Mkuu wa Mkoa wa Arusha Azomewa na Wananchi Karatu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Mkuu wa mkoa wa Arusha ndg Mrisho Gambo amekutana na hasira ya wananchi katika wilaya ya Karatu.Gambo amezomewa na kuachwa pekee yake mkutanoni kufuatia yeye Gambo kupuuza agizo rasmi la waziri mkuu ambaye aliagiza Pampu za matajiri wachache kuondolewa kwenye vyanzo vya maji,baadhi ya watu wakatoa mashine zao kwa hiari na wale wengine waliokaidi agizo hilo mashine zao zilitolewa kwa Nguvu na mkuu wa Wilaya kutumia jeshi la police na mashine zote zikawa zimetolewa kwenye chanzo

Na baada wiki mbili toka waziri mkuu aondoke wakajitokeza watu wengine na kurudisha mashine zao kwenye chanzo na baada ya wananchi kuona kuwa kuna kundi ambalo limekaidi agizo la waziri mkuu wakaamua kupiga mwano yaani wakapiga YOWE na wakaamua kwenda kutoa mashine zote zilizorudishwa na pia mashine hizo zote zilichomwa moto na wananchi wenye hasira kali hiyo ilikuwa jana tar 27/12/16.

Hivyo baada tukio la jana Mhe Mkuu wa Mkoa wa Arusha ndg Mrisho Gambo akaamua kuja Karatu bonde la Eyasi na wanachi wakaalikwa na wananchi walijitokeza kwa wingi sana

Mkuu wa Mkoa akaja asubuhi ya leo akifuatana na kamati ya ulinzi na usalama mkoa na wakaenda kukagua mashine zote zilizochomwa na wanachi jana lakini ikumbukwe kuwa hata leo asubuhi wananchi waliendelea kuchoma mashine zote zilizowekwa kwenye chanzo,,,


Na mkuu wa Mkoa akaanza kuhutubia akaanza Eyasi hoyeee wananchi kimya,,,,karatu hoyeeeee kimya na baada ya hapo akasema naona ni kama hamnielewi naombeni basi niwakaribishe madiwani wa kata hizi yaani kata ya Baray na Mang'ola aliuliza wapo? Wananchi wakajibu wapo basi akakaribishwa mhe Thomas Darabe diwani kata ya Baray ambaye pia ni mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya hivyo akaeleza jinsi ambavyo waziri mkuu aliagiza mashine zitolewe kwenye chanzo na pampu zote ziwekwe umbali wa mita 500 wanachi wakamshangilia sana na akakaribishwa Diwani wa mangola CCM naye akawa upande wa wanachi akashangiliwa kama mwenzake wa chadema baada ya hapo akakaribishwa mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe Taresia mahongo ndipo pale wanachi waliposimama na kuanza kupiga miluzi na kumzomea sana na mkuu wa Mkoa akaamua kumshusha jukwaani na akasema kuwa sasa yeye ataanza kuongea na akaanza kwa kusema kuwa mashine zote ni marufuku kwenye chanzo badala yake mashine ziwekwe umbali wa mita 60 hapo ndipo wananchi walipoanza kupiga kelele wakidai kuwa waziri mkuu aliagiza mita 500 leo wewe unasema mita 60 haiwezekani,, hapo wananchi waanza kusimama na kuanza kuondoka na kumwacha mkuu wa Mkoa akiwa jukwaani na ikawa ndo mwisho wa mkutano ikabidi ashuke jukwaani,,,

Sababu kubwa ambayo wananchi wanalalamikia ni kitendo cha waziri mkuu kusema Mashine ziwekwe umbali wa mita 500 toka chanzo cha maji na leo mkuu wa Mkoa kusema iwe mita 60 ,, wananchi wanaamini kuwa mkuu huyo wa mkoa anawahujumu wananchi na amepunguza hizo mita kutokea 500 za waziri mkuu hadi 60 kwa sababu ya kumpendelea mkulima mkubwa wa vitunguu ambaye pia ni mnec wa CCM ndg Daniel Awaki

Ikumbukwe kuwa hicho chanzo cha maji inategemewa na wananchi zaidi ya 20 Elfu(20,000) kwa huduma za kawaida kama kunywesha Ng'ombe na matumizi ya maji ya kawaida hivyo kitendo cha watu kuweka pampu kwenye chanzo kinawafanya wao kukosa maji

Na baada ya wananchi kumwacha mkuu wa Mkoa jukwaani ikabidi ashuke na akaagiza Madiwani wa kata ya Baray na mang'ola wakamatwe na tumejitahidi kutafuta mdhamana lakini imeshindikana police wanasema ni kwa order ya RC hivyo wanasubiri RC Gambo atoe maelekezo mengine.


Taarifa za uhakika kutoka Mangola Karatu zinasema kuwa wafanyabiashara wenye Ukwasi mkubwa wa fedha wamempa Mkuu wa mkoa fedha nyingi ili awasaidie.Rc Gambo ni miongoni mwa the most corrupt leaders in Arusha.Itakumbukwa kuwa alipewa fedha kule Loliondo,sasa Karatu.
Tabia yake hii ni aibu na fedheha kwa mteule wake yaani Mh Rais wa nchi ambaye amejipambanua kupambana na rushwa na ufisadi
 
Hii nayo ni habari?
Chadema mmechoka kiakili, kimwili mpaka kimawazo. Siku zote ni watu wakufurahia utengano katika Taifa
1483000934848.jpg
kwahiyo hii ndio habari? Kweli upumbavu ni hasara sana

Kwanza hiyo miradi ya maji Dr Slaa aliwapigania sana watu wa karatu halafu sasa hivi inahujumiwa na vijana wa juzi tena mi nawaita wapumbavu tu maana hata elimu yao ni ya kuunga na kubebwa na chama cha magamba.

Nonsense
 
Back
Top Bottom