19 nyumba kwa nyumba, kitanda kwa kitanda na katika nyumba za ibada kuazia kesho Jumamosi Septemba 25, 2021.

Homera ametoa msimamo huo leo Ijumaa Septemba 24, 2021 kwenye kikao cha wadau cha uhamasishaji wa chanjo kwa wananchi mkoani Mbeya.

Amesema wamefikia uamuzi huo kwa sababu Mkoa ulipokea chanjo 50,000 lakini mpaka sasa waliopata chanjo ni 10,000 jambo ambalo halikubaliki huku Serikali ikiwa imetumia gharama kubwa kwa lengo la kuokoa uhai wa Watanzania

"Zoezi la utoaji chanjo ya Uviko 19 ni nyumba kwa nyumba ,kitanda kwa kitanda kwa kuwashirikisha watendaji wa ngazi za kata na vijijini kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa na jamii kupata chanjo dhidi ya ugonjwa wa uviko 19 ingawa sio lazima lakini itabidi iwe hivyo,"amesema.

Mwakilishi wa Wizara ya Afya, Dk Baraka Nzobo amesema jamii inapaswa kutambua chanjo hiyo haina madhara kwa binadamu na kwamba inasaidia kupunguza vifo na maambukizi ya Uviko 19.

"Ni hofu tu imejengeka miongoni mwa jamii na tafsiri tofauti juu ya kinga hiyo hivyo niungane na mkuu wa mkoa kwa kuanza kwa zoezi la nyumba kwa nyumba ,kitanda kwa kitanda ili kufikia malengo ya serikali ya chanjo zikizotolewa katika kila mkoa."amesema.

Mkazi wa Forest, Saada Abdalla amesema msimamo huo wa Homera ni sahihi kwani jamii imekuwa ikiona chanjo hiyo ni kama sumu jambo ambalo linachangia kuwepo kwa vifo vitokanavyo na Uviko 19 na kuwepo kwa changamoto ya vifaa hususan oksijeni kwenye hosptali zetu nchini.

Mwananchi
Kesho ni siku ya mapumziko ya familia, nitakuwa nyumbani kwangu hapa Soweto Mbeya, sasa nione huyo atakayekuja kwangu eti kulazimisha Mimi au familia tuchanje kwa nguvu, yaani tusije kulaumiana.

Mimi na familia yangu tulishaamua badala kutumia haya machanjo chanjo yasiyokuwa na guarantee yoyote, tuimarishe mifumo ya kinga ya mwili kwa ulaji wa vyakula maalum na mchanganyiko wa herbs maalum zinazotokana na viungo, mizizi na matunda kama tulivyopata formula yake kutoka kwa watalaam wa NIMR kipindi cha JPM, na tume_ survive phase zote ngumu kuanzia mlipuko wa kwanza hadi sasa, na imeonyesha matokeo ya uhakika compare na haya madubwasha ya tunayotupiwa huku Afrika.

Sasa nione huyo mtu atakayekanyaga kwangu hiyo kesho kunilazimisha upuuzi wowote, Ebo.

Kama hiyo michanjo imewadodea na wanataka ku_retire imprest ya hao mabeberu watafute njia nyingine, siyo kukanyaga hapa kwangu.
 
Watakuwa wameichoka amani..kumlazimisha mtu chanjo ni sawa na kumlazimisha mtu kula sumu ya panya..ama ameshaichoka hiyo nafasi. Huo ukanda wa nyanda za juu kusini uliwahi kumuua mkuu wa mkoa bwana kleruu enzi za nyerere..pengine historia inataka kujirudia.
 
Zishawadodea, waliochanja ni 10,000 (idadi ya mwanasiasa).
10000 ya mwanasiasa ni sawa na 1000.
Mpaka sasa mbeya waliochoma ni buku moja.

Hesabu ya serikali ya kisiasa
Waliochoma mpaka sasa ni laki tatu ya kisiasa ambayo ni sawa na laki 1.
Kama mark mwandosya kachoma basi idadi inaweza kufika hiyo ya 1000, kama hajachoma ujue hata 500 hawafiki.
 
wakitaka kupata watu wengi wa kuchanja watangaze tu kila anayechanjwa atapewa sahani ya ubwabwa na soda moja.

hii itafanikiwa sana kwasababu waTZ wengi wanafikiria kwa kutumia matumbo.
Usiniambie kuwa hata hichi ulichokiandika hapa ulitumia tumbo kwanza kufikiri.
 
Swala la chanjo ya COVID 19 linawafanya waTz kuwa wafuaei wa JPM kwa Corona ni Futaaaa tu ukijichesha linayeyuka,.
Wengi wanamuenzi Jpm mioyoni na kumkana midomoni.

Wote wanakuwa Sukuma gang
 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera ametangaza kuanza utoaji wa chanjo ya Uviko 19 nyumba kwa nyumba, kitanda kwa kitanda na katika nyumba za ibada kuazia kesho Jumamosi Septemba 25, 2021.

Homera ametoa msimamo huo leo Ijumaa Septemba 24, 2021 kwenye kikao cha wadau cha uhamasishaji wa chanjo kwa wananchi mkoani Mbeya.

Amesema wamefikia uamuzi huo kwa sababu Mkoa ulipokea chanjo 50,000 lakini mpaka sasa waliopata chanjo ni 10,000 jambo ambalo halikubaliki huku Serikali ikiwa imetumia gharama kubwa kwa lengo la kuokoa uhai wa Watanzania

"Zoezi la utoaji chanjo ya Uviko 19 ni nyumba kwa nyumba ,kitanda kwa kitanda kwa kuwashirikisha watendaji wa ngazi za kata na vijijini kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa na jamii kupata chanjo dhidi ya ugonjwa wa uviko 19 ingawa sio lazima lakini itabidi iwe hivyo,"amesema.

Mwakilishi wa Wizara ya Afya, Dk Baraka Nzobo amesema jamii inapaswa kutambua chanjo hiyo haina madhara kwa binadamu na kwamba inasaidia kupunguza vifo na maambukizi ya Uviko 19.

"Ni hofu tu imejengeka miongoni mwa jamii na tafsiri tofauti juu ya kinga hiyo hivyo niungane na mkuu wa mkoa kwa kuanza kwa zoezi la nyumba kwa nyumba ,kitanda kwa kitanda ili kufikia malengo ya serikali ya chanjo zikizotolewa katika kila mkoa."amesema.

Mkazi wa Forest, Saada Abdalla amesema msimamo huo wa Homera ni sahihi kwani jamii imekuwa ikiona chanjo hiyo ni kama sumu jambo ambalo linachangia kuwepo kwa vifo vitokanavyo na Uviko 19 na kuwepo kwa changamoto ya vifaa hususan oksijeni kwenye hosptali zetu nchini.

Mwananchi
Serikali yenyewe iliyoingia gharama imesema ni hiari, sasa yeye ndio anajifanya anakichwa kikubwa kuliko serikali??!!! Hawa watu sikui huwa wanaokotwa wapi (apart from Jalalani)
 
Kuna kila dalili zile takwimu waliochoma chanjo karibu 357,000 ni kama za Uongo kwa sababu mbeya waliopata Chanjo 10,000, mkoa wa pwani ni 15,000 , Tanga nako Idadi ilitolewa tusubirie mikoa mingine
Hizi takwimu za mkoa zitakuja kuumbuwa

Watoto wa shule ya msingi wanakimbia wanapoona dalili za Chanjo je kwa watu wazima majumbani kazi ipo
 
Back
Top Bottom