Mkutano wa CHADEMA Njombe na Matukio yake

Mkutano wa CHADEMA Njombe na Matukio yake

Hakikwanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2010
Posts
4,043
Reaction score
1,012
Kweli mwenyezi Mungu yupo upande wa chadema.Wenje anachana mawingu. Kasimu kangu hakana uwezo wa kutuma picha.

Katika hali ya kushangaza wakazi na wananchi wa Mkoa wa Njombe wamemkana Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa madai kuwa hawakumtuma kutumikia chama bali kushughulikia kero na matatizo ya wananchi.

Hayo yalitokea katika mkutano wa hadhara uliofanyika mkoani hapo katikati ya Jimbo la Njombe Kusini ambalo yeye ndiye Mbunge wake.

Mkutano huo ambao uliongozwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Mandeleo( CHADEMA), Dr wilbrod Peter Slaa,Naibu katibu mkuu kutoka zanzibari pamoja na wabunge machachari kutoka katika chama hicho(Mh Joseph Mbilinyi-Mbeya mjini, Mhezekiel Wenje-Nyamagana pamoja na Mchungaji Peter MsigwaIringa mjini) ambao wote kwa pamoja walifukuzwa bungeni kwa madai kuwa wanaleta fujo bungeni.

Dr Slaa aliwataka wananchi wamthibitishie kuwa Makinda hakwenda bungeni kuwatetea bali kukitumikia Chama Cha Mapinduzi hivyo wabunge wa Chadema waendelee na kasi hiyo hiyo ya kuisimamia na kuikosoa serikali, hapo ndipo umati wote uliohudhuria mkutano huo uliponyoosha mikono yote juu kwa ishara ya kuunga mkono hoja iliyotolea na kiongozi huyo.

Spika Anne Makinda anatuhumiwa kwa kuliongoza Bunge ki ubabe hivyo kuwanyima wapinzani haki yao ya msingi ya kuihoji serikali juu ya matuimizi mabaya ya mali ya umma .

SAM_1480.JPG

MH Ezekiel Wenje Akiwahitubia wananchi wa mkoa wa Njombe


SAM_1483.JPG

Naibu Katibu Mkuu kutoka Zanzibar akizungumza na wananchi wa Njombe


SAM_1493.JPG

Dr Wilbrod Slaa akihutubia umati mkubwa wa watu mkoani hapo

SAM_1499.JPG

Wananchi wakisikiliza kwa makini katika mkutano huo

SAM_1489.JPG

Dr slaa akiendelea kuwahutubia wakazi na wanachi wa mkoani Njombe

SAM_1503.JPG

Wananchi wa njombe wakiunga mkono maamuzi ya wapinzani juu ya uendeshwaji wa Bunge
 
Jamani sasa itakuwaje kama mchina wako hawezi hata kutpatia picha,anyway tu-update japo kinachoongelewa
 
Kweli mwenyezi Mungu yupo upande wa chadema.Wenje anachana mawingu. Kasimu kangu hakana uwezo wa kutuma picha

tiririka na updated kamanda hambakati chini ya belti lazima chini wakae
usikonde kamanda mtoi,makene and the like ipad zitatupiamo live covarage soon
 
Wenje amemaliza kuzungumza. Amezungumzia hali halisi juu ya mafisadi wanavyo ifisadi nchi
 
Naibu wa katibu mkuu kwa upande wa Zanzibar anahutubia jinsi makinda anavyo hujumu bunge na amemkaribisha katibu mkuu wa chadema
 
Slaa ana wasalimia wananchi na kushukuru wananchi kwa kuwakaribisha
 
Spika wapi bana, rudidha mitu hii bungeni haraka, naharibu wananchi bana, najaza watu wetu mambo ya uwongo kuharibu jina yetu bana, sasa nchi inakuwa ngumu sana kutawalika bana!!
 
Sema unaona aibu watoto wachache wa mtaani ndo wapo hapo.Eti simu yangu haina uwezo
 
Kwa mwendo huu ccm mwisho wake mgumu kwani wananchi wamejaa sana na taarifa ninazozipata ccm wameitisha kikao cha dharura
 
Sema unaona aibu watoto wachache wa mtaani ndo wapo hapo.Eti simu yangu haina uwezo

vuta subira mkuu kama ilivyokuwa mwanza,mbeya,dom,iringa na kwingineko kuhusu shazi hilo nikupigia mstari tu.....wakati mwingine screan ya kamera haitoshi
 
Sema unaona aibu watoto wachache wa mtaani ndo wapo hapo.Eti simu yangu haina uwezo
Mkuu Wingu, umenifurahisha sana kwa kuleta hoja ya watoto wa mitaani. Maana kwa siku kadhaa nimekuwa nikijiuliza ni kwanini kwenye mikutano ya CHADEMA Hatuoni watoto wa shule wala wale wa mitaani? Wewe angalia picha zote, Mwanza, Mbeya Iringa huoni mtoto kabisa? Hii inakuwaje? Na kwanini kwenye mikutano ya CCM tunaona hadi wanafunzi wakiwa bado na sare za shule plus watoto kibao wamekaa mstari wa mbele karibu na Jukwaa?

Hivi inawezekana kwamba huwa wanavutiwa na ule wali ambao CCM wanagawa au ni wale wasanii wa bongo flava? Napata shida sana kuelewa, au CHADEMA haipendwi na watoto? Labda CHADEMA wanaongea hard points ambazo watoto hawazielewi? Au ni kwamba CCM huwa wanaimba taarabu jukwaani kiasi cha kuwavutia watoto? Nina maswali mengi mieee? Tafadhari nisaidie kujibu kwanza haya kabla sijauliza mengine.
 
Chadema inapendwa na watu wanaipenda toka moyoni mwao hii ni mara ya kwanza kwangu kuhudhuria mkutano kweli watu wamejaa
 
Sema unaona aibu watoto wachache wa mtaani ndo wapo hapo.Eti simu yangu haina uwezo
Wingu unakuwaje na kihoro namna hiyo? Njombe ni baba wa mageuzi muulize Semamba makinda alivyopigwa mweleka na ngunangwa mwaka 1995.mama miaka yote hii anakwenda kwa tiamaji tiamaji kwa kuhonga wagombea wa cdm mfano mzuri ni 2010 pale mgombea wa cdm alipotoweka na kuonekana muda ambao urudishaji wa fomu ulishapita.
njombe iko tayali kwa mageuzi na naomba wanacdm njombe mpigane kulirudisha jembe la mageuzi diwani Luvanda aliyetekwa nyara na ccm,yule ni mpambanaji na ukiufunua moyo wake asilimia 75% ni cdm na 15% ni ccm.
 
Back
Top Bottom