Mkuu wa mkoa ataka maiti zifufuliwe

Mkuu wa mkoa ataka maiti zifufuliwe

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,065
Reaction score
61,398
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amewataka waganga wa kienyeji maarufu kama lambalamba mkoani humo kwenda kuwafufua watu waliofariki dunia, ndipo atakapowaruhusu kuendelea na kazi yao ya kutoa uchawi.
Mh. Chalamila amesema kwamba ameamua kutoa agizo hilo baada ya wananchi kumuomba awaruhusu waganga hao kufanya kazi yao ya kutoa uchawi, jambo ambalo serikali haiamini.

“Walileta maombi maalum kuwa serikali iwaruhusu huku wakitoa ushuhuda watu hao wakitoa uchawi, kutoa baadhi ya vitu na kuponya watu, ndipo mimi niliposimama nikasema haitawezekana, nikawaambia kama mnawashukuru wanaowaponya, nitawaruhusu kwa masharti, tukutane nao mochwari katika hospitali ya rufaa ya Mbeya, wanifufulie maiti zilizopo pale, kwa ushuhuda huo nitawaruhusu kweli ni waponyaji katika ulimwengu wa roho”, amesema Chalamila.

Mh. Chalamila aliendelea kwa kusema kwamba iwapo watu hao wataweza kufanya kazi zao kisayansi yenye kuleta manufaa, hatosita kuwaruhusu kuendelea kufanya shuhuli zao zenye imani ya kishirikina.

"Mimi nataka kwa sayansi, wakinisaidia hilo nitawaruhusu, kwa mfano mtu anataka kuwahi Dar es salaam wakanionyesha nitakubali, au walete mvua wakati wa kiangazi tumwagilie mazao yetu, wanaopotea waseme wako wapi, mimi nataka hilo”, amesema Mh. Chalamila.
 
Serikali iwaruhusu tu maana uchawi ni utamaduni uliopo duniani kote na hata viongozi mbalimbali wanauamini. Mfano Waziri wa Maliasili kaonekana kwenye media akifanyiwa tambiko. Kwa RC tusidharau tamaduni zetu kisa tunasoma biblia
 
Wamepeleka jiwe kuu pale Mbeya!!, fyatu wa mafyatu....hahahahaa. RC Mby, RC Tabora, Mambosasa Dar , Muroto Dom.....zamu yenye kutalawa mitandao, tuache kuangalia uchi za akina dada mitandaoni😀..... Wapambane watupe matukio kila wakati ili angalau tushawishike
 
japo wanasema huyu jamaa ana utindio wa ubongo kulingana na Muundo wa kichwa chake lakini kwa hili anapoint.
Hao lambalamba ni matapeli tu.
 
Asubiri tu. Wachawi mambo ya maana hawana shida nayo. Kuna DC (mwanamke) alipelekwa Tarime - enzi ya Mkapa - alipofika tu kituoni kazi yake ya kwanza ilikuwa ni kuwawashia moto ngariba (wanaokeketa wasichana). Na akapiga marufuku mambo hayo; wenyeji wakamwambia "isiwe shida".
Asubuhi moja akajikuta kakeketwa yeye, aliondoka bila kuaga Tarime.
 
Uchawi ni mila ndo maana viongozi karibia wote wanaenda kwa waganga ili wawape dawa za kuwalinda na majanga, wasafishiwe nyota nk hata viongozi wa dini wanauogopa uchawi
 
Asubiri tu. Wachawi mambo ya maana hawana shida nayo. Kuna DC (mwanamke) alipelekwa Tarime - enzi ya Mkapa - alipofika tu kituoni kazi yake ya kwanza ilikuwa ni kuwawashia moto ngariba (wanaokeketa wasichana). Na akapiga marufuku mambo hayo; wenyeji wakamwambia "isiwe shida".
Asubuhi moja akajikuta kakeketwa yeye, aliondoka bila kuaga Tarime.
Chai.
 
Back
Top Bottom