Kwanini Zanzibar haiwezi kushitaki au kushitakiwa kwenye mahakama/mabaraza ya Kimataifa

Ngamanya Kitangalala

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
501
1,214
Kwanza kabisa ili kuweza kuelewa dhana hii kwa ufasaha, ni LAZIMA upate fursa japo kwa uchache kusoma nyaraka zifuatazo

1. Katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977(The Constitution of the United Republic of Tanzania,1977)

2. Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, toleo 2010( The Constitution of Zanzibar,1984)

3. Statute of The International Court of Justice,1945

4. The Convention on the Settlement of the Investment Disputes between States and Nationals of other States,1966

5. Montevideo Convention on the Rights and Duties of States,1933

Sasa hapa tuangalie, Je Zanzibar anaweza kushitaki au kushitakiwa kwenye hiyo mahakama ya kimataifa ( The International Court of Justice) au kwenye kituo cha usuluhishi cha migogoro ya kimataifa ya uwekezaji ( The International Centre for Settlement of Investment Disputes) ?

Ukisoma, sura ya pili, ibara ya 34(1) ya Statute of The International Court of Justice,1945, inasema only States may be parties in the cases before court

Maana yake nimi?

Ni nchi( state) pekee are eligible to appear kwenye mahakama hii, mahakama hii HAINA jurisdiction ya ku deal na maombi kutoka kwa mtu binafsi ( Individual), mashirika yasiyo ya kiserikali( Non Govermental Organisation) au any private entity

Lakini pia ukisoma kwenye sura ya pili, ibara ya 25(1) ya ICSID CONVENTION, 1966,inasema kituo hiki cha usuluhishi kina jurisdiction ya ku deal na mashauri kati ya

1. Contracting state Vs Investor

2. Contacting state vs Contracting state

Contracting State ni nini?
Contracting state ni nchi zote ambazo zimeridhia( rectified) International Centre for Settlement of Investment Disputes Convention, mpaka sasa ni nchi 158

Kwa hiyo hapo, tunaona, pia ili uweze kupeleka shauri ICSID either uwe nchi( State) au mwekezaji( investor) kutoka kwenye Contracting state

Sasa tujiulize, Je Zanzibar ni nchi( State)?

Ukisoma katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, toleo la 2010 kwenye ibara ya 1, inasema Zanzibar ni NCHI ( state)

Kwenye ibara ya 2, ya kati hiyo, inasema Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda jamhuri ya muungano wa Tanzania

Lakini Ukisoma katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kwenye ibara ya 1, inasema Tanzania ni NCHI MOJA. na ni jamhuri ya muungano

☝🏿☝🏿☝🏿

Hivyo, ukiitazama Zanzibar kwa jicho la ndani ya mipaka ya jamhuri ya muungano wa Tanzania , utaona ZANZIBAR NI NCHI

Sasa tuitazame Zanzibar kwa jicho la kimataifa( International law)

Ukisoma Montevideo Convention, 1933 kwenye ibara ya 1, inataja sifa za nchi( state) kutambulika kama nchi kwenye sheria za kimataifa ni zifuatazo

1. Ni lazima nchi hiyo iwe permanent population

2. Ni lazima nchi hiyo iwe na mipaka inayotambulika( Defined territory)

3. Ni lazima nchi hiyo iwe na serikali

4. NI lazima nchi hiyo iwe na uwezo wa kuingia kwenye mahusiano na nchi ingine(Capicity to enter into relations with other states )

Sasa ukiangalia hapo, utaona ZANZIBAR inazo sifa zote hapo juu, kasoro sfa namba 4

Zanzibar HAINA uwezo wa kuingia kwenye mahusiano na nchi zingine

Hivyo basi, ukiitazama Zanzibar kwa jicho la kimataifa, ZANZIBAR SIO NCHI ( STATE)

Ndio maana Zanzibar HAIWEZI kushitaki wala kushitakiwa kwenye

1. International Court of Justice

2. International Centre for Settlement of Investment Disputes

Itashitakiwa nchi ya jamhuri ya muungano wa Tanzania (The United Republic of Tanzania)
 
Back
Top Bottom