Mkutano wa CHADEMA na Jumuiya ya Ulaya Umevunja Mikataba ya Kimataifa

Sioni chochote Ulichoandika hapa kuwa kimefanywa na EU au CHADEMA! Cramming and understanding are two different things! What I see from your Article is the result of cramming and quoting of provisions rather than showing which provisions were breached! Unless you come again n tell us specifically which provisions did the EU breach, and How!
Wakati naandika sikutegemea kwamba kila mtu ataelewa kila kitu, ukizingatia kwamba kila mtu anaoupande wake ambao atakua anatumia katika kuangalia mambo.
 
stroke
I think wamefanya kikao pale kwa vile hawana sehemu ya kufanyia kikao chao

Walifanya kikao giraffe hotel wakavamiwa na police, walifanya tena sehemu nyingine police Ikaenda kuwatoa

So now solution ni kufanyia sehemu ambazo police hawez kwenda

Ndio kama hapo walipo sasa
 
Ibara ya 15 (2) ya International Covenant on Civil and Political Rights (1966) inasema, nanukuu;

" Art. 15 (2). Nothing in this article shall prejudice the trial and punishment of any per son for any act or omission which, at the time when it was committed, was criminal according to the general principles of law recognized by the community of nations".

Kwa kuzingatia hayo, ni dhahiri mambo haya yanatakiwa kufanyika;

(i) Jumuiya ya Ulaya kuomba radhi kwa hayo yaliyotokea,

(ii) Serikali Kupitia Waziri wa Mambo ya Nje na jumuiya ya afrika mashariki kutoa tamko kulaani kitendo hicho.


Ni waase tu ndugu zangu kuacha kufanya vitendo ambavyo vitazua mtafaruku bila ya kuwa na grounds zozote zile za kujustify vitendo vyao hivyo batili.

Sasa si muwaite wajieleze tuone!
 
Yapo maelezo na uzi upo hapa, kwamba walikua wakifanya kikao cha ndani katika premises za jumuiya ya Ulaya, meaning waliomba venue kwa ajili ya kufanya shughuli za kisiasa na wakakubaliwa. Mwisho wa siku ni kuwa Mikataba Tajwa katika article hii, imevunjwa yote.

Nilichokuuliza wapi ilipokatazwa mabalozi au maofisa wa balozi kukutana na raia yeyote..? Wewe umejua walichokizungumza..? Hao mabalozi/maafisa balozi wameshatoa kauli yeyote kuonyesha muelekeo wa mazungumzo waliozungumza..?
 
Umepitwa na wakati. UN ya sasa inaidhinisha kuingilia mambo ya nchi nyingine katika masuala kama:
1- Dola kufanya mauaji ya kimbari kwa watu wake
2- Dola kufanya mabo ambayo huenda yakapelekea kwenye mauaji ya watu wengi.
Kuna baadhi ya nchi zimependkeza kuingilia ikiwa:
- Dola inaonesha dhahiri uonevu mkubwa wa watu wake na kukandamiza demokrasia.
Sijui Tanzania katika hali ya sasa unaiweka katika fungu gani? Soma :"interventions by Kofi Annan. Naona waishi mbali sana na mji!
 
I think wamefanya kikao pale kwa vile hawana sehemu ya kufanyia kikao chao

Walifanya kikao giraffe hotel wakavamiwa na police, walifanya tena sehemu nyingine police Ikaenda kuwatoa

So now solution ni kufanyia sehemu ambazo police hawez kwenda

Ndio kama hapo walipo sasa
Kwa bahati mbaya kufanya hivyo ni kwenda kinyume na makubaliano yaliyowekwa na nchi wanachama katika mikataba ya kimataifa, ambapo Tanzania na Nchi za Jumuiya ya Ulaya zote ni wanachama.
 
Umepitwa na wakati. UN ya sasa inaidhinisha kuingilia mambo ya nchi nyingine katika masuala kama:
1- Dola kufanya mauaji ya kimbari kwa watu wake
2- Dola kufanya mabo ambayo huenda yakapelekea kwenye mauaji ya watu wengi.
Kuna baadhi ya nchi zimependkeza kuingilia ikiwa:
- Dola inaonesha dhahiri uonevu mkubwa wa watu wake na kukandamiza demokrasia.
Sijui Tanzania katika hali ya sasa unaiweka katika fungu gani? Soma :"interventions by Kofi Annan. Naona waishi mbali sana na mji!
Pitia mikataba hiyo, Yote hayo yapo,

Hakuna kati ya yale waliyofanya chadema yamehalalishwa na mikataba hiyo.
 
Wewe stroke ,

Katika mazingira ambayo hadi misiba inavamiwa kwa kuhisi vikao vya chadema vinaendelea mnategemea nini?

Katika mazingira ambayo wanapigwa risasi mchana kweupe kwenye maeneo ya vingozi wa bunge na serikali mnategemea nini?

Katika mazingira ambayo viongozi hao wa chadema wanauwawa kinyama kwa mapanga nk, na wengine kutekwa na kupotezwa, mnategemea nini?

Mifano ni mingi sana kuirodhesha yote hapa. Sasa na wale waliompokea Ngurumo mbona hujawataja? Au tofauti ni nini?

Kiukweli imewauma sana kwasababu ndo wafadhili manaowategemea kwa misaada yao huku mkisema ni “mabeberu wanaopewa sapoti na chadema”. Na wakati bajeti karibia yote wao ndo wako responsible!

Jambo kubwa mtakalojutia, haijalishi maendeleo mtakayoclaim kuyaleta, ni hili la kuminya demokrasia na ubabe, visasi, na matendo ya kinyama dhidi ya wananchi wenzenu kwa kusingizia uzalendo, huku makosa yote mkiwa mmeyafanya nyie kwa kuingia mikataba bila kuwa makini, mukaliingiza Taifa hasara kubwa! Sasa mnatetea watu waliotuingiza hasara, na wakati ni wazi kuwa uzalendo ni kwa Taifa na si mtu au watu!

Ni haki ya wananchi kumpiga chini mtu anayewapa hasara ama anayelipa taifa hasara, tunapiga chini, tunaweka wengine, na wao wakizingua, tuweze kufanya the same. Ndo utawala wa kidemokrasia, na siyo longo longo zenu. Taifa kwanza!
 
Hivi Syria, Egypt, hizo sheria huwa zinakuwa suspended.

Israel anaingia na kuboom bila kuomba idhini huko kumekaaje

Balozi wa China kupanda jukwaani na kupigia kampeni hakuona hizo international treaties
 
Sawa tumekuelewa
Russia na US kuingilia mambo ya Syria ni kuingilia kinyume na maumbile siyo?
US kuingilia mambo ya Afaghanstan ilikuwa ni kitu gani?
US na UK kuingilia Iraq mpaka kumuua tena Rais wa nchi hicho unakiita nini!!
Nimekosa jina la kukuita, ngoja nikuite UMOJA WA ULALAMALAYA
 
Ccm mjiandae kisaikolojia kukosa kazi maana Revolution ishapewa baraka kutoka UN nadhani ..mmeanza kukosa Amani .
 
Back
Top Bottom