Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,214
- 3,587
Marais wa dola mbili nguli wa siasa, uchumi na biashara, ulinzi na usalama; wenye nguvu za turufu duniani wamekutana kujadili mustakabali wa diplomasia baina yao zikiwemo agenda za mnyororo wa ugavi (biashara), hatima ya Taiwan, Olympics Beijing, muingiliano wa ki-uhamiaji, haki za binadamu, hali ya hewa duniani kufuatia COP26 Climate Summit in Glasgow, Scotland. Mkutano huo ulifanyika Jumatatu usiku 15 Novemba, 2021 kwa njia ya mtandao (virtual meeting).
Aidha, mkutano huo ulitazamiwa kurekebisha dosari za kidiplomasia zilizojiri wakati wa utawala wa Republican kupitia Rais Mstaafu Donald Trump dhidi ya Mamlaka ya Beijing hususan kwenye tasnia za biashara, afya (mlipuko wa kirusi cha Corona), upendeleo wa WHO kwa China dhidi ya US kwa habari ya Covid-19 nk. Dunia ilitega masikio kutaka kujuwa mustakabali wake wanapokutana mafahari hawa wawili.
Mataifa haya yana ushindani mkali wa kimaendeleo licha ya tofauti kubwa sana ya umri wao wa miaka 173 (zaidi ya karne moja na nusu) US miaka 245 na China miaka 72 (yaani China ilipata uhuru US ikiwa tayari ina miaka 173 ya uhuru), ambapo China imejituma kwa spidi kali hadi kuifikia US kimaendeleo. Bila shaka dunia inalo la kujifunza kwa China.
Taswira kwa hisani ya Google