Mkuu wa mkoa na Polisi wapiga marufuku M4C Kanda ya Kati

Wilbroad Slaa
Uzinduzi M4C kanda ya kati,
Baada ya Mh Freeman Mbowe kuongoza harakati
za zinduzi za M4C kanda nyingine basi Mungu
akipenda kesho Ntakuwepo pamoja na uongozi
mkuu tukiendeleza harakati za mabadiliko
zinashuka Kanda ya kati Ambayo itafanyika
Dodoma,
Viongozi makini wa kusimamia haki za wananchi
wenye uzalendo bungeni na nje ya bunge
watakuwepo kuweza kutoa elimu ya Urania,
Tutafanya seminar asubuhi saa 3 asubuhi kwa
wadau wa Chadema kanda ya kati katika ukumbi
ndani ya uwanja wa vijana AREA'C na ratiba
nyingine tutapewa na uongozi wa mkoa.
Tanzania ya nguvu ya umma na nguvu ya umma
ni sisi tujitokeze kwa wingi zaidi.
7 hours ago · Like · Share · Repor
 
jamani huo mkutano wa mwakasege unaanza kesho j.2, leo jamhuri uwanjani kuna mechi ya wabunge, hivyo basi cdm wao mkutano wao upo viwanja vya maili 2, na jana nilimuona dr slaa ameshafka tayari dodoma. Ccm waache propoganda.
 
mkuu asante kwa taarifa ila kuna vitu vinahitaji maelezo
1. Cdm hawana taarifa ya huo uwanja kutumiwa na mwakasege?
2. Mmiliki wa huo uwanja ni polisi au?
3. Mkutano wa cdm unahusika nini na bunge kuendelea?
4. Mkutano wa mwakasege hauna uhusiano na bunge kuendelea?
5.je cdm wakifanyia mkutano wao mahala pengine kwa polisi ni sawa?

haya maswali hayajibiki, Nchimbi kighaidi katoa amri.
 
na kinana je anavyo watumia wanafunzi kule moro kama condom uyo mkuu wa mkoa ni tango poli anamamlaka ya kuzuia mkutano ----- tu
 
Ati ......
attachment.php

View attachment 90672

Maskini babe Wa watu, ah!! Duniani watu jamani wabaya!! Babe Wa watu, babe huyu kipindi kile nyota yake inang'aa, Basi akisema Nape Basi si magazeti hayo, si maredio hayo, si ma-Tv, Basi kila kOna nape-nape, ah sikuizi nyota imeshafunikwa, ah.. Anatema speech lakini Hata mbu haimgusi, babe wa watu kaishia kulazake vitumbua, Hata like TANGAZO la WHO, la kufunika vyakula tulavyo alikumbuke wapi, nyota ikifunikwa shida mtindO mmoja, chezea watu.. Watu wabaya nakwambia.. Kha waleta maskhara!?
 
Wakati M4C KANDA YA KATI maandalizi yake yakiwa YAMEKAMILIKA.

Taarifa nilizosikia muda si mrefu ni kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Jeshi la polisi wamesema ole wao CHADEMA wajitokeze kiama chao watakiona.

Tayari Ulinzi mkali kuanzia usiku huu umeimarishwa huku Magari ya Kuwasha pamoja na Defender zaidi ya 100 zinaranda randa kila kona.

Sababu zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa: '' Bunge linaendelea....''

Polisi: ''....mchungaji Mwakasege amewahi UWANJA kabla ya CHADEMA...''

Source: WAPO FM.

mkuu hizi habari zio kweli maana muda huu ninapoongea na wewe wanapita na matangazo wakitangazo mkutano upo palepale
 
Mikutano ya siasa ilishakatazwa hairuhusu wakati wa kipindi cha Bunge.Nyie mnavichwa kweli.Napata wasiwasi na watu waliomo humu ndani kama wako sawa
 
cdm wanahitaji kuwa makini mno kipindi hiki kuelekea 2015, na hii ni kutokana na ccm kukwama kwa mipango yao mahsusi ya kuidhoofisha na kuivuruga cdm, na inaonekana ni mipango inayoratibiwa ndani ya chama na ushirika wa sirikali hasa kwa kulitumia jeshi la polisi, ni wakati sasa cdm kuwa wavumilivu na pia kujiepusha na migongano isiyo ya lazima na jeshi la polisi na hii ni ili kuepuka kutimia kwa mipango ya ccm
 
Mungu wangu, kama bunge linaendelea maisha yasiendelee? Kazi kweli kweli!!!!!!

Tena wasithubutu kusema bunge linaendelea , hili la sasa hivi nalo ni bunge au sehemu ya ku practice matusi....? Si waende na maji yao ya kuwasha kwa kina Serukamba?
 
Maskini babe Wa watu, ah!! Duniani watu jamani wabaya!! Babe Wa watu, babe huyu kipindi kile nyota yake inang'aa, Basi akisema Nape Basi si magazeti hayo, si maredio hayo, si ma-Tv, Basi kila kOna nape-nape, ah sikuizi nyota imeshafunikwa, ah.. Anatema speech lakini Hata mbu haimgusi, babe wa watu kaishia kulazake vitumbua, Hata like TANGAZO la WHO, la kufunika vyakula tulavyo alikumbuke wapi, nyota ikifunikwa shida mtindO mmoja, chezea watu.. Watu wabaya nakwambia.. Kha waleta maskhara!?

Hivi walikumbuka kunawa mikono? Hivi kula vitumbua na kupigwa picha nayo ni siasa? We still have a long way to go......
 
Ccm wapo mkoa wa morogoro wanafanya mikutano yao bila bughudha yoyote
 
Dodoma sio mkoa wa kufanyia majaribio...maandamano kafanyieni huko Kaskazini!Wagogo hawataki maandamano
 
Mikutano ya siasa ilishakatazwa hairuhusu wakati wa kipindi cha Bunge.Nyie mnavichwa kweli.Napata wasiwasi na watu waliomo humu ndani kama wako sawa

serukamba weee!!
ndio maana nilikuona unafakamia vitumbua vya bure
 
badala ya kupambana na umaskini wa Taifa pamoja na Deni la Taifa Wao Wanapambana Na CHADEMA....
Chadema kinapata umaarufu kutokana na uongozi mbovu wa ccm. Sasa badala ya ccm kutumia muda wao kuondoa kasoro na mapungufu ya kiuongozi, wanatumia muda mwingi na mbinu chafu kupambana na CHADEMA. Eti atahakikisha anakabidhi uongozi wa nchi 2015 kwa mwenzake wa ccm. Sio kura za wananchi zitaamua?
Utasikia eti 'hawa CHADEMA'! Unaposema CHADEMA unaongelea mamilioni ya wananchi wanaokiunga mkono.
 
Embu basi kuwe na ziara za kuwatembelea wafanya biashara wadogo, wakulima, wanafunzi, walimu mashuleni na sehemu zingine za jamii kusikiliza kero zao, kila siku mikusanyiko na wauni tu khaa, inachosha kusoma sasa mambo yaleyale kila kukicha.

Tatizo hata wakisikiliza kero zao bungeni haziwasilishwi wanapoteza muda kwa "miongozo" na kuchambua kanuni kwa lugha za kikamanda!!!
 
Back
Top Bottom