Moja ya vituko ktk mkutano huu ni Askari mmoja wa jeshi la polisi aliyekuwa akirikodi mkutano wa Dr kwa siri kuchanwa live na Dr Slaa mwenyewe. Ilianza hivi, kama kuna mtu ametumwa kupiga picha tunaomba aje huku mbele apige kwa uwazi na sio kwa siri. Ndipo alipomgeukia huyo askari na kumwambia,binti yangu kwa nini unapiga picha na kurikodi mkutano wangu kwa siri?njoo huku mbele urikodi vizuri ili umtumie huyo aliyekutuma maana inaelekea hujui nani unayemrikodi.Kwa taarifa yako nguo ulizovaa ni kodi zetu,kamera unayotumia ni kodi zetu kwa hiyo sasa kwa nini ufanye kwa siri? Ikikumbukwe kuwa hapa Dr alikuwa akielezea Rais kugeuka kuwa afisa manunuzi. Dr alipogundua anarikodiwa alirudia kwa msisitizo kauli yake na kumwambia yule askari rikodi hiyo kisha mpelekee aliyekutuma sasa hivi. Kwa aibu yule askari mwanadada alianza kujisogeza taratibu kuondoka huku akiwa amezongwa na wananchi hadi pale Dr alipowasihi kumuacha aondoke zake