Mkutano wa CHADEMA na Jumuiya ya Ulaya Umevunja Mikataba ya Kimataifa

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,632
40,790
Zipo taarifa, kutokana na Picha zinazozunguka katika mitandao ya kijamii kwamba siku ya Tarehe 27 ya mwezi wa tatu(3) 2018, Chama cha Demokrasia na maendeleo kilifanya kikao cha chama ndani ya ofisi za jumuiya ya nchi za ulaya. Sina hakika sana na kilichofanyika kama kilifanyika , ila ninayo machache ya kuyajadili hapa;

Kikao hicho ni matokeo ya hatua ya serikali kupitia vyombo vyake vya kiulinzi na usalama pamoja na utoaji haki kuwafikisha mahakamani viongozi sita (6) wa Chadema kutokana na makosa mbali mbali yaliyofanyika mwezi mmoja kabla, yaliyopelekea kutokea kifo cha wanafunzi wa chuo cha usafirishaji NIT.

Tanzania kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa ( UN) ni mmojawapo wa nchi zilizokubaliana katika matumizi ya mikataba mbali mbali ya kimataifa inayotoa maelekezo ya nchi wanachama namna ya kufanya mambo yake ya ndani na jinsi ya kuhusiana na nchi nyingine.

Moja wapo ya mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeipitisha ni pamoja na United Nations Charter, ya mwaka 1945, International Covenant on civil and Political Rights ( 1966) na pia ni mwanachama wa mahakama ya kimataifa ya ICJ.

Ni kanuni ya kimataifa inayotambulika kwamba, hakuna Taifa lolote lenye mamlaka ya kuingilia mambo ya ndani ya Taifa jingine mwanachama kwa namna yoyote ile, iwe ni kwa matumizi ya nguvu ama la, kanuni hiyo ni zao la mikataba mbali mbali ya kimataifa kama ilivyonukuliwa hapo juu.

Kanuni hiyo, ilianza kutumika kuanzia miaka ya 1933 kupitia Ibara ya 15 ya mkataba wa kimataifa wa Covenant of the League of Nations na pia The Montevideo Convention on Rights and Duties of States ambayo kwa pamoja ilikataza mambo yafuatayo;

" The inteference with the freedom(uhuru), sovereignty ( mamlaka ya nchi) or other internal affairs (mambo ya ndani ya nchi) or the process of the governments of other states ( au shughuli(michakato) za/ya nchi husika)"

Kanuni hiyo, kama ilivyoaninishwa hapo juu, katika mikataba hiyo ya kimataifa, iliwekewa nguvu na Mkataba wa Umoja wa kimataifa wa mwaka 1945 ama UN Charter na katika maazimio mbali mbali.

UN Charter (1945) inatambua kanuni hiyo katika Ibara ya 2.4 na 2.7 kama ifuatavyo;

2. 4. All Members shall refrain in their international relations from the threat or use of force against the territorial integrity or political independence of any state, or in any other manner inconsistent with the Purposes of the United Nations.

2. 7. Nothing contained in the present Charter shall authorize the United Nations to intervene in matters which are essentially within the domestic jurisdiction of any state or shall require the Members to submit such matters to settlement under the present Charter; but this principle shall not prejudice the application of enforcement measures under Chapter VII.


Maazimio mbali mbali ya Umoja wa kimataifa kama Azimio Na. 2131(xx) la mwaka 1965, pia lilitambua kanuni hiyo ya kimataifa inayoweka katazo kwa nchi wanachama kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine.

Kwa kuzingatia kanuni hiyo, mahakama ya Kimataifa ya Utoaji haki ama ICJ, imetoa maamuzi kulingana na mashitaka yatokanayo na madai ya nchi moja kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, mfano mzuri ni shauri lile lihusulo nchi ya Nicaragua na Marekani mwaka 1986 na pia Congo na Uganda la mwaka 2005, tukianza na lile la marekani na Nicaragua Mahakama ya ICJ ilikua na haya ya kusema;

NICARAGUA VS USA, (Merits) ICJ Reports (1986),

"The principle of Non- Intervention involves the right of every foreign state to conduct its affairs without outside interference, though examples of trespass against this principle is not infrequent, the court considers that it is part and parcel of the customary international law....

The principle forbids all states or groups of states to intervene directly or indirectly in the internal or external affairs of the states.."


Katika shauri la Congo na Uganda mahakama ilikua na haya ya kusema,

DRC Vs UGANDA, ( Merits) ICJ Reports (2005),

" The principle of non -intervention prohibits a state to intervene directly , or indirectly, with or without armed force, in support of the internal opposition within a state".

Kitendo cha Jumuiya ya Ulaya kuruhusu Chadema kutumia premises zao katika kufanya mkutano wao, kimekwenda kinyuma na kanuni za kimataifa zinazokataza nchi kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, na kimevunja mikataba yote ya kimataifa.

Ikumbukwe kwamba makosa waliyoshitakiwa viongozi wa chadema, sio ya kisiasa, bali ni makosa ya kawaida kabisa ambayo mtu yetote ambaye ni Raia wa Tanzania anaweza kushitakiwa nayo, hivyo hakuna sheria yeyote iwe ya ndani au nje iliyovunjwa jambo ambalo lingewapa Jumuiya ya Ulaya uhuru wa kufanya walichokifanya na kwa kuzingatia kwamba viongozi wa chadema hawana kinga ya kushitakiwa.

Ibara ya 15 (2) ya International Covenant on Civil and Political Rights (1966) inasema, nanukuu;

" Art. 15 (2). Nothing in this article shall prejudice the trial and punishment of any per son for any act or omission which, at the time when it was committed, was criminal according to the general principles of law recognized by the community of nations".

Kwa kuzingatia hayo, ni dhahiri mambo haya yanatakiwa kufanyika;

(i) Jumuiya ya Ulaya kuomba radhi kwa hayo yaliyotokea,

(ii) Serikali Kupitia Waziri wa Mambo ya Nje na jumuiya ya afrika mashariki kutoa tamko kulaani kitendo hicho.

Ni waase tu ndugu zangu kuacha kufanya vitendo ambavyo vitazua mtafaruku bila ya kuwa na grounds zozote zile za kujustify vitendo vyao hivyo batili.
 
stroke
Ulitaka wafanye wapi kama hata mikutano ya ndani "inabakwa?"

Unapata nini kwa viongozi hao kuswekwa umande kwa sababu za "gari bovu?"

Nini waliongea/walijibu Jumuiya hiyo baada ya kuongea n.a. Chadema au ni uchawi unakusumbua? Binafsi sijasikia wakitoa tamko lolote!

KAMA ni mikataba kuvunjwa kwa MANUFAA ya raia ni bora mara 100 kuliko kwa masilahi ya "nyang'au" wachache waliojipa umasiha !

NB.Kabla Jumuiya ya kimataifa haijaomba radhi (japo hakuna sababu za msingi),mnaoleta "hewa chafu" Tz muombe radhi kwa watz .

Mlikabidhiwa nchi yenye amani,nyie mnaoleta utamaduni wa ajabu toka kwa mababu zenu wenye roho ngumu mithili ya Kaini!

OLE WENU SIKU MEZA IKIPINDULIWA.
 
stroke
Sioni chochote Ulichoandika hapa kuwa kimefanywa na EU au CHADEMA! Cramming and understanding are two different things! What I see from your Article is the result of cramming and quoting of provisions rather than showing which provisions were breached! Unless you come again n tell us specifically which provisions did the EU breach, and How!
 
Yaani masisiemu sio kwa kuweweseka huko.. Akili ya kawaida tu ingekuonyesha kwamba wale waliomba kukutana na maafisa wa ubalozi.. Na maafisa wa ubalozi wasingeweza kuwakatalia kuwasikiliza.. Hilo ndilo ambalo nyie masisiemu hamna na hamuwezi.. Kuwasikiliza wale mnaopingana nao mawazo na itikadi.. Reference zako hazionyesha popote pale ambapo maafisa ubalozi au mabalozi wanazuiwa kuonana na raia wa nchi wanazowakilisha..
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Yaani masisiemu sio kwa kuweweseka huko.. Akili ya kawaida tu ingekuonyesha kwamba wale waliomba kukutana na maafisa wa ubalozi.. Na maafisa wa ubalozi wasingeweza kuwakatalia kuwasikiliza.. Hilo ndilo ambalo nyie masisiemu hamna na hamuwezi.. Kuwasikiliza wale mnaopingana nao mawazo na itikadi.. Reference zako hazionyesha popote pale ambapo maafisa ubalozi au mabalozi wanazuiwa kuonana na raia wa nchi wanazowakilisha..
Yapo maelezo na uzi upo hapa, kwamba walikua wakifanya kikao cha ndani katika premises za jumuiya ya Ulaya, meaning waliomba venue kwa ajili ya kufanya shughuli za kisiasa na wakakubaliwa. Mwisho wa siku ni kuwa Mikataba Tajwa katika article hii, imevunjwa yote.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom