Wagner wanaweza kujifanya kama wahamiaji kuingia EU - Waziri Mkuu wa Poland

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,329
33,139

34149024-c26f-4f37-8ea6-d9048248e300.jpg


Wapiganaji wa Wagner nchini Belarus wanaweza kujifanya wahamiaji na kuingia EU, Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki ameonya.
Wagner pia wanaweza kunaweza kuchangia uhamiaji haramu kutoka Belarus, ambayo Poland inaelezea kama "vita vya mseto", anasema.
Takriban wapiganaji 100 wa Wagner wamehamia karibu na mji wa Grodno, karibu na mpaka wa Poland na Lithuania, Waziri Mkuu aliongeza.
Baadhi ya wanajeshi wa Wagner wamehamia Belarus chini ya makubaliano ya kumaliza maasi ya muda mfupi nchini Urusi mwezi Juni.
Kiongozi wa Belarus Alexander Lukashenko hapo awali alipinga kuzusha mzozo wa wahamiaji barani Ulaya kwa kuwarubuni wahamiaji wanaotarajiwa kuingia kwenye mipaka yake na mataifa ya EU.
Lakini Bw Morawiecki alisema Jumamosi kwamba zaidi ya wanachama 100 wa kundi la Wagner walihamia Belarus kaskazini-magharibi karibu na pengo la Suwalki - mpaka wa Poland wa maili 60 (95km) na taifa la EU la Lithuania, ambalo linatenganisha Belarus na Urusi ya Kaliningrad.
Alidai kuwa mamluki hao wanaweza kujifanya kama walinzi wa mpaka wa Belarus ili kuwasaidia wahamiaji kuvuka EU, au hata kujifanya wahamiaji wenyewe na kuingia katika umoja huo.
"Hali sasa inazidi kuwa hatari," aliambia mkutano wa waandishi wa habari kwenye ziara ya kiwanda cha silaha huko Gliwice, kusini mwa Poland.
"Hakika hii ni hatua kuelekea mashambulizi zaidi mseto katika eneo la Poland," aliongeza.
Maelfu kadhaa ya wapiganaji wa Wagner wamehamia Belarus tangu maasi ya muda mfupi ya kundi hilo dhidi ya Kremlin mwezi Juni.
Walipewa chaguo la kujiunga na jeshi la kawaida la Urusi au kwenda nchini Belarus, mshirika wa karibu wa Urusi.
Bw Morawiecki alisema kumekuwa na majaribio 16,000 ya kuvuka mpaka kati ya Belarus na Poland kufikia sasa mwaka huu.
Kulingana na shirika la udhibiti wa mpaka wa EU Frontex, kulikuwa na majaribio 2,312 ya kuvuka mpaka wa kuingia EU kutoka Belarus kati ya Januari na Juni.
chanzo. BBC
 
Sasa hata wakienda huko nchi za magharibi watafanya nini cha kustua sana kihivyo si ni njaa tu wanakimbia kwa sababu akina Belarus ndio nchi maskini sana Ulaya na ndio shida ya kuwa rafiki wa Russia kwani mara nyingi lazima uwe maskini tu. Bure kabisa.
 
Tatizo mnaosema Wagner group wana njaa hao wanaenda ivuruga Poland nyie tulieni muone Nato anavyo potezwa mmoja bada mmoja.
Wewe umelewa bangi au labda madhara ya kugonga kichwa sakafuni mara kwa mara.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom