Asubuhi hii nimepita maeneo ya mjini iringa, nikafika sehemu kupata supu, akaingia jamaa mmoja akakaa meza moja na mimi, mara simu yake ikanza kuita, akawa anaongea kwa hasira na uchungu. Mwishowe akawa anamtia moyo huyo mpigaji kuwa msikate tamaa, hawa jamaa wahuni wanaweza kuzua kisingizio hata wakamtumia daktari kudanganya watu kuwa kuna magonjwa ya mlipuko, ili mradi chadema wasifanikiwe kufanya mkutano.
Alipomaliza kuongea nikaanza kuongea naye, akaniambia kuwa mkutano wa chadema unazuiliwa tena, ila sababu ya msingi haionekani. Nilipotoka pale nikapita maeneo ya m.r. Hotel, nikakuta magari ya m4c yamajazana pale na wanatimu kibao wakiwepo kashidye wa igunga. Lakini sikuona shamra shamra zozote, inaonekana kama wanajaadiliana jambo.
Samahani kwa kutokuweka picha ila kama nilivyosema, ni tetesi tuu, naendelea kufuatilia.