#COVID19 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya amesema Chanjo itakwenda nyumba kwa nyumba

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera ametangaza kuanza utoaji wa chanjo ya Uviko 19 nyumba kwa nyumba, kitanda kwa kitanda na katika nyumba za ibada kuazia kesho Jumamosi Septemba 25, 2021.

Homera ametoa msimamo huo leo Ijumaa Septemba 24, 2021 kwenye kikao cha wadau cha uhamasishaji wa chanjo kwa wananchi mkoani Mbeya.

Amesema wamefikia uamuzi huo kwa sababu Mkoa ulipokea chanjo 50,000 lakini mpaka sasa waliopata chanjo ni 10,000 jambo ambalo halikubaliki huku Serikali ikiwa imetumia gharama kubwa kwa lengo la kuokoa uhai wa Watanzania

"Zoezi la utoaji chanjo ya Uviko 19 ni nyumba kwa nyumba ,kitanda kwa kitanda kwa kuwashirikisha watendaji wa ngazi za kata na vijijini kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa na jamii kupata chanjo dhidi ya ugonjwa wa uviko 19 ingawa sio lazima lakini itabidi iwe hivyo,"amesema.

Mwakilishi wa Wizara ya Afya, Dk Baraka Nzobo amesema jamii inapaswa kutambua chanjo hiyo haina madhara kwa binadamu na kwamba inasaidia kupunguza vifo na maambukizi ya Uviko 19.

"Ni hofu tu imejengeka miongoni mwa jamii na tafsiri tofauti juu ya kinga hiyo hivyo niungane na mkuu wa mkoa kwa kuanza kwa zoezi la nyumba kwa nyumba ,kitanda kwa kitanda ili kufikia malengo ya serikali ya chanjo zikizotolewa katika kila mkoa."amesema.

Mkazi wa Forest, Saada Abdalla amesema msimamo huo wa Homera ni sahihi kwani jamii imekuwa ikiona chanjo hiyo ni kama sumu jambo ambalo linachangia kuwepo kwa vifo vitokanavyo na Uviko 19 na kuwepo kwa changamoto ya vifaa hususan oksijeni kwenye hosptali zetu nchini.

Mwananchi
Mbona analazimisha
 
Huu upumbavu wote kaleta huyu mzenji ,kama watu awataki chanjo si uwaache ,wewe umesha timiza jukumu lako la kuleta chanjo basi
Uwoga wake. Ivi ndani ya miaka mitano iliyopita UNGA hawakukutana New York kweli Mana mtangulizi wake hajavuka bahari.
Yeye mwaka haujaisha
 
Kama Jamii inaona chanjo hiyo ni sumu.

Mkuu wa mkoa na watu wake, wasihangaike kupita nyumba za watu.

Wawape watu elimu kwanza kua chanjo sio sumu

Ngoja wajichanganye... Kuna watu watauliwa na Raia wenye hasira kali
Ahhhh, mzee wa kula kimasihara upo hadi huku? Naonaga unasema wewe ni daktari, naomba nijifunze kitu kwako. Je chanzo hii hakijaharibika/expire ukiangalia muda iliyoletwa na mazingira ya utunzaji wake hadi sasa?
 
Suala la chanjo wananchi hawalitaki kabisa. Leo Mbunge wa Iringa Mjini Jesca alikuwa anaongea na wamachinga. Alipozungumza kuhusu chanjo, watu wote waliondoka alipokuwa anahutubia. Huu ni mtihani kwa serikali na hata huyo anayesema atapita nyumba kwa nyumba ataenda pigwa mawe tu.
 
Washukuru tu wamepiga mahesabu wakaamua kuwabana mbavu CHADEMA kipindi hiki, ila wangelipa sana kisiasa kwa u-turn walizofanya.

Mimi nashauri CHADEMA warudi dimbani, msilielie tu kuhusu Mwenyekiti wenu mkasahau kuendeleza mapambano.

Kazeni kudai KATIBA na TUME HURU YA UCHAGUZI, huku mkipiga mahesabu kuwavuruga CCM maana kuna wengi sana ndani mule wanasononeka kwa jinsi walivyotelekeza sera na misimamo ya Magufuli. Kanda ya Ziwa tu pekee mnaweza kuisambaratisha CCM.

Mkiongea lugha nzuri na ya kueleweka mnaweza kuvuna support kubwa sana.
 
Ahhhh, mzee wa kula kimasihara upo hadi huku? Naonaga unasema wewe ni daktari, naomba nijifunze kitu kwako. Je chanzo hii hakijaharibika/expire ukiangalia muda iliyoletwa na mazingira ya utunzaji wake hadi sasa?
Mkuu J&J zinahifadhika kati ya miezi nne mpaka sita.
 
Ahahaha wewe uko sawa.
Ila njaa yake ya kulinda cheo asilazimishe wananchi.
Au hakusikia kule Tegeta watu walimwambia rais hawachanjwi?
Ila kwa taarifa zilizo chini ya kapeti kuna amri inakuja kutolewa punde kwa kila mtoa huduma ama muuzaji anatakiwa awe amechanjwa.
Baadae watakuja katika majumuiko ya dini na masoko makubwa.
Time will tell
 
Washukuru tu wamepiga mahesabu wakaamua kuwabana mbavu CHADEMA kipindi hiki, ila wangelipa sana kisiasa kwa u-turn walizofanya.

Mimi nashauri CHADEMA warudi dimbani, msilielie tu kuhusu Mwenyekiti wenu mkasahau kuendeleza mapambano.

Kazeni kudai KATIBA na TUME HURU YA UCHAGUZI, huku mkipiga mahesabu kuwavuruga CCM maana kuna wengi sana ndani mule wanasononeka kwa jinsi walivyotelekeza sera na misimamo ya Magufuli. Kanda ya Ziwa tu pekee mnaweza kuisambaratisha CCM.

Mkiongea lugha nzuri na ya kueleweka mnaweza kuvuna support kubwa sana.
Upo sahihi, wananchi sasa hv wapo nusu nusu kama ulimsikia machinga mmoja akihojiwa akasema kwa uchungu huku akilia wamemkumbuka magu.
Statement za watu wakiwa katika uchungu ni uhalisia.
Na chama na demokrasia wametaitiwa kwa mwenyekiti wao na kusahau chachu ama vision wakumbuke kuwa Nelson Mandela alifungwa miaka 30 lakini mapambano ya haki nje yaliendelea
Kama vyama vya upinzani kwa sasa ndio ungekuwa muda mzuri wa kuwavuta wananchi kwa sera maana chama cha malofa wamekengeuka.
Wakiingia katika mtego wa kushangilia rais wa kwanza wa kike, wakumbuke watasimama nae 2025.
 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera ametangaza kuanza utoaji wa chanjo ya Uviko 19 nyumba kwa nyumba, kitanda kwa kitanda na katika nyumba za ibada kuazia kesho Jumamosi Septemba 25, 2021.

Homera ametoa msimamo huo leo Ijumaa Septemba 24, 2021 kwenye kikao cha wadau cha uhamasishaji wa chanjo kwa wananchi mkoani Mbeya.

Amesema wamefikia uamuzi huo kwa sababu Mkoa ulipokea chanjo 50,000 lakini mpaka sasa waliopata chanjo ni 10,000 jambo ambalo halikubaliki huku Serikali ikiwa imetumia gharama kubwa kwa lengo la kuokoa uhai wa Watanzania

"Zoezi la utoaji chanjo ya Uviko 19 ni nyumba kwa nyumba ,kitanda kwa kitanda kwa kuwashirikisha watendaji wa ngazi za kata na vijijini kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa na jamii kupata chanjo dhidi ya ugonjwa wa uviko 19 ingawa sio lazima lakini itabidi iwe hivyo,"amesema.

Mwakilishi wa Wizara ya Afya, Dk Baraka Nzobo amesema jamii inapaswa kutambua chanjo hiyo haina madhara kwa binadamu na kwamba inasaidia kupunguza vifo na maambukizi ya Uviko 19.

"Ni hofu tu imejengeka miongoni mwa jamii na tafsiri tofauti juu ya kinga hiyo hivyo niungane na mkuu wa mkoa kwa kuanza kwa zoezi la nyumba kwa nyumba ,kitanda kwa kitanda ili kufikia malengo ya serikali ya chanjo zikizotolewa katika kila mkoa."amesema.

Mkazi wa Forest, Saada Abdalla amesema msimamo huo wa Homera ni sahihi kwani jamii imekuwa ikiona chanjo hiyo ni kama sumu jambo ambalo linachangia kuwepo kwa vifo vitokanavyo na Uviko 19 na kuwepo kwa changamoto ya vifaa hususan oksijeni kwenye hosptali zetu nchini.

Mwananchi
Msilazimishe watu kuchanjwa ili serikali iendelee kuvuta mpunga kwa wahisani na bado maisha yetu magumu shilee hakuna dawati, barabara mbovu, maji safi ndio hadithi. Mbona hamhimizi KATIBA ambayo ndio kipaumbele! Tuachwe tuamue.
 
Back
Top Bottom