Mkutano wa Freeman Mbowe mjini Kahama

Mkutano wa Freeman Mbowe mjini Kahama

Joined
Dec 11, 2010
Posts
3,321
Reaction score
6,331
Wakuu.

Leo unafanyika mkutano mkubwa wa hadhara kanda ya Serengeti hapa jimbo la Kahama. Ni mkutano ulioandaliwa na kanda ya Serengeti kabla ya kikao cha kamati tendaji ya kanda.

Kanda hii inaundwa na mikoa ya Mara, shinyanga na mkoa mpya wa simiyu.

Hoja zilizozungumzwa na Mwenyekiti Mbowe:-

1. Tutafanya mabadiliko ya mfumo wa utawala uliopo na kutekeleza mfumo wa Majimbo/Kanda kwa mujibu wa sera ya Chadema. Wananchi watakuwa na sauti kwenye mfumo wa uongozi na matumizi ya rasilimali zao.

2. Mamlaka ya Rais ya uteuzi wa nafasi mbalimbali yatapunguzwa kuliko ilivyo sasa

3. Mfumo wa kuandikisha wapiga kura kwa BVR hauwezi kutekelezwa kwa ukamilifu wake na kutumika kwenye kura ya maoni, nguvu kubwa ipelekwe kuandaa uchaguzi mkuu.

4. Katiba ya sasa na hata Katiba inayopendekezwa zote hatuzikubali. Madai ya Katiba mpya yapo palepale.

5. Wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi mkuu.

6. Marehemu na waathirika wa mvua ya mawe Kahama walifanyiwa dua maalum ya kiislam na kikristo uwanjani pamoja na sadaka kutolewa na wanachama.

7. Chadema itachangia mabati ya Tshs Mil. 10 kwa ajili ya waathirika wa mvua ya mawe.

Mwisho; Baada ya mkutano maelfu ya wananchi walimsindikiza Mwenyekiti Mbowe mpaka hotelini alikoshukia kwa ajili ya mapumziko mafupi kabla ya kushiriki vikao viwili vikubwa "Kamati Tendaji ya Kanda ya Ziwa Mashariki 'Serengeti' na Baraza la Uongozi la Kanda"


attachment.php

attachment.php

attachment.php
 

Attachments

  • 1425909029234.jpg
    1425909029234.jpg
    64.3 KB · Views: 6,931
  • 1425909063286.jpg
    1425909063286.jpg
    68.4 KB · Views: 6,908
  • 1425909100518.jpg
    1425909100518.jpg
    85.9 KB · Views: 6,878
  • 1425909133178.jpg
    1425909133178.jpg
    88.7 KB · Views: 1,390
Msafara huo ishara ya nguvu ya umma kurudisha madaraka mikononi mwao kupita chadema October 2015.
 
Tumwagie na picha kabisa kina Tomaso waone.
 
  • Thanks
Reactions: MTK
wananchi wana imani kubwa sana na CHADEMA wameshachoka kuongozwa na chama ambacho kimeshapoteza dira na mwelekeo ccm ,
 
chadema mkombozi wa maskini hilo ccm ni chama la mashetani wekundu yanaroho mbaya watu wanakufa hospitalini hawana hela ya dawa yenyewe yanagawana mabilioni yanalaaniwe
 
Walichokiona leo waki na lembeli na mwenzake maige kimewaacha kinywa wazi kwa kweli mji ulisimama gafla mbowe alipoingia mjini watu ni wengi sana sasa ivi ndo tunaelekea uwanjani siditii!
 
Safi sana kamanda Mbowe.hakuna kulala mpaka mccm yakimbie nchi.


Hukuona kuwa yameshakimbia? Kitendo cha Kinana kuingia uwanjani ni ishara tosha hawana jipya sasa yameamua kutumia nguvu za giza mchana kweupe. Ukiona hivyo ujue hapo kabla yalikuwa yanaenda kwa kalumanzira ucku sasa kalumanzira dawa zake hazifanyi kazi ucku akawapa wazo la kutembea na fisi mchana kweupe.
 
Walichokiona leo waki na lembeli na mwenzake maige kimewaacha kinywa wazi kwa kweli mji ulisimama gafla mbowe alipoingia mjini watu ni wengi sana sasa ivi ndo tunaelekea uwanjani siditii!


Picha picha picha jamani wekeni tuone waTz wamesoma alama za nyakati.
Lembeli mwenyewe kajijengea migorofa hiyo. Pale Nyahanga Kahama Fm alafu bungeni anahishaua anawatetea wanaNchi. WanaNchi wamechoka na maneno ya hadaa sasa wanataka vitendo.
 
Baada ya kupokelewa na msafara mkubwa wa magari na pikipiki takribani 120+, akitokea kuwaona waathirika wa mvua kubwa Kijiji cha Mwakata, Msafara sasa ndiyo unaelekea Uwanjani...
 
eee bhana mkuu , uzi uko chukuchuku utadhani msosi wa mgonjwa wa kisukari bhana ! tupia mapicha mjomba .
 
Back
Top Bottom