Mkutano wa CCM Kizota, Novemba 11-13, 2012

Mkutano wa CCM Kizota, Novemba 11-13, 2012

Mbona jk mishipa imemsimama sana usoni..ni uzee au amepanic
 
Kila ngazi itambue wajibu wa kujitegemea kwa kutumia fursa zilizopo kwa kila eneo
 
Huu si uungwana ccm bara na visiwani itakuwaje sehmu kama bara iwe sawa na visiwani? u,e nikama mkoa tu utawezaje kuchua 50% ya wana ccm? hapo kunaulakini kama hawajaliona hili nao ni kutumika wala si kujua nini wanachokifanya kweli ccm ni full mziki tena bolingo
 
Hii movie nzuri sana. Wakimaliza na kuamua tuambieni. Wengine movie ni bora kuliko kuangalia huo mkutano!
 
Uvccm na uwt wameweza kujenga majengo makubwa,kwanini sisi chama tushindwe?
 
CCM wamezinduka na sasa vita vyao wamehamishia kwenye twitter nawaonea huruma wazee kama akina Mukama, Mangula & Co ndani ya Chama ambao hawajui maana ya twitter.

Hii kitu twitter inaweza kuwa ni hatari na nzuri sana lakini msisahau kuwa ndio imeangusha tawala zate kwenye Arab spring

Msisahau kuwa JF nayo ipo kwenye twitter

8E9U3967.JPG
 
JK anasema yeye na Chiligati walianza kuwa makada pindi tu walipomaliza chuo 1975 baada ya kujiunga na TANU. Baadae anasema ndiyo wakaja akina Lowasa.

Anasisitiza chama kujitegemea japokuwa hajui nchi hii toka uhuru tumeshindwa kujitegemea!!!!

Anakandia utaratibu wa kuchangisha matajiri, anasema siku wakikuchoka basi tena, anasisitiza juu ya utaratibu endelevu wa mapato ili chama kisimamie.

Anakiri kuwa upinzani sana umeanza kukomaa na siku zijazo kuna uwezekano wa kura kupungua (wabunge) hivyo kunaweza kupelekea ruzuku kupungua.
 
JK asema inabidi watafute vyanzo vingine vya fedha kuliko kutegemea ruzuku maana wapinzani wameipunguza na wanaendelea kuipunguza kwa kuchukua idadi kubwa ya wapiga kura.
 
Huu si uungwana ccm bara na visiwani itakuwaje sehmu kama bara iwe sawa na visiwani? u,e nikama mkoa tu utawezaje kuchua 50% ya wana ccm? hapo kunaulakini kama hawajaliona hili nao ni kutumika wala si kujua nini wanachokifanya kweli ccm ni full mziki tena bolingo

Swali hilo hata mimi nimejiuliza sana, lakini akitokea mtu kuhoji jambo kama hilo ambalo lipo wazi ataambiwa ni kambi ya Lowasa wakati jambo kama hilo halihitaji kuwa na PHD ndiyo utambue.
 
Mageuzi ndani ya chama yanategemea uwepo wa makada wazuri wa kukisaidia chama
 
Kuwe na program maalum kwa ajili ya mageuzi ndani ya chama
 
Anasikia kizunguzungu, hachelewi kusema, Mambo mambo mamboooooooo, then chini. Kama yaleyale ya mnazi mmoja
 
kama ni bug, ni bora wasimweke live, hawezi tuliza akili kama atasikiliza minong`ono ya chini kwa chini ktk podium.
 
Wanabodi nipo ninafuatilia mkutano mkuu wa ccm kupitia runinga. Jambo moja lililonigusa ni uungwana wa Kikwete kukiri kwamba kwa sasa upinzani umekomaa sana na hauwezi kulinganishwa na ule dhaifu wa 1995. Hoja hii ameitoa pale alipokuwa akiwasisitiza wajumbe kuona umuhimu wa kuwa na vyanzo mbadala vya mapato kuliko kutegemea ruzuku ambayo inategemea idadi ya kura. Alienda mbali zaidi kwa kusema kuwa upinzani sasa unafanya vizuri zaidi na huko tunakokwenda ndio watafanya vizuri zaidi. Je Kikwete anaiandaa ccm kuwa chama cha upinzani?
 
Back
Top Bottom