Mkutano wa spika Tabora

Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,359
692
spikasitajimbo.jpg
 
Jamani makamba na chili wameingia JF nini? Mbona hamumpongezi mzee six kwa kuhutubia umati mkubwa?
 
Brother Six naona yuko kazini akijisaisha kwa maji ya Tabora kutoka bwawa la Igombe.

kila la kheri kaka'angu. Ila sasa na wewe lazima ufahamu kuwa kwa sasa wanakuwinda sana jamaa ili waonyeshe kuwa wewe ni MWENZAO. Upunguze au uache vidogodogo maana watakukamata huko na kumwaga Urambo yote picha zako ukila URODA. Tunaweza samehe kuwa ulikuwa hela CDA na kudanganya dawa za dola elfu........

Mengine yote yatategemea wewe. Kuhutubia UMATI wa Wanyamwezi si BIG deal na hasa kama wameahidiwa kitu kidogo wale wapambe. Sijui Redio ya Rage ilimsaidia kuutangaza huu mkutano? Na uzuri/ubaya wa Tabora huwa EVENT kama hizi ni za nadra sana. Sas akija SIX na kutangaza MKUTANO, watu kibaoo maana walau wakajionyeshe na wao wamenunua vinguo vikali siku hizi au wanaendesha......
 
Kaka Sikonge

Ulionekana na baiskeli yako ukiwahi huo mkutano, eti alisema nn?
 
Kaka Sikonge

Ulionekana na baiskeli yako ukiwahi huo mkutano, eti alisema nn?

Mkuu sikufika huko.

Nyani Ngabu alinitumia visenti wikii jana na ilipofika weekend nikaenda kwa mama Muuza na kununua bar nzima ya Wanzuki. Mhhh, wanzuki ilikuwa kali sana na matokeo yake mkutano nimeusikia tu. Ntajaribu kumpigia simu kaka yangu pale Tabora mjini anipashe habari kama yeye alikwenda.

Huyo mwenye Baiskeli alikuwa ni Mwana Kansimba mdogo.

Mkuu Masa, sasa hivi huku ni poa kabisa. summer ndiyo inakolea na ngoja nikuonyeshe picha jinsi Sikonge ilivyo kwa sasa.
 
Attachments

  • Si.jpg
    Si.jpg
    102.8 KB · Views: 61
Ur so funny! hii picha imenikumbusha mbali sana wakati tunahamia Iloganzala tulikodi huo usafiri....
 
Muhimu ni kaongea kitu gani?ndo point

Sitta sio hapendeki kiasi hicho lakini wananchi wamekusanyika kumpongeza kwa ujasiri wake wa kupambana na mafisadi, kwa hio watu wanapaswa kujua kuwa umati huo ni wa kupongeza na kumuunga mkono na sio kusikiliza atasema nini pekee
 
Brother Six naona yuko kazini akijisaisha kwa maji ya Tabora kutoka bwawa la Igombe.

kila la kheri kaka'angu. Ila sasa na wewe lazima ufahamu kuwa kwa sasa wanakuwinda sana jamaa ili waonyeshe kuwa wewe ni MWENZAO. Upunguze au uache vidogodogo maana watakukamata huko na kumwaga Urambo yote picha zako ukila URODA. Tunaweza samehe kuwa ulikuwa hela CDA na kudanganya dawa za dola elfu........

Mengine yote yatategemea wewe. Kuhutubia UMATI wa Wanyamwezi si BIG deal na hasa kama wameahidiwa kitu kidogo wale wapambe. Sijui Redio ya Rage ilimsaidia kuutangaza huu mkutano? Na uzuri/ubaya wa Tabora huwa EVENT kama hizi ni za nadra sana. Sas akija SIX na kutangaza MKUTANO, watu kibaoo maana walau wakajionyeshe na wao wamenunua vinguo vikali siku hizi au wanaendesha......

Mwambie "Brother" yako analikoroga atalinywa soon...
 
Sitta sio hapendeki kiasi hicho lakini wananchi wamekusanyika kumpongeza kwa ujasiri wake wa kupambana na mafisadi, kwa hio watu wanapaswa kujua kuwa umati huo ni wa kupongeza na kumuunga mkono na sio kusikiliza atasema nini pekee

Kweli wewe ni great sinker....kwa hiyo hata kama SS angeimba kinyamwezi mbele ya hiyo kadamnasi anastahili pongezi....Are you serious?
 
Sitta sio hapendeki kiasi hicho lakini wananchi wamekusanyika kumpongeza kwa ujasiri wake wa kupambana na mafisadi, kwa hio watu wanapaswa kujua kuwa umati huo ni wa kupongeza na kumuunga mkono na sio kusikiliza atasema nini pekee
Acha ujinga hapa alikuwa anafungua tamasha la Injili,kama ujuavyo siku hizi katika matamasha wajinga ndio hujazana hivyo ndivyoilivyokuwa!
 
Acha ujinga hapa alikuwa anafungua tamasha la Injili,kama ujuavyo siku hizi katika matamasha wajinga ndio hujazana hivyo ndivyoilivyokuwa!

Acha Jazba ndugu,sasa kila mtu ni mjinga? Kuanzia mwenye kutoa maoni hadi wenye kuhudhuria tamasha?Sema basi wewe ujanja ndo upi?Umati wa kuwapokea mafisadi ama? Pls be specific ni formula gani unatumia ku determine kuwa waudhuriaji wa mkutano/tamasha hili ni wajinga vs wahudhuriaji wa mkutano ama tamasha lile.la mafisadi.

Pointi ya Bunduki iko pale pale kwamba kuna waliokwenda kumsikiliza Sita,lakini pia kuna uwezekano wengi wao walikwenda kumsapoti Six kutokana na yaliyojiri kwenye vikao vyao vya chama,tukio zima la mkutano wa ccm lililosababishwa na kutofautiana na mafisadi ndo limepelekea sapoti aliyoipata hapo Tabora na pengine nchi nzima kwa ujumla,na kwa hivyo kabla ya kwenda kusikiliza,kuna waliokwenda just for support maana aliyoyafanya speaker na misimamo yake bungeni tayari wanayafahamu na since yeye bado ni speaker,anahitaji support...Ndivyo nilivyoelewa na sijaona ujinga wowote hapo kutoka kwa Bunduki.
 
Ni muhimu kujua ameongea nini...suala si kupongeza tu!

Nadhani Mwananchi wameicover hapa

Boniface Meena

KATIBU mkuu wa CCM, Yusuf Makamba na katibu wa itikadi na uenezi, John Chiligati wamepatwa kigugumizi kuhusu madai ya Spika Samuel Sitta kwamba ofisi ya makao makuu ya chama hicho ilizuia viongozi wa Mkoa wa Tabora kumpokea kwenye ziara yake.

Viongozi hao pia wamekwepa kusema chochote kuhusu maelezo ya Sitta, ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (CC), kwamba anasikitishwa na namna makao makuu inavyoshughulikia baadhi ya mambo, akihoji sababu za wao kuzungumzia masuala ambayo yako mikononi mwa kamati maalum.

Sitta alilalamikia kitendo cha viongozi wa mkoa wa Tabora kususia mapokezi wakati wa ziara yake mkoani humo akituhumu kwamba walitimiza maagizo ya viongozi wa juu wa chama hicho.

Sitta alinusurika kuvuliwa uanachama wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM wakati baadhi ya wajumbe walipotaka arejeshe kadi kwa madai kuwa, amekuwa akiendesha vikao vya Bunge kwa kuruhusu na kuishabikia mijadala inayokichafua chama na serikali.

Jaribio hilo, ambalo linadaiwa kufanywa na watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi, lilikwama na tangu wakati huo mbunge huyo wa Urambo Mashariki anaonekana kuwa kwenye hali ngumu ndani ya chama.

Mwishoni mwa wiki alitumia mkutano wa hadhara kunena yaliyoujaza moyo, akilalamikia kauli zinazotolewa na viongozi tofauti kuhusu maazimio ya Nec na madai kuwa ofisi ya makao makuu ya CCM ilizuia viongozi wa chama hicho mkoani Tabora kushiriki kwenye mapokezi yake, kitu ambacho kimetafsiriwa kuwa ni kulalamika nje ya vikao vya CCM.

"Analalamika kwenye magazeti badala ya kuleta taarifa kwetu; aje na malalamiko yake nitayashughulikia; sijayaona malalamiko yake," alisema Makamba jana alipoongea na Mwananchi kwa njia ya simu.

Makamba, ambaye pia aligoma kuzungumzia malalamiko ya Sitta kwamba, amekuwa akizungumzia mambo yaliyojadiliwa na Nec nje ya vikao badala ya kuiachia kamati iliyoundwa, alimtaka Sitta kuwasilisha malalamiko hayo kwake ili ayafanyie kazi.

Naye Chiligati alisema: "Halmashauri inasema mambo hayo yazungumzwe ndani ya chama na magazeti yaandike mambo ya maendeleo."

Chiligati alisema Sitta anapaswa kutoa malalamiko yake ndani ya vikao vya chama, ili yajadiliwe na kupatiwa ufumbuzi kuliko kuzungumza nje ya vikao kama anavyofanya sasa.

Juzi Spika Sitta aliwaambia waandishi wa habari nyumbani kwake Urambo, Tabora kuwa amesikitishwa na wakuu wa chama kumzuia katibu na mwenyekiti wa mkoa wasimpokee wakati alipowasili mkoani humo. Hata hivyo, wanachama wengi walijitokeza kumpokea.

"Nimesikitishwa na wakuu wa chama ambao waliruhusu, (Andrew) Chenge na (Edward) Lowassa wapokewe, lakini wanawazuia katibu na mwenyekiti (Wa Tabora) wasinipokee, ingawa wanachama walijitokeza kunipokea; hii ndiyo inatufanya wanachama tuamini kuwa kuna wanachama wenye haki na wasio na haki; hii si dalili nzuri,"alisema Spika Sitta.

Alishangazwa na kitendo cha ofisi ya makao makuu ya CCM kuushinikiza uongozi wa mkoa usimpokee wakati alifika kwenye ofisi ya mkoa na kuweka saini katika daftari la wageni, lakini akashangazwa kuwa viongozi hao hawakujitokeza pamoja na kuwa wanachama walijitokeza kwa wingi.

Akizungumzia kuhusu uamuzi uliotolewa na CCM mjini Dodoma, alisema anashangaa kuona kila mtu anatoa kauli katika mambo ambayo ni dhahiri yanayoonekana kuwa ni tuhuma bila ya kuacha vyombo vilivyoundwa na chama vifanye maamuzi yake.

"Nasikitishwa na jinsi ambavyo makao makuu ya CCM yanashughulikia baadhi ya mambo kwa kuwa ingekuwa ni mara moja kama kutoa taarifa, basi kauli ya katibu wa itikadi na uenezi, Kapteni John Chilligati ingetosha, lakini inashangaza wanavyorudiarudia mambo ambayo bado yanatakiwa yashughulikiwe na kamati maalumu," alisema.

Alisema anashangazwa jinsi kikundi cha watu kinavyojaribu kuzungumza mambo ya uzushi kuhusu yeye na kujaribu kusema mambo ambayo hata hayapo.

Sitta, ambaye alikuwa kwenye hali ngumu wakati wa kikao cha Nec ambacho kilitawaliwa na maombi ya baadhi ya wajumbe ya kutaka avuliwe uanachama, alisema kuwa anasikitishwa na kauli zilizotolewa na baadhi ya viongozi wa CCM ambazo alisema zilionyesha kuhukumu hata kabla tume iliyoundwa na NEC haijatoa matokeo yake.
Kuhusu malalamiko ya Sitta kuwa Makamba amekuwa akizungumza zungumza nje, Chiligati alisema kuwa suala hilo pia linatakiwa lizungumzwe ndani ya chama.
 
acha ujinga hapa alikuwa anafungua tamasha la injili,kama ujuavyo siku hizi katika matamasha wajinga ndio hujazana hivyo ndivyoilivyokuwa!

Pale hakukuwa na mjinga hata mmoja, labda kwenye mikutano ya kuwapokea mafisadi ambayo naamini wewe ulikuwepo.
 
Last edited:
mjinga mwenyewe! Yaani sisi tuliokuwa pale unatuita wajinga! Ebo!

Mh spika naomba mwogozo....jukwaa limeanza kuharibika...tupunguze makali ya hizi lugha ...tutafautiane kimitizamo ila tusiparurane! Sisi wote batoto ba baba mmoja
 
Mimi nilikuwepo kwenye ule mkutano pamoja na watu wengi tulio na akili kuliko huyo anayejiita MtanzaniaRaia. Inakuwaje aseme mikutano kama hiyo huhudhuriwa na watu wajinga! Moderators inabidi wadhibiti watu wa aina hii wanaoingia humu kutukana watu wengine.
 
Sawa Mazee ila unajua kale kausemi ---ukijibishana na mjinga watu wengine watashindwa kukutofautisha....
 
Sikonge unanifurahisha sana taratibu naanza kutamani kukutana nawe nawe siku moja maana unaichambua Tabora kuliko, any way. mkutano wa six ulikuwa na watu kiasi chake hasa jukwaa kuu ndilo lililojaa watu na zaidi nilichoshuudia kwa six pale Al Hasan Mwinyi ni six kutamba kuwa atakula sahani moja na wabaya wake na in fact ilikuwa ni sehemu ya Ibada maana watu walikwenda kwenye uzinduzi wa Kanda. aidha mapokezi ya six hayakuwa mazuri kama mwenyewe alivyolalamika kwenye vyombo vya habari
 
Last edited:
Back
Top Bottom