Ameongele mambo kadhaa ya msingi.
1. uchaguzi wa serikali za mitaa, ambapo ameawaasa wanachadema kuanzia kesho kujiandikisha kwenye daftari ya kupigia kura za mitaa, kwani daftari hizo zipo kwenye ofisi za mitaa na watuwengi hawana taarifa kuwa wanatakiwa kujisajili kabla ya kupiga kura. amesema wanachadema wasijekulalamika kuwa wameshidwa kupiga kura kwani wapinzani wao wanaweza kutumia turufu hii kuandikisha wanachama wao tu na kisha kushibda uchaguzi.
pia amesisitiza kuwa chadema inahitaji sana uongozi mashinani ili kukipa nguvu chama kwenda uchguzi wa wabunge na rais
2 Kura ya maoni kwa katiba pendekezwa.
amewasihi wananchi kujianda kupiga kura ya hapana kwani chadema inaamini katiba mpya pamoja na kutaja maeneo mengi ya haki za wakulima, wafugaji, walemavu na nk, lakini katiba hiyohiyo imewanyanganya nguvu wananchi kwani kuna ibara inayowanyima haki ya kudai mahakamani, kwahiyo ni sawa na kutokuwepo.