mkutano wa uchaguzi wa CCM Songea vijijini kufanyika chini ya ulinzi mkali wa polisi

ligendayika

JF-Expert Member
Aug 31, 2012
1,183
198
Leo utafanyika uchaguzi wa nafasi mbalimbali za chama cha mapinduzi wilayani Songea Vijijini.

Uchaguzi huo utakua chini ya ulinzi mkali kwa kile kinachadaiwa kuwa wanachama wapiga kura kugoma kupiga kura katika nafasi ya mwenyekiti wa wilaya wa CCM kwakuwa hawajakubaliana na majina yaliyorudishwa toka Taifa hasa Baada ya wagombea wote wawili walioomba nafasi hizo kukatwa na kurudi majina ya wanachama wengine.

Hivyo polis hao wameletwa ili kuwashinikiza wanachama kupiga kura za mwenyekiti kwani wanachama hao wamedhamilia kupiga kura kuanzia nafasi za NEC kushuka chini. Chanzo ni wanachama wa CCM wilayani hapa.
 
Mmh!! nashukuru watanzania uelewa unaongezeka kila kukicha. Ni hatua nzuri kuelekea safari ya watanzania kujitambua na kukataa akili za wengine kujiona wao ndo waamuzi wa kila kitu bila kushirikisha umma.
 
Back
Top Bottom