Mkutano wa CHADEMA na Jumuiya ya Ulaya Umevunja Mikataba ya Kimataifa

Umenukuu vifungu vingi kwa nia ya kutetea uovu?

Lakini unajua kuwa baada ya mauaji ya kimbali ya Rwanda, ni Umoja huo huo wa Mataifa umetoa haki ya uingiliaji kati pale inapoonekana kama kuna mauaji ya kimbali au kuna njama za kufanya mauaji ya kimbali?

Halafu kwa unafiki wako, mbona hujasema lolote kuhusiana na mikataba ya kimataifa ambayo tumeridhia inayohusiana na kulinda na kuheshimu haki za binadamu?

Kwa sasa Watanzania tuna haki ya kutumia nguvu na jitihada zote zinazoruhusiwa na na zisizoruhusiwa kwa nia ya kuondokana na uonevu, ugandamizaji, utesaji na mauaji maana hata huyo anayetutendea uovu huu haheshimu sheria wala katiba.
 
Hata mkifanya nini, tunachukua nchi yetu 26042018. Hakuna mkataba wa kuwazuia wananchi kujitetea katika nchi yao.
Hamna uwezo huo hata mkiwaita mabwana zenu wote, hata mita 500 hamtasogea kulifikia geti la jumba jeupe.
 
Nadhani unapaswa kuweka kumbukumbu sawa,kikao hicho hakikutokana na kuwekwa ndani viongozi wa CHADEMA hisipokuwa kilitokana na viongozi wa CHADEMA waliokuwa maabusu kutoletwa mahakamani siku ambayo maamuzi juu ya dhamana yao ilipangwa kutolewa kwa kile serikali kupitia magereza walidai gari la kuwaleta viongozi hao mahakamani lilikuwa limeharibika.Haya ebu jadili hoja zako sasa.
 
Soma na Katiba ya Tanzanzia ya 1977. Imeweka kuwa dhamana kwa mtuhumiwa ni haki yake na siyo ombi kwani imeweka "presumption of innocence".

Katiba hiyo inaruhusu maandamano na mikusanyiko huru kwa wananchi.
 
kwamba jpm ameingilia na wahuni?-hawa wahuni ndio akina bashite washauri wake
IMG-20180330-WA0060.jpeg
 
Wakati naandika sikutegemea kwamba kila mtu ataelewa kila kitu, ukizingatia kwamba kila mtu anaoupande wake ambao atakua anatumia katika kuangalia mambo.
Kwani lugha iliyotumika si Kiswahili na lugha ya Malkia unafikiri kila mtu ni mbumbumbu kama ccm
Njoo na waraka na sheria zoooote jibu ni moja
Mmelikoroga mnatafuta pa kutokea mtatia akili nyumbu
 
Zipo taarifa, kutokana na Picha zinazozunguka katika mitandao ya kijamii kwamba siku ya Tarehe 27 ya mwezi wa tatu(3) 2018, Chama cha Demokrasia na maendeleo kilifanya kikao cha chama ndani ya ofisi za jumuiya ya nchi za ulaya. Sina hakika sana na kilichofanyika kama kilifanyika , ila ninayo machache ya kuyajadili hapa;

Kikao hicho ni matokeo ya hatua ya serikali kupitia vyombo vyake vya kiulinzi na usalama pamoja na utoaji haki kuwafikisha mahakamani viongozi sita (6) wa Chadema kutokana na makosa mbali mbali yaliyofanyika mwezi mmoja kabla, yaliyopelekea kutokea kifo cha wanafunzi wa chuo cha usafirishaji NIT.

Tanzania kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa ( UN) ni mmojawapo wa nchi zilizokubaliana katika matumizi ya mikataba mbali mbali ya kimataifa inayotoa maelekezo ya nchi wanachama namna ya kufanya mambo yake ya ndani na jinsi ya kuhusiana na nchi nyingine.

Moja wapo ya mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeipitisha ni pamoja na United Nations Charter, ya mwaka 1945, International Covenant on civil and Political Rights ( 1966) na pia ni mwanachama wa mahakama ya kimataifa ya ICJ.

Ni kanuni ya kimataifa inayotambulika kwamba, hakuna Taifa lolote lenye mamlaka ya kuingilia mambo ya ndani ya Taifa jingine mwanachama kwa namna yoyote ile, iwe ni kwa matumizi ya nguvu ama la, kanuni hiyo ni zao la mikataba mbali mbali ya kimataifa kama ilivyonukuliwa hapo juu.

Kanuni hiyo, ilianza kutumika kuanzia miaka ya 1933 kupitia Ibara ya 15 ya mkataba wa kimataifa wa Covenant of the League of Nations na pia The Montevideo Convention on Rights and Duties of States ambayo kwa pamoja ilikataza mambo yafuatayo;

" The inteference with the freedom(uhuru), sovereignty ( mamlaka ya nchi) or other internal affairs (mambo ya ndani ya nchi) or the process of the governments of other states ( au shughuli(michakato) za/ya nchi husika)"

Kanuni hiyo, kama ilivyoaninishwa hapo juu, katika mikataba hiyo ya kimataifa, iliwekewa nguvu na Mkataba wa Umoja wa kimataifa wa mwaka 1945 ama UN Charter na katika maazimio mbali mbali.

UN Charter (1945) inatambua kanuni hiyo katika Ibara ya 2.4 na 2.7 kama ifuatavyo;

2. 4. All Members shall refrain in their international relations from the threat or use of force against the territorial integrity or political independence of any state, or in any other manner inconsistent with the Purposes of the United Nations.

2. 7. Nothing contained in the present Charter shall authorize the United Nations to intervene in matters which are essentially within the domestic jurisdiction of any state or shall require the Members to submit such matters to settlement under the present Charter; but this principle shall not prejudice the application of enforcement measures under Chapter VII.

Maazimio mbali mbali ya Umoja wa kimataifa kama Azimio Na. 2131(xx) la mwaka 1965, pia lilitambua kanuni hiyo ya kimataifa inayoweka katazo kwa nchi wanachama kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine.

Kwa kuzingatia kanuni hiyo, mahakama ya Kimataifa ya Utoaji haki ama ICJ, imetoa maamuzi kulingana na mashitaka yatokanayo na madai ya nchi moja kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, mfano mzuri ni shauri lile lihusulo nchi ya Nicaragua na Marekani mwaka 1986 na pia Congo na Uganda la mwaka 2005, tukianza na lile la marekani na Nicaragua Mahakama ya ICJ ilikua na haya ya kusema;

NICARAGUA VS USA, (Merits) ICJ Reports (1986),

"The principle of Non- Intervention involves the right of every foreign state to conduct its affairs without outside interference, though examples of trespass against this principle is not infrequent, the court considers that it is part and parcel of the customary international law....

The principle forbids all states or groups of states to intervene directly or indirectly in the internal or external affairs of the states.."

Katika shauri la Congo na Uganda mahakama ilikua na haya ya kusema,

DRC Vs UGANDA, ( Merits) ICJ Reports (2005),

" The principle of non -intervention prohibits a state to intervene directly , or indirectly, with or without armed force, in support of the internal opposition within a state".

Kitendo cha Jumuiya ya Ulaya kuruhusu Chadema kutumia premises zao katika kufanya mkutano wao, kimekwenda kinyuma na kanuni za kimataifa zinazokataza nchi kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, na kimevunja mikataba yote ya kimataifa.

Ikumbukwe kwamba makosa waliyoshitakiwa viongozi wa chadema, sio ya kisiasa, bali ni makosa ya kawaida kabisa ambayo mtu yetote ambaye ni Raia wa Tanzania anaweza kushitakiwa nayo, hivyo hakuna sheria yeyote iwe ya ndani au nje iliyovunjwa jambo ambalo lingewapa Jumuiya ya Ulaya uhuru wa kufanya walichokifanya na kwa kuzingatia kwamba viongozi wa chadema hawana kinga ya kushitakiwa.

Ibara ya 15 (2) ya International Covenant on Civil and Political Rights (1966) inasema, nanukuu;

" Art. 15 (2). Nothing in this article shall prejudice the trial and punishment of any per son for any act or omission which, at the time when it was committed, was criminal according to the general principles of law recognized by the community of nations".

Kwa kuzingatia hayo, ni dhahiri mambo haya yanatakiwa kufanyika;

(i) Jumuiya ya Ulaya kuomba radhi kwa hayo yaliyotokea,

(ii) Serikali Kupitia Waziri wa Mambo ya Nje na jumuiya ya afrika mashariki kutoa tamko kulaani kitendo hicho.

Ni waase tu ndugu zangu kuacha kufanya vitendo ambavyo vitazua mtafaruku bila ya kuwa na grounds zozote zile za kujustify vitendo vyao hivyo batili.
Mkuu Stroke,

Vifungu ulivyo-quote havina shida, viko sahihi na hata maelezo yako mengine.
Shida inakuja unapojaribu kuwatia hatiani watu ambao kwa vyovyote vile, hawajahatarisha hali ya usalama wa nchi kama unavyotaka tuamini.
Fikiri ikiwa wangefanya kikao hicho Court Yard, Blue Pearl au JNICC nini kingewatokea? Kama huwezi kufanya kikao hata kwenye ofisi yako unaweza kujiita uko huru?
Kama EU waliwaalika basi washitakini EU kwenye Baraza la Usalama la UN.
 
Soma na Katiba ya Tanzanzia ya 1977. Imeweka kuwa dhamana kwa mtuhumiwa ni haki yake na siyo ombi kwani imeweka "presumption of innocence".

Katiba hiyo inaruhusu maandamano na mikusanyiko huru kwa wananchi.
Nge umenifurahisha
 
Yapo maelezo na uzi upo hapa, kwamba walikua wakifanya kikao cha ndani katika premises za jumuiya ya Ulaya, meaning waliomba venue kwa ajili ya kufanya shughuli za kisiasa na wakakubaliwa. Mwisho wa siku ni kuwa Mikataba Tajwa katika article hii, imevunjwa yote.

..mimi nimependekeza Tz izifunge balozi za nje zinazokiuka mikataba ya kimataifa.
 
Yapo maelezo na uzi upo hapa, kwamba walikua wakifanya kikao cha ndani katika premises za jumuiya ya Ulaya, meaning waliomba venue kwa ajili ya kufanya shughuli za kisiasa na wakakubaliwa. Mwisho wa siku ni kuwa Mikataba Tajwa katika article hii, imevunjwa yote.
kasome viuri hujaelewa kilichoandikwa
 
Kwa lugha nyengine wanatakiwa kufukuzwa nchi maana kwa kushirikian na chadema wanaweza kupindua nchi
 
Zipo taarifa, kutokana na Picha zinazozunguka katika mitandao ya kijamii kwamba siku ya Tarehe 27 ya mwezi wa tatu(3) 2018, Chama cha Demokrasia na maendeleo kilifanya kikao cha chama ndani ya ofisi za jumuiya ya nchi za ulaya. Sina hakika sana na kilichofanyika kama kilifanyika , ila ninayo machache ya kuyajadili hapa;

Kikao hicho ni matokeo ya hatua ya serikali kupitia vyombo vyake vya kiulinzi na usalama pamoja na utoaji haki kuwafikisha mahakamani viongozi sita (6) wa Chadema kutokana na makosa mbali mbali yaliyofanyika mwezi mmoja kabla, yaliyopelekea kutokea kifo cha wanafunzi wa chuo cha usafirishaji NIT.

Tanzania kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa ( UN) ni mmojawapo wa nchi zilizokubaliana katika matumizi ya mikataba mbali mbali ya kimataifa inayotoa maelekezo ya nchi wanachama namna ya kufanya mambo yake ya ndani na jinsi ya kuhusiana na nchi nyingine.

Moja wapo ya mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeipitisha ni pamoja na United Nations Charter, ya mwaka 1945, International Covenant on civil and Political Rights ( 1966) na pia ni mwanachama wa mahakama ya kimataifa ya ICJ.

Ni kanuni ya kimataifa inayotambulika kwamba, hakuna Taifa lolote lenye mamlaka ya kuingilia mambo ya ndani ya Taifa jingine mwanachama kwa namna yoyote ile, iwe ni kwa matumizi ya nguvu ama la, kanuni hiyo ni zao la mikataba mbali mbali ya kimataifa kama ilivyonukuliwa hapo juu.

Kanuni hiyo, ilianza kutumika kuanzia miaka ya 1933 kupitia Ibara ya 15 ya mkataba wa kimataifa wa Covenant of the League of Nations na pia The Montevideo Convention on Rights and Duties of States ambayo kwa pamoja ilikataza mambo yafuatayo;

" The inteference with the freedom(uhuru), sovereignty ( mamlaka ya nchi) or other internal affairs (mambo ya ndani ya nchi) or the process of the governments of other states ( au shughuli(michakato) za/ya nchi husika)"

Kanuni hiyo, kama ilivyoaninishwa hapo juu, katika mikataba hiyo ya kimataifa, iliwekewa nguvu na Mkataba wa Umoja wa kimataifa wa mwaka 1945 ama UN Charter na katika maazimio mbali mbali.

UN Charter (1945) inatambua kanuni hiyo katika Ibara ya 2.4 na 2.7 kama ifuatavyo;

2. 4. All Members shall refrain in their international relations from the threat or use of force against the territorial integrity or political independence of any state, or in any other manner inconsistent with the Purposes of the United Nations.

2. 7. Nothing contained in the present Charter shall authorize the United Nations to intervene in matters which are essentially within the domestic jurisdiction of any state or shall require the Members to submit such matters to settlement under the present Charter; but this principle shall not prejudice the application of enforcement measures under Chapter VII.

Maazimio mbali mbali ya Umoja wa kimataifa kama Azimio Na. 2131(xx) la mwaka 1965, pia lilitambua kanuni hiyo ya kimataifa inayoweka katazo kwa nchi wanachama kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine.

Kwa kuzingatia kanuni hiyo, mahakama ya Kimataifa ya Utoaji haki ama ICJ, imetoa maamuzi kulingana na mashitaka yatokanayo na madai ya nchi moja kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, mfano mzuri ni shauri lile lihusulo nchi ya Nicaragua na Marekani mwaka 1986 na pia Congo na Uganda la mwaka 2005, tukianza na lile la marekani na Nicaragua Mahakama ya ICJ ilikua na haya ya kusema;

NICARAGUA VS USA, (Merits) ICJ Reports (1986),

"The principle of Non- Intervention involves the right of every foreign state to conduct its affairs without outside interference, though examples of trespass against this principle is not infrequent, the court considers that it is part and parcel of the customary international law....

The principle forbids all states or groups of states to intervene directly or indirectly in the internal or external affairs of the states.."

Katika shauri la Congo na Uganda mahakama ilikua na haya ya kusema,

DRC Vs UGANDA, ( Merits) ICJ Reports (2005),

" The principle of non -intervention prohibits a state to intervene directly , or indirectly, with or without armed force, in support of the internal opposition within a state".

Kitendo cha Jumuiya ya Ulaya kuruhusu Chadema kutumia premises zao katika kufanya mkutano wao, kimekwenda kinyuma na kanuni za kimataifa zinazokataza nchi kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, na kimevunja mikataba yote ya kimataifa.

Ikumbukwe kwamba makosa waliyoshitakiwa viongozi wa chadema, sio ya kisiasa, bali ni makosa ya kawaida kabisa ambayo mtu yetote ambaye ni Raia wa Tanzania anaweza kushitakiwa nayo, hivyo hakuna sheria yeyote iwe ya ndani au nje iliyovunjwa jambo ambalo lingewapa Jumuiya ya Ulaya uhuru wa kufanya walichokifanya na kwa kuzingatia kwamba viongozi wa chadema hawana kinga ya kushitakiwa.

Ibara ya 15 (2) ya International Covenant on Civil and Political Rights (1966) inasema, nanukuu;

" Art. 15 (2). Nothing in this article shall prejudice the trial and punishment of any per son for any act or omission which, at the time when it was committed, was criminal according to the general principles of law recognized by the community of nations".

Kwa kuzingatia hayo, ni dhahiri mambo haya yanatakiwa kufanyika;

(i) Jumuiya ya Ulaya kuomba radhi kwa hayo yaliyotokea,

(ii) Serikali Kupitia Waziri wa Mambo ya Nje na jumuiya ya afrika mashariki kutoa tamko kulaani kitendo hicho.

Ni waase tu ndugu zangu kuacha kufanya vitendo ambavyo vitazua mtafaruku bila ya kuwa na grounds zozote zile za kujustify vitendo vyao hivyo batili.
Sheria mama za kimataifa zinazobeba misingi ya sheria zote ni zile za human rights ambazo nchi yetu inazivunja kila siku,hizo zingine uwa hazina maana kama watu hawaheshimiki na wanauawa ovyo!
Mataifa makubwa wakishaona mnavunja articles za HRs makusudi basi watatafuta support ya wenyeji wachache wanaojielewa kisha watawala mnaonyeshwa kwa nguvu namna ya kuzitii hizo sheria. Mambo yalipofikia hakukuwa na namna zaidi ya kushirikiana na wenye dunia ...kumbuka mambo ya big fish kumla small fish,safari hii mtanyooka tu
 
maswala ya haki za kibinadamu utayasikia pale Serikali flani ya nchi ambayo imeozoea kuibiwa ikiwa serious kulinda rasilimali zake; ila ukiwapa mwanya wa kuiba hutasikia mambo kama hayo yakizungumzwa;

Ni kama vile haki ya kuiba imehalalishwa kwa baadhi ya mataifa na haki ya kulinda rasilimali kwa nchi maskini hugeuzwa kuwa uhalifu; na kwa kawaida hutafutwa watu wachache wenye Tamaaa ya madaraka na kupewa jukumu la kuvuruga mchakato mzima wa kuendelea kupitia rasilimali; Mara nyingi nchi hizo hujukuta wakiendelea kuwa maskini kwa muda mrefu kutokana na watu wa aina hiyo kutokosekana.
 
Back
Top Bottom