Mwaka 2018 umemalizika juzi na kwa kweli kuna Watendaji wa Serikali ya Magufuli kwa ngazi ya Mkoa waliofanya vizuri na waliofanya vibaya. Kwa tathmini yangu binafsi nimechagua RC aliyekua bora kabisa kulingana na utendaji wake wa kazi lakini pia na RC alifanya vibaya kabisa.Vigezo ni:
- Usimamizi wa kazi na miradi ya Serikali.
- Mahusiano yake na Viongozi wengine hasa wa Upinzani.
- Anavyoitumia sheria ya masaa 24/48 kwa walio chini yake.
- Lugha na kauli zake kwa Jamii.
Aliyepata alama za juu kabisa ni
Mhe. Aggrey Mwanri- Mkuu wa Mkoa wa
Tabora.
Anayefuatia hapo ni
Mhe. Anthony Mtaka- Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu.
Aliyapta alama za chini kabisa ni
Mhe. Ally Happy- Mkuu wa Mkoa wa
Iringa
Aliyefuatia kwa alama za chini kabisa ni
Mhe. Mrisho Gambo- Mkuu wa Mkoa wa
Arusha.
Karibuni kwa mjadala na maoni.