Mkuu wa Mkoa wa Arusha Azomewa na Wananchi Karatu

Jana iliwekwa taarifa ya mkuu huyu huyu kuhusu mgogoro wa arthi huko ngorongoro amepewa cha juuu kuna kitu si bure
 
Mkuu wa mkoa wa Arusha ndg Mrisho Gambo amekutana na hasira ya wananchi katika wilaya ya Karatu.Gambo amezomewa na kuachwa pekee yake mkutanoni kufuatia yeye Gambo kupuuza agizo rasmi la waziri mkuu ambaye aliagiza Pampu za matajiri wachache kuondolewa kwenye vyanzo vya maji,baadhi ya watu wakatoa mashine zao kwa hiari na wale wengine waliokaidi agizo hilo mashine zao zilitolewa kwa Nguvu na mkuu wa Wilaya kutumia jeshi la police na mashine zote zikawa zimetolewa kwenye chanzo

Na baada wiki mbili toka waziri mkuu aondoke wakajitokeza watu wengine na kurudisha mashine zao kwenye chanzo na baada ya wananchi kuona kuwa kuna kundi ambalo limekaidi agizo la waziri mkuu wakaamua kupiga mwano yaani wakapiga YOWE na wakaamua kwenda kutoa mashine zote zilizorudishwa na pia mashine hizo zote zilichomwa moto na wananchi wenye hasira kali hiyo ilikuwa jana tar 27/12/16.

Hivyo baada tukio la jana Mhe Mkuu wa Mkoa wa Arusha ndg Mrisho Gambo akaamua kuja Karatu bonde la Eyasi na wanachi wakaalikwa na wananchi walijitokeza kwa wingi sana

Mkuu wa Mkoa akaja asubuhi ya leo akifuatana na kamati ya ulinzi na usalama mkoa na wakaenda kukagua mashine zote zilizochomwa na wanachi jana lakini ikumbukwe kuwa hata leo asubuhi wananchi waliendelea kuchoma mashine zote zilizowekwa kwenye chanzo,,,

Na mkuu wa Mkoa akaanza kuhutubia akaanza Eyasi hoyeee wananchi kimya,,,,karatu hoyeeeee kimya na baada ya hapo akasema naona ni kama hamnielewi naombeni basi niwakaribishe madiwani wa kata hizi yaani kata ya Baray na Mang'ola aliuliza wapo? Wananchi wakajibu wapo basi akakaribishwa mhe Thomas Darabe diwani kata ya Baray ambaye pia ni mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya hivyo akaeleza jinsi ambavyo waziri mkuu aliagiza mashine zitolewe kwenye chanzo na pampu zote ziwekwe umbali wa mita 500 wanachi wakamshangilia sana na akakaribishwa Diwani wa mangola CCM naye akawa upande wa wanachi akashangiliwa kama mwenzake wa chadema baada ya hapo akakaribishwa mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe Taresia mahongo ndipo pale wanachi waliposimama na kuanza kupiga miluzi na kumzomea sana na mkuu wa Mkoa akaamua kumshusha jukwaani na akasema kuwa sasa yeye ataanza kuongea na akaanza kwa kusema kuwa mashine zote ni marufuku kwenye chanzo badala yake mashine ziwekwe umbali wa mita 60 hapo ndipo wananchi walipoanza kupiga kelele wakidai kuwa waziri mkuu aliagiza mita 500 leo wewe unasema mita 60 haiwezekani,, hapo wananchi waanza kusimama na kuanza kuondoka na kumwacha mkuu wa Mkoa akiwa jukwaani na ikawa ndo mwisho wa mkutano ikabidi ashuke jukwaani,,,

Sababu kubwa ambayo wananchi wanalalamikia ni kitendo cha waziri mkuu kusema Mashine ziwekwe umbali wa mita 500 toka chanzo cha maji na leo mkuu wa Mkoa kusema iwe mita 60 ,, wananchi wanaamini kuwa mkuu huyo wa mkoa anawahujumu wananchi na amepunguza hizo mita kutokea 500 za waziri mkuu hadi 60 kwa sababu ya kumpendelea mkulima mkubwa wa vitunguu ambaye pia ni mnec wa CCM ndg Daniel Awaki

Ikumbukwe kuwa hicho chanzo cha maji inategemewa na wananchi zaidi ya 20 Elfu(20,000) kwa huduma za kawaida kama kunywesha Ng'ombe na matumizi ya maji ya kawaida hivyo kitendo cha watu kuweka pampu kwenye chanzo kinawafanya wao kukosa maji

Na baada ya wananchi kumwacha mkuu wa Mkoa jukwaani ikabidi ashuke na akaagiza Madiwani wa kata ya Baray na mang'ola wakamatwe na tumejitahidi kutafuta mdhamana lakini imeshindikana police wanasema ni kwa order ya RC hivyo wanasubiri RC Gambo atoe maelekezo mengine.

Taarifa za uhakika kutoka Mangola Karatu zinasema kuwa wafanyabiashara wenye Ukwasi mkubwa wa fedha wamempa Mkuu wa mkoa fedha nyingi ili awasaidie.Rc Gambo ni miongoni mwa the most corrupt leaders in Arusha.Itakumbukwa kuwa alipewa fedha kule Loliondo,sasa Karatu.
Tabia yake hii ni aibu na fedheha kwa mteule wake yaani Mh Rais wa nchi ambaye amejipambanua kupambana na rushwa na ufisadi
Gambo=Gasho tu!!
 
Nilivyoona heading nimekuja mbio nikasahau hata kuvaa nguo za ndani, kumbe!?
 
Habari kwako ni ipi mpendwa?????????
Zipo habari nyingi zenye faida kubwa kwa nchi hii. Sidhani kama kuzomewa kwa Gambo ni Habari. Gambo ni Mtu wa kawaida hata kama ni mteule wa Rais. Kuandika kila kinachotokea ni kuonyesha chuki zisizo na maana. Tujiulize HIVI BAADA YA KUMZOMEA NI KIPI WANANCHI WAMEFAIDIKA? Hizi siasa za kipuuzi mkoani Arusha
 
Umesahau hata kwenda kwa mzee wa upako ni habari
 
View attachment 451630kwahiyo hii ndio habari? Kweli upumbavu ni hasara sana

Kwanza hiyo miradi ya maji Dr Slaa aliwapigania sana watu wa karatu alafu sasa hivi inahujumiwa na vijana wa juzi tena mi nawaita wapumbavu tu maana hata elimu yao ni ya kuunga na kubebwa na chama cha magamba.

Nonsense
Dk Slaa ndio ameondoka na Chadema yake. Daima hatuamini habari za kufikirika na kupikwa. Maana ya (inadaiwa) kwa akili yako inasimamia wapi. Upuuzi ni kuamini katika kupika uongo huku mkishindwa kufanya maendeleo.
 
Bahati mbaya hakuna anaye hoji kuhusu hoja za upande wa pili na nina hakika hakuna aliye zomea...
 
Umesahau hata kwenda kwa mzee wa upako ni habari
Ni habari tena kubwa sana Maeneo ya kinondoni Ufipa. Lakini kwa wanatambua na
Kuujua ukweli kamwe hawawezi kukubaliana na hili. Huu ni wakati wa kuijenga arusha. DHAHABU HAISHUKI THAMANI KWA KUPAKWA MATOPE.

Chadema badilikeni
 
Zipo habari nyingi zenye faida kubwa kwa nchi hii. Sidhani kama kuzomewa kwa Gambo ni Habari. Gambo ni Mtu wa kawaida hata kama ni mteule wa Rais. Kuandika kila kinachotokea ni kuonyesha chuki zisizo na maana. Tujiulize HIVI BAADA YA KUMZOMEA NI KIPI WANANCHI WAMEFAIDIKA? Hizi siasa za kipuuzi mkoani Arusha

Kwa watanzania wenye vichwa safi na salama hiyo ni muhimu kuliko habari za CNN / BBC za kukomboa Alepo or Mosul.
Mantiki siyo kuzomewa mkuu wa mkoa ila ni jinsi gani wananchi wanaweza kutaabika kwa mtu mmoja kupindisha maamuzi yanye manufaa mapana kwa jamii na yaliyotolewa na mtu mwenye dhamana kubwa kama PM kwa faida yake binafsi au genge lake dogo.
Usiwe unasoma heading tu kwa kuwa ulifundishwa kusoma bali soma kwa kuelewa kama mtu aliyeelimika. Happy New Year 2017
 
Hii nayo ni habari?
Chadema mmechoka kiakili, kimwili mpaka kimawazo. Siku zote ni watu wakufurahia utengano katika Taifa
We maku kweli unaona hii sio habari [emoji16] [emoji16] [emoji35] [emoji35]
 
View attachment 451630kwahiyo hii ndio habari? Kweli upumbavu ni hasara sana

Kwanza hiyo miradi ya maji Dr Slaa aliwapigania sana watu wa karatu alafu sasa hivi inahujumiwa na vijana wa juzi tena mi nawaita wapumbavu tu maana hata elimu yao ni ya kuunga na kubebwa na chama cha magamba.

Nonsense

Jifunze kuandika siyo alafu ni halafu
 
Mkuu wa mkoa wa Arusha ndg Mrisho Gambo amekutana na hasira ya wananchi katika wilaya ya Karatu.Gambo amezomewa na kuachwa pekee yake mkutanoni kufuatia yeye Gambo kupuuza agizo rasmi la waziri mkuu ambaye aliagiza Pampu za matajiri wachache kuondolewa kwenye vyanzo vya maji,baadhi ya watu wakatoa mashine zao kwa hiari na wale wengine waliokaidi agizo hilo mashine zao zilitolewa kwa Nguvu na mkuu wa Wilaya kutumia jeshi la police na mashine zote zikawa zimetolewa kwenye chanzo

Na baada wiki mbili toka waziri mkuu aondoke wakajitokeza watu wengine na kurudisha mashine zao kwenye chanzo na baada ya wananchi kuona kuwa kuna kundi ambalo limekaidi agizo la waziri mkuu wakaamua kupiga mwano yaani wakapiga YOWE na wakaamua kwenda kutoa mashine zote zilizorudishwa na pia mashine hizo zote zilichomwa moto na wananchi wenye hasira kali hiyo ilikuwa jana tar 27/12/16.

Hivyo baada tukio la jana Mhe Mkuu wa Mkoa wa Arusha ndg Mrisho Gambo akaamua kuja Karatu bonde la Eyasi na wanachi wakaalikwa na wananchi walijitokeza kwa wingi sana

Mkuu wa Mkoa akaja asubuhi ya leo akifuatana na kamati ya ulinzi na usalama mkoa na wakaenda kukagua mashine zote zilizochomwa na wanachi jana lakini ikumbukwe kuwa hata leo asubuhi wananchi waliendelea kuchoma mashine zote zilizowekwa kwenye chanzo,,,

Na mkuu wa Mkoa akaanza kuhutubia akaanza Eyasi hoyeee wananchi kimya,,,,karatu hoyeeeee kimya na baada ya hapo akasema naona ni kama hamnielewi naombeni basi niwakaribishe madiwani wa kata hizi yaani kata ya Baray na Mang'ola aliuliza wapo? Wananchi wakajibu wapo basi akakaribishwa mhe Thomas Darabe diwani kata ya Baray ambaye pia ni mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya hivyo akaeleza jinsi ambavyo waziri mkuu aliagiza mashine zitolewe kwenye chanzo na pampu zote ziwekwe umbali wa mita 500 wanachi wakamshangilia sana na akakaribishwa Diwani wa mangola CCM naye akawa upande wa wanachi akashangiliwa kama mwenzake wa chadema baada ya hapo akakaribishwa mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe Taresia mahongo ndipo pale wanachi waliposimama na kuanza kupiga miluzi na kumzomea sana na mkuu wa Mkoa akaamua kumshusha jukwaani na akasema kuwa sasa yeye ataanza kuongea na akaanza kwa kusema kuwa mashine zote ni marufuku kwenye chanzo badala yake mashine ziwekwe umbali wa mita 60 hapo ndipo wananchi walipoanza kupiga kelele wakidai kuwa waziri mkuu aliagiza mita 500 leo wewe unasema mita 60 haiwezekani,, hapo wananchi waanza kusimama na kuanza kuondoka na kumwacha mkuu wa Mkoa akiwa jukwaani na ikawa ndo mwisho wa mkutano ikabidi ashuke jukwaani,,,

Sababu kubwa ambayo wananchi wanalalamikia ni kitendo cha waziri mkuu kusema Mashine ziwekwe umbali wa mita 500 toka chanzo cha maji na leo mkuu wa Mkoa kusema iwe mita 60 ,, wananchi wanaamini kuwa mkuu huyo wa mkoa anawahujumu wananchi na amepunguza hizo mita kutokea 500 za waziri mkuu hadi 60 kwa sababu ya kumpendelea mkulima mkubwa wa vitunguu ambaye pia ni mnec wa CCM ndg Daniel Awaki

Ikumbukwe kuwa hicho chanzo cha maji inategemewa na wananchi zaidi ya 20 Elfu(20,000) kwa huduma za kawaida kama kunywesha Ng'ombe na matumizi ya maji ya kawaida hivyo kitendo cha watu kuweka pampu kwenye chanzo kinawafanya wao kukosa maji

Na baada ya wananchi kumwacha mkuu wa Mkoa jukwaani ikabidi ashuke na akaagiza Madiwani wa kata ya Baray na mang'ola wakamatwe na tumejitahidi kutafuta mdhamana lakini imeshindikana police wanasema ni kwa order ya RC hivyo wanasubiri RC Gambo atoe maelekezo mengine.

Taarifa za uhakika kutoka Mangola Karatu zinasema kuwa wafanyabiashara wenye Ukwasi mkubwa wa fedha wamempa Mkuu wa mkoa fedha nyingi ili awasaidie.Rc Gambo ni miongoni mwa the most corrupt leaders in Arusha.Itakumbukwa kuwa alipewa fedha kule Loliondo,sasa Karatu.
Tabia yake hii ni aibu na fedheha kwa mteule wake yaani Mh Rais wa nchi ambaye amejipambanua kupambana na rushwa na ufisadi
Hivi kosa la RC ni nini? Hizi mita 60 amesema alipoanza kuongea; kabla ya hapo alisema KARATU OYEEEE wakamnyamazia. Ni nini walichonyamazia kama alikuwa hajapingana na PM kwanza? Hawa ni watu waliopangwa na Chadema makusudi kukorofisha mahusiano ya serkali na wananchi. Sijui kama hii ndiyo njia sahihi ya kutunza dola ya Kaskazini.
 
Back
Top Bottom