Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima aongoza mazishi ya mtoto wa dereva wake

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima amewaongoza mamia ya wakazi wa Musoma sambamba na watumishi wa serikali na taasisi za umma na binafsi katika mazishi ya mtoto wa dereva wake Shida Masaba, Kasobi Shida aliyefariki dunia usiku wa jumatano katika hospitali ya mkoa wa Mara.

Kasobi alifariki kutokana na majeraha ya tumbo aliyopata kutokana na ajali baada ya kuchukua gari ambalo baba yake hutumia kumuendeshea mkuu wa mkoa , Adam Malima Agosti 4 mjini Musoma.

Akitoa salam za pole Malima amemtaka dereva huyo kutokufikiria thamani ya gari hilo ambalo limeharibika kabisa badala yake amfikirie marehemu mtoto wake.

Amesema kuwa hakuna haja ya dereva wake huyo kufikiria kuhusu gari hilo na kwamba tayari serikali imeanza utaratibu wa kumpatia gari huku akisema kuwa yuko tayari kutumia hata bajaji wakati utaratibu ukifanyika ili apewe gari lingine.

Ameitaka jamii kuungana na familia ya dereva huyo katika kuomboleza na kuwafariji badala ya kuhangaika na maneno ambayo yanasemwa na kuandikwa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na tukio hilo ambapo alisema kuwa mambo mengi ya yanayosemwa hayana ukweli na kwamba huu sio muda muafaka kwaajili ya kujibu mambo hayo.

" ndugu yangu amefiwa Na mtoto wake ambaye ni mtoto wangu la muhimu kwasasa ni kuungana na familia katika kuomboleza na kufarijiana mambo mengine hayana nafasi kwasasa, gari limekwisha teketea hatuna namna kikubwa tumuombee kijana wetu apumzike kwa amani" amesema Malima

1565202586100.jpeg

1565202605769.jpeg
 
View attachment 1174887

View attachment 1174888
natoa pole kwa familia...
 
Kunaweza kuwepo changamoto kwa tukio kama hili hususani kwa muhusika ila kwenye nchi zetu za kiafrika ni sahihi kusema baadaye hatachukuliwa hatua za kinidhani?.
 
" ndugu yangu amefiwa Na mtoto wake ambaye ni mtoto wangu la muhimu kwasasa ni kuungana na familia katika kuomboleza na kufarijiana mambo mengine hayana nafasi kwasasa, gari limekwisha teketea hatuna namna kikubwa tumuombee kijana wetu apumzike kwa amani" amesema Malima

Maneno mazuri ya faraja sijui kingesemwa nini kama kijana huyo asingefariki na sijui kama kuna yeyote alitia mguu hospitali kumjulia hali
 
Back
Top Bottom