Mkutano wa CHADEMA Kuwashukuru watu wa Mbeya

Mkutano wa CHADEMA Kuwashukuru watu wa Mbeya

Hizo gear nyeusi ndo gwanda jipya la chadema?
security_5897936-655x280.jpg


65HRX63D1security_guard_tshirtp235713554308640898zvkhk_400.jpg
 
Huyo jamaa na nguo zake za kimasai is toomuch,halafu hao walinzi sijui,sijui ninja wanakazi gani? kwani haukuwa mkutano wa amani? hao ndio wanapigaga watu na vitu vya chuma baadae msingizie police
 
attachment.php


attachment.php


Kwa mikwala basi na mbwembwe CDM ndio wenyewe na maninja tena (hivi kwanza ninja mpaka ajichore kwenye nguo ya uso ndio tumjue).

Halafu huyo anaelindwa hadharani hivyo baadae anaingia bar kulewa akiwa mwenyewe, sasa sijui assasin gani atakaetaka kupoteza muda wa kufukuzana na polisi wakati target is accessible easily hata bar-tender anaweza mzuru.
 
Chama cha Demokrasia na maendeleo kimeendelea kufanya mikutano katika mkoa mbeya ya kuwashukuru wananchi kwa uamuzi wao wa kikikataa ccm na kuiamini CHADEMA katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana 2014.jana ilikuwa ni zamu ya mbeya jiji.mkutano huo uliofana mgeni rasm alikuwa Mh.SUGU akiambatana na mbunge wa Iringa mjini Mh.msigwa,pro.jay,makamu mwenyekiti bavicha taifa,mwenyekiti bavicha mkoa wa Mbeya,mwenyekiti bawacha mkoa wa mbeya.
picha inayonyeshwa kwamwitikio,mahudhurio ya wananchi kwenye mikutano hiyo,ni wazi ccm hawana nafasi tena mkoa wa mbeya.wameamua kuikataa ccm kutokana na madhambi yake.mh. sugu pia aliutumia mkutano huo kuwasihi wananchi kujiandkisha kwa wingi katika daftari jipya la wapiga kura,alisisitiza umihimu wa kujiandikisha kwa wingi ili kufanikisha azma ya kuindoa ccm madarakani,alitoa mfano uchaguzi wa serikari za mitaa uliopita ambao CCM kimeshinda katika maeneo ambao waliojiandikisha idadi ya ilikuwa ndogo.aliongeza kuwa pamoja CCM kuizidi CHADEMA viti vichache hasa maeneo ya pembezoni bado CDM ndicho kilichopata kura nyingi za jumla jiji zima kwa kuizid ccm kura zaidi ya 20 elfu.akatania kwa kusema "uku mbeya tuna viaz na ndizi kijana akiwa na miaka 15 wengi wanakua na miili mikubwa ukiona kijana wako hajafikisha miaka 18 lakini ana mwili mkubwa,mpeleke akajiandikishe,ili tuiondoe ccm,tumechoka"watu wakaangua kicheko.
aligusia utizamizaji wa ahadi zake wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2010 na kusisitiza kuwa kwa kiasi kikubwa zimetekelezwa,kuhakikisha hakuna mtoto anaeshindwa kujiunga na elimu ya sekondari kwa sababu ya kukosa uwezo,aliueleza mkutno kuwa anao watoto zaidi ya 200 bila kuhusisha wanaojiunga mwaka huu,ambao anawahudumia adfa,sare ikibidi mpaka daftari,aliwasihi viongozi waliochaguliwa kwenda kuwatumikia wananchi na kuwa waadilifu wajitofautishe na viongoz wa ccm ambao wengi walizuia habari za mfuko wa elimu zisiwafikie wananchi kwa hofu ya CDM kuzidi kupata umaarufu.ahadi ya kuanzisha madarasa ya komputer inatekelezwa kwa awamu awam hii shule 5 zimefaulu ufungaji wa computer unaendelea,kwa upande wa barabara alisema ninyi wananchi ni mashahidi n a wanajua kinachoendelea waache [ccm]waendelee kusema ni za WB,sijui kopo,n.k ata kama ni za saccos cha tumezisimamia hizo fedha zimetimiza lengo.kuhusu soko la mwanjelwa alimlaumu meya na timu yake kukwamisha mradi na kuisababishia jiji hasara kwa kulipa liba ya zaid ya ml.100 kwa mwezi uku mradi haujakamilika kwa uzembe wa halm na meya maana tatizo sio pesa bali ni usimamizi.aliwaomba wananchi kuipa CDM viti vingi vya udiwani hapo OCT ili waweze kuingoza halm ya jiji kwa manufaa ya wananchi.
Nae pro.jay mwana wa Msolopa Ganzi,mzee wa mtulinga,mtainia wa jimbo la mikumi uchaguzi wa october aliwashukuru wananchi wa mkoa wa mbeya kwa mwamko wao wa kisiasa na kuwa chachu ya mikoa mingine kuiga kinachoendelea mbeya,akawasihi kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura pia kuitosa katiba ya mzee six.
Mh.Msigwa alihutubia na kuendelea kuto elimu na kuwasihi wananchi kutokubweteka na matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwani huo ni mwanzo wa mapambano kamili ili kupata uhuru kamili.mchungiji kwa kweli ni jembe.
makamu mwenyekiti wa BAVICHA nae aliwasalimu wananchi na kuwaacha hoi kwa swaga zake za kimasai kwa ufupi,kila aliekuwepo alikubali kuwa huyu ni jembe,ingekuwa unyakyusani tungemwambia Lukuvi "aheri Lukufi"Aheri ccm
 
CHADEMA uongo wenu na maigizo yenu yanadhihirika sasa.

Walinzi wote hao wa nini? kwa kiongozi anayependwa na watu?

NGUVU ya UMMA ingetosha kumlinda huyu" RAIS WA MBEYA" !


hapa mnajiandaa kwa vita gani? WWIII?
 

Attachments

  • 1.jpg
    1.jpg
    9.4 KB · Views: 97
  • 3.jpg
    3.jpg
    9.3 KB · Views: 82
huyo muhuni hapo nyuma ya SUGU ni msanii mwezie na SUGU aitwa C-MURDER, yeye na dereva wa hilo gari ajulikanaye kama BBG ambaye pia ni DJ wa SUGU ndio wanaomletea SUGU bangi na huwa wanavuta wote.

View attachment 217071

DSC03385.jpg
​
Rais Jakaya Kikwete akifuta machozi huku akiangaliwa na Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt, wakati ndege iliyombeba mgeni wake, Rais Barack Obama wa Marekani ikiruka angani.
 
Bwana alitoa.... Bwana Ametwaa.....

Born 5th Feb 1977 - Died 30th October 2015. (R.I.P)
 
Huyo jamaa na nguo zake za kimasai is toomuch,halafu hao walinzi sijui,sijui ninja wanakazi gani? kwani haukuwa mkutano wa amani? hao ndio wanapigaga watu na vitu vya chuma baadae msingizie police

Huna hoja mbulura wewe!
 
DSC03385.jpg
​
Rais Jakaya Kikwete akifuta machozi huku akiangaliwa na Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt, wakati ndege iliyombeba mgeni wake, Rais Barack Obama wa Marekani ikiruka angani.

Anamlilia Bwana wake
 
Back
Top Bottom