Mkutano wa Chadema M4C-Iringa wasitishwa!

Mkutano wa Chadema M4C-Iringa wasitishwa!

Nzenzu

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2011
Posts
858
Reaction score
164
Ulipangwa kufanyika leo trh 28 August, 2012 kuanzia mida ya saa 8 mchana katika viwanja vya mwembetogwa. Sababu ni zile zile za kiintelejensia na kupisha zoezi la Sensa linaloendelea sasa!

[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Polisi wazuia mikutano ya Chadema Iringa
[/TD]
[TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Tuesday, 28 August 2012 23:00 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
Waandishi Wetu
Mwananchi

VUTA nikuvute baina ya Polisi na Chadema imehamia Iringa, ambako jeshi hilo limezuia maandamano na mikutano yote ya chama hicho iliyokuwa imepangwa kufanyika kwa siku nane kuanzia jana.
Amri hiyo ya polisi imekuja siku moja baada ya kutokea vurugu kubwa mjini Morogoro, baina ya wafuasi wa chama hicho na polisi na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wawili kujeruhiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamhanda alisema jana kuwa wameamua kuzuia maandamano na mikutano ya Chadema iliyopangwa kuanza jana kutokana na Sensa ya Watu na Makazi.
"Kutokana na hali halisi ya Sensa, tumeamua kuzuia maandamano na mikutano yote ya vyama vya kisiasa mkoani Iringa wakiwamo hawa watu wa Chadema," alisema.
Alisema kabla ya kuwazuia, walikutana na viongozi wa chama hicho Wilaya ya Iringa na kuwataka wazuie mikutano yao, jambo ambalo alisema walilikubali kwa ‘mbinde'.

Dk Slaa: Wametuomba
Awali, akiwa Mjini Morogoro, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema polisi wamekiomba chama hicho kusitisha maandamano na mikutano yake iliyopangwa kufanyika mkoani Iringa kupisha Sensa ya Watu na Makazi.

Alisema Chadema imekubali ombi hilo lililotolewa na Mkuu wa Polisi, IGP Said Mwema hivyo kuamua kusitisha mkutano wake uliopangwa kufanyika katika Viwanja vya Mwembetogwa, Iringa jana.

"Juzi Agosti 27, 1:00 usiku tulipata barua kutoka Jeshi la Polisi Iringa iliyokubali Chadema kufanya maandamano wakiwa ndani ya magari na si matembezi ya miguu, lakini baadaye saa 3:00 usiku, tulipigiwa simu na OCD wa Iringa akitujulisha kuwa maandamano yao yamebatilishwa na kutengua mambo yote tuliyoafikiana mwanzo," alisema Dk Slaa na kuongeza:

"Asubuhi ya leo (jana) tulipigiwa simu na RPC (wa Iringa) na kudai kuwa wanataka kuonana na viongozi wa Chadema, huku wakiwa na hoja kuwa tuahirishe kufanya mkutano kutokana na Sensa.
Hoja nyingine ambayo mimi naona ni ya upuuzi ni ile ya kusema kwamba wananchi wa Iringa watakuwa wameathirika na kifo cha kijana aliyekufa Morogoro," alisema Dk Slaa.

Alisema baada ya kutokubaliana na hoja hizo, alipigiwa simu na IGP Mwema akimwomba asitishe mkutano na maandamano ya mkoani Iringa kwa kuwa hiyo ni amri kwa vyama vyote vya siasa na si Chadema pekee.

"Nimeongea na IGP leo kwa dakika zaidi ya 40 akisema Dk Slaa sijawahi kukuomba hata siku moja, naomba nikuombe na usinikatalie kati ya siku nne hadi tano kuanzia sasa tumezuia vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara kutokana na kuwapo kwa Sensa naomba tuelewane," alisema Dk Slaa akimnukuu IGP Mwema.

Vurugu za Morogoro
Juzi, chama hicho kikuu cha upinzani kilifanya maandamano mjini Morogoro na kuzua taharuki, baada ya kutokea vurugu wakati polisi walipoamua kuyasambaratisha na kusababisha mauaji ya mtu mmoja, Ally Zona (38) mkazi wa Kihonda

Akizungumzia kifo hicho, Dk Slaa alisema chama chake kitashiriki kikamilifu katika mazishi ya kijana huyo kulingana na ratiba ya ndugu wa marehemu.

"Endapo familia itaamua kusoma dua hapa Morogoro na kuzika hapa, tutashiriki kikamilifu. Tumejadiliana na wanafamilia kuna mambo ya msingi tumekubaliana na walichoomba ni kusaidia kusafirisha mwili. Hatutajali itikadi aliyokuwa nayo marehemu," alisema.

Nchimbi achunguza
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi ametuma kikosi maalumu mkoani Morogoro kuchunguza mauaji ya kijana huyo anayedaiwa kupigwa risasi na polisi katika vurugu hizo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Dk Nchimbi alisema Serikali imesikitishwa na tukio hilo hivyo itahakikisha uchunguzi unafanywa na hatua kuchukuliwa kwa watakaobainika kuhusika.

Alisema polisi walipata taarifa ya kuwapo kwa mtu mwenye majeraha umbali wa mita 300 kutoka eneo la tukio na kwamba wasamaria wema walimchukua na kumpeleka hospitali ambako alifariki dunia.
Aliishutumu Chadema kwa kukaidi amri ya polisi iliyowataka wasiandamane.

UVCCM yalaani
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umekishutumu Chadema ukisema kimehusika na mauaji ya kijana Zona yaliyotokea juzi mjini Morogoro.

Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela alisema: "Tunatoa pole kwa vijana na wananchi wa Morogoro kwa kuondokewa na kijana wao na tunataka uchunguzi ufanyike haraka ili wajulikane waliofanya kitendo hicho."
"Haiingii akilini kusema Jeshi la Polisi linahusika wakati wafuasi wa Chadema walikuwa wanaonekana vizuri kwa sare zao halafu wawaache na kwenda kumuua mtu aliyekuwa anaendelea na shughuli zake za uuzaji wa magazeti."

Habari hii imeandikwa na Nora Damian, Tausi Ally, Habiba Yahya na Lilian Lucas na Clement Sanga.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Blessing in disguise ... huu itakuwa ni kudanganya muafaka kuhudhuria mazishi ya kijinga Ally aliyepigwa risasi na polisi
 
Ulipanga kufanyika leo trh 28 August, 2012 kuanzia mida ya saa 8 mchana katika viwanja vya mwembetogwa. Sababu ni zile zile za kiintelejensia na kupisha zoezi la Sensa linaloendelea sasa!
Well done polisi, msikubali watu wachache wenye uchu wa madaraka kumwaga damu za watanzania kwa mtaji wao wa kisiasa. Hakuna uhuru usio kuwa na mipaka !
 
Ulipanga kufanyika leo trh 28 August, 2012 kuanzia mida ya saa 8 mchana katika viwanja vya mwembetogwa. Sababu ni zile zile za kiintelejensia na kupisha zoezi la Sensa linaloendelea sasa!

Good decision
 
Well done polisi, msikubali watu wachache wenye uchu wa madaraka kumwaga damu za watanzania kwa mtaji wao wa kisiasa. Hakuna uhuru usio kuwa na mipaka !

unavyosema hivyo huyo ally kawawa na police ama cdm? Acha unafiki
 
Well done polisi, msikubali watu wachache wenye uchu wa madaraka kumwaga damu za watanzania kwa mtaji wao wa kisiasa. Hakuna uhuru usio kuwa na mipaka !
nawe unadhani hao polisi hawana uchu wa kupata 'vya bure' na ndio kisa cha kufanya hayo yote!?
Hii ni kwa sababu:
- Chama dhaifu huzaa serikali dhaifu
- serikali dhaifu huzaa taasisi dhaifu (Police inclusive)
- Taasisi dhaifu nazo huzaa matokeo dhaifu (maendeleo)
 
Well done polisi, msikubali watu wachache wenye uchu wa madaraka kumwaga damu za watanzania kwa mtaji wao wa kisiasa. Hakuna uhuru usio kuwa na mipaka !
Kuna watu wanafikiri hii ni nchi yao peke yao, uoga wa M4C umewafanya washindwe kifikiri kabisa. M4C haitasimama mpaka kieleweke. Cha moto mtakiona.

Habari ndio hii hapa chini. Na inakuja Iringa

483695089.jpg
 
Well done polisi, msikubali watu wachache wenye uchu wa madaraka kumwaga damu za watanzania kwa mtaji wao wa kisiasa. Hakuna uhuru usio kuwa na mipaka !

serikali ya kiwete inazidi kuanikwa uchi. atajuta kulazmisha kuwa RAIS
 
Well done polisi, msikubali watu wachache wenye uchu wa madaraka kumwaga damu za watanzania kwa mtaji wao wa kisiasa. Hakuna uhuru usio kuwa na mipaka !

Wewe ni crazyBrain!

Unataka kutuambia uhuru wa mipaka ni kuzuia maandamano ya CHADEMA lakini maandamano ya CCM ruksa!

Hivi for your tiny and small Brain, unafikiri Watanzania wote ni wapuuzi na wajinga kama wewe? Sahau! Watanzania wanajua wanachokifanya na kwa taarifa yako tu jinsi Policcm wanavyoendelea kuua na kujaribu kuzuia maandamano ya wapinzani hususan CHADEMA ujue tu CCM wanaendelea KUSAFISHA NJIA YA CHADEMA KUINGIA IKULU 2015!

Wewe subiri 2015 utaelewa ninachomaanisha.
 
serikali ya kiwete inazidi kuanikwa uchi. atajuta kulazmisha kuwa RAIS
Nchi imetulia , na mambo yanaenda kama kawaida including kukusanya kodi yako kwa maendeleo ya nchi, tutasimamia sheria na hatoogopwa mtu. Huu ni utawala wa sheria na sio utawala wakimangi wa CDM
 
Ikiwa mkutano umehairishwa kwasababu ya msiba,.. ita "hold water" zaidi lakini kupisha zoezi la sensa..Mhh hapana!!...
Damu ya Ally Zona imemwagika katika mazingira ya harakati za kupigania utu na demokrasia katika ardhi ya MAIGIZO ya Demokrasia na haki...Kitendo cha kuipuuza na kuendelea na operation kitatoa picha ya tofauti juu ya lengo hasa la Operation M4C!!..
Ikiwa CDM watapostpon ziara ya Iringa hata kwa wiki zaidi,..ntaendelea kuwaamini zaidi.Maana ninaujua umuhimu wa kujenga Imani hapa Morogoro miongoni mwa mioyo ya watu hapa,..Kwanza hii ilikua ngome imara ya CCM kwa wakati wote (kabla ya mwezi uliopita)..Wakati Iringa Imeshakombolewa ni sehemu ndogo tu imebakia,.ambayo hata Rev Msigwa na Abwao wanaweza kumalizia,.Tusiwe na haraka huku tukiacha hawa wenzetu tuliotoka kuwakomboa wakiwa njia panda!!..
Makamanda naomba Tubaki hapa Moro,.Tuwape Moyo wa Kusonga mbele na utayari wa kupigania haki hata kwa damu yetu wenyewe...Tuwaondoe woga, wachache wanaonesha hali ya kutaka kukata tamaa,.Tuwashike mkono twende nao!!
 
Well done polisi, msikubali watu wachache wenye uchu wa madaraka kumwaga damu za watanzania kwa mtaji wao wa kisiasa. Hakuna uhuru usio kuwa na mipaka !
GAMBA linaleta mambo ya kipuuzi... uchu wa madaraka unaonekana kwa kuandamana na kufanya mikutano ya amani?... Polisi waue kwa kuagizwa na CCM na ninyi mtetee!!!!!... Ni muhimu vifo hivi viwaguse wauaji na mashabiki wake ili nao wajue uchungu wa kupoteza ndugu!...
 
watabana mwisho wataachia, sensa ikimalizika watasingizia nn?
 
Wewe ni crazyBrain!

Unataka kutuambia uhuru wa mipaka ni kuzuia maandamano ya CHADEMA lakini maandamano ya CCM ruksa!

Hivi for your tiny and small Brain, unafikiri Watanzania wote ni wapuuzi na wajinga kama wewe? Sahau! Watanzania wanajua wanachokifanya na kwa taarifa yako tu jinsi Policcm wanavyoendelea kuua na kujaribu kuzuia maandamano ya wapinzani hususan CHADEMA ujue tu CCM wanaendelea KUSAFISHA NJIA YA CHADEMA KUINGIA IKULU 2015!

Wewe subiri 2015 utaelewa ninachomaanisha.
Ni ndoto za mchana kwa CDM kuingia ikulu sio tu 2015 hata 3000, haipo . Na usidhanie kuingia ikulu ni kwa kile kikaratasi chhako unacho tumbukiza kwenye boksi, ni zaidi ya hapo, sasa utatumia njia gani km hiyo itashindwa? CDM ni sawa na kuku wa kuchora, hadonoi, hali, hawiki na hafai kwa nyama wala mayai
 
GAMBA linaleta mambo ya kipuuzi... uchu wa madaraka unaonekana kwa kuandamana na kufanya mikutano ya amani?... Polisi waue kwa kuagizwa na CCM na ninyi mtetee!!!!!... Ni muhimu vifo hivi viwaguse wauaji na mashabiki wake ili nao wajue uchungu wa kupoteza ndugu!...
CCM ni watu wakufuata sheria na wanajua sheria, ila wenzetu ni watu wakutumia nguvu na kuacha sheria, ndio maana wao hawauliwi kwani hawafanyi fujo. Hakuna maandamano bila kibali, sasa kibali mlikuwa nacho? na mliambiwa msiandamane ila mkalazimisha, huko sio kumwaga damu kwa dhamira za uchu wa madaraka?
 
Hata polisi wasipoingilia kati CDM iko msibani. Iringa M4C inasimama!.... HUU NI MSIBA MKUBWA SAANA KWA CDM!.
 
Back
Top Bottom