Mkurugenzi wa VODACOM, TIGO, ZANTEL, TTCL, AIRTEL pitieni hapa, huwenda kukawa kuna faida kwenu

hiyo njia ni ndefu, pia itahitaji mpesa wapate commission.

Kuibiwa hakuwezi kwepeka. inategemea na inteligensia ya muuzaji na mnunuaji.

kitu ninachokiona ni kibaya ni pale unauza kitu, unatumiwa muamala feki au unatumiwa pesa inaingia halafu mtu anapiga simu kuomba irudishwe as if amekosea muamala.

cha kufanya ni issue moja.

Muuzaji awe na uwezo wa kutengeneza quote. ambayo ina maelezo na bei ya huduma au bidhaa inayouzwa na kisha kisha mlipaji atapewa quote ya namba kisha itakuwa reference wakati analipa pesa.

So hapa tutaepuka miamala feki ike inayokujaga na Msg ya Mpesa/ Tigopesa pia pesa ikiingia kwenye hiyo quote, mnunuaji hawezi reverse muamala mpaka makubaliano maalum
 
Safari on Kenya wana hii kitu
 
Wazo zuri...ila badi halijakidhi haja 100% ya lengo tarajiwa.

1. Vipi pale mnunuzi anapokuwa hana uamjnifu na hatumi hizo namba za uthibitisho kwa muuzaji baada ya kupokea bidhaa??

2. Mtandao wa simu unakuwa na uthibitisho gani wa kuwa bidhaa imefika au haijafika pale mnunuzi unapoamua kutotuma code ya uthibitisho ??

3. Mitandao ya simu inakuwa inabeba dhamana ya mtu wa kati kati..Je,wanafaidikaje na muamala huu ukiacha ada za kawaida za utumaji na kupokea ??
 
wazo zuri ila halitekelezeki sababu kuna mambo yanafanyika nje ya mfumo na inahitaji tena uaminifu wa muuzaji na mnunuzi kukamilisha, chukua mfano wa aliexpress ukilipia kitu pesa wanakaa nayo wao mzigo ukifika seller ndio analipwa hii njia kwao inawezekana sababu wana tracking system ya kujua mzigo ulipo toka umetumwa.
Njia rahis ini kumtuma mtu aukague mzigo kabla hujanunua au tuwe na mfuoma kama wa amazoni au aliepress katika kufanya manunuzi.
 
Bado bado bado sana, una wazo zuri sana lakini bado wazo lako haliwezi kufanya kazi kwa ufanisi.

Mfano, kuna ile ukienda kutoa pesa kwenye ATM huwezi kuchukua pesa kama hujatoa kadi, post n kwann.? Watz sisi tukishapata tunachokihitaji hatuwezi kumkumbuka aliyetusaidia, vp kama nimepata mzigo lkn sijathibitisha.?

Nadhani tuendelee hv hv na ibaki kuwa na uaminifu kati ya muuzaji na mnunuzi.
 
1- Mnunuzi akiwa hana uwaminifu ni kwamba hiyo pesa aliyotuma hataweza kuitoa wala kuirejesha kwenye accounta yake. Sasa sidhani kama mtu umepokea mzigo ambao ni wenyewe, na pesa umeshalipa inachobakia ni kuthibitisha ili mtu apokee, kwasababu hata usipo thibitisha pesa hairudi kwako inabakia kwa mtandao husika.

2-Mtandao wa simu hauhusiki na kufika kwa bidhaa, wao wanachotoa ni code za uthibitisho ili kuridhia pesa iyondoke, yaani wanakuwa wameikamata wao kwa hiyo ukiweka hizo code wanaiyachia inakwenda.

3-Makato yanakuwa pale pale kama M PESA ya kawaida. Sema hichi kinakuwa ni kipengele ndani ya M PESA

Kwa namna hii voda watashikilia pesa hadi wachokee na itawalazimu wawe na mahakama yao
 
1- Mnunuzi akiwa hana uwaminifu ni kwamba hiyo pesa aliyotuma hataweza kuitoa wala kuirejesha kwenye accounta yake. Sasa sidhani kama mtu umepokea mzigo ambao ni wenyewe, na pesa umeshalipa inachobakia ni kuthibitisha ili mtu apokee, kwasababu hata usipo thibitisha pesa hairudi kwako inabakia kwa mtandao husika.

2-Mtandao wa simu hauhusiki na kufika kwa bidhaa, wao wanachotoa ni code za uthibitisho ili kuridhia pesa iyondoke, yaani wanakuwa wameikamata wao kwa hiyo ukiweka hizo code wanaiyachia inakwenda.

3-Makato yanakuwa pale pale kama M PESA ya kawaida. Sema hichi kinakuwa ni kipengele ndani ya M PESA
Hakika wazo ni zuri lakini bado kuna maeneo ya muhimu hayajatatuliwa.

1. Umesema mnunuzi hawezi kurudisha fedha baada ya kulipa..Sasa je,akiletewa bidhaa ambayo siyo ya vigezo vyake inakuwaje ??

Nadhani ili huu mfumo ufanye kazi lazima kuwe na self reversal (Mnunuzi kueeza kurudisha fedha zake pale ambapo bidhaa inakiwa tofauti na alichoagiza).

2. Kwa mitandao ya simu,hii ni huduma ya nyongeza (add on) hivyo ni lazima gharama za ziada ziwepo.Kazi ya kuwa verifier au middleman ni risk na lazima mitandao itranslate risk hii kwa malipo.
 
LIPA KWA UTHIBITISHO

Kutokana na wimbi kubwa la utapeli mitandaoni, kundi hili hupelekea biashara zingine za mtandaoni zilizo halali kufifizwa na kutoaminiwa. Hivyo kuwakosesha riziki wale wafanya biashara waaminifu mtandaoni. Kwasababu maisha ya sasa hayawezi kwenda bila mitandao ya kijamii, bishara na huduma zote zimehamia huko.

Hii ni njia ambayo itawasaidia wanunuzi na wauzaji wa bishara kwa njia ya mtandao, ambapo muuzaji atapoakea pesa ya muamala wa malipo lakini hataweza kuitoa pesa hiyo mpaka ithibitishwe na mnunuzi au mlipaji baada ya kupokea mzigo husika.

Jinsi mfumo ulivvyo

Mnunuzi amekiona kitu mtandaoni, kisha anatakiwa akilipie hicho kitu kwa njia ya muamala kabla ya kukipokea au kabla hakijamfikia, sasa njia hii itamruhusu mnunuzi kulipia hiyo bidhaa bila hofu, na muuzaji atapokea muamala wa malipo kutoka kwa mnunuzi ili kuweka uwaminifu baina ya muuzaji na mnunuzi.

LAKINI, muuzaji hatoweza kuitoa pesa hiyo mpaka apate namba ya uthibitisho kutoka kwa mnunuzi, na vilevile mnunuzi akishalipa hatoweza kuitoa au kuirejesha pesa hiyo kwenye account yake mpaka apate namba ya uthibitisho kutoka kwa muuzaji. Kwa maana yake watategemeana.

Kwa mfano

Mnunuzi
ameona TV ikitangazwa instagram inauzwa Tsh 500,000/=, lakini yeye yuko Dodoma, na Muuzaji yuko Dar es salaam.

Kwenye menu ya M PESA wekeni kipengele kinaitwa Lipa kwa uthibitisho.

Mnunuzi ataingia kwenye kipengele cha Lipa kwa uthibitisho kisha atatuma pesa taslim TSH 500,000/= kwenda kwenye namba ya Muuzaji 07567563890 kwa ajili ya ununuzi wa TV

Mnunuzi atapokea meseji ya uthibitisho kwamba muamala umefika kwa muuzaji, meseji itaambatana na namba ya uthibitisho labda 7689

Huku kwa Muuzaji, nayeye atapokea muamala wa TSH 5000000/= kutoka kwenye namba ya Mnunuzi 06517271992
Muamala huo utaambatana na namba ya uthibitisho, labda 8126

Sasa, Mnunuzi baada ya kupokea mzigo na kuhakikisha ni wenyewe kwa uhakika, atamtumia namba yake ya uthibitisho yule muuzaji ambayo ni 7689 kwa njia ya kawiada yaani sms,

Kisha huyu Muuzaji nayeye atamatumia mnunuzi namba yake ya uthibitisho ambayo 8126 kwa njia ya kawaida.

Ambapo Muuzaji ataingia kwenye menu ya M PESA kipengele cha Liba kwa uthibitisho kisha ataingia kipengele Thibitisha muamala ulio tumiwa kisha weka namba ya uthibitisho kutoka kwa mnunuzi,ataweka 7689 , akishaweka ataambiwa subiri muamala kuthibitishwa.

Kwa upande wa Mnunuzi, ataingia tena kwenye menu ya M PESA kipengele cha Lipa kwa uthibitisho kisha Thibitisha muamala ulio tuma kisha weka namba ya uthibitisho kutoka kwa muuzaji 8126, akishaweka tu, Muuzaji kule atapokea meseji ya muamala kamili yaani muamala wa kawaida ambao ataweza kuitoa hiyo pesa kwa wakala au kumtumia mtu au kufanya vyovyote vile. (Yaani kwa kifupi ndio inakuwa imeingia rasmi kwenye account yake)

ENDAPO MNUNUZI AKIKATAA KUWKEA HIYO NAMBA YA UTHIBITISHO KUTOKA KWA MUUZAJI, HIYO PESA INABAKIA VODACOM. AMBAPO MNUNUZI NAYEYE HATAWEZA KUITOA.

Kwa mfumo huu, hakuna mtu atakaye uziwa au kuagiziwa bidhaa hewa au yenye utofauti, pia utapeli wa uuzaji na ununuzi utapungua.

Vingine mtaongezea kutokana na Dira niliyoitoa kama nimeelewa.
We jamaa una akili sana Mungu akubariki
 
Hakika wazo ni zuri lakini bado kuna maeneo ya muhimu hayajatatuliwa.

1. Umesema mnunuzi hawezi kurudisha fedha baada ya kulipa..Sasa je,akiletewa bidhaa ambayo siyo ya vigezo vyake inakuwaje ??

Nadhani ili huu mfumo ufanye kazi lazima kuwe na self reversal (Mnunuzi kueeza kurudisha fedha zake pale ambapo bidhaa inakiwa tofauti na alichoagiza).

2. Kwa mitandao ya simu,hii ni huduma ya nyongeza (add on) hivyo ni lazima gharama za ziada ziwepo.Kazi ya kuwa verifier au middleman ni risk na lazima mitandao itranslate risk hii kwa malipo.
1. Inawezekana, ila kwa due process ama due diligence; siyo mnunuzi kujiamulia kuichunia ilhali amepokea bidhaa ama muuzaji kama amedanganya.

2. Makato ni yaleyale ya kawaida na mitandao itafaidikia hapo, sana tu. Business "itachanganya" na wateja wengi, kama si wote, watatokea kuamini katika usalama wa mitandao 100%.
 
34h3h45
 
Back
Top Bottom