Mkurugenzi wa takukuru atia aibu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugenzi wa takukuru atia aibu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 21, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,476
  Likes Received: 5,716
  Trophy Points: 280
  Mkurugenzi Takukuru apigachenga waandishiNa Ramadhan Semtawa

  MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah, jana aliwazidi ujanja waandishi wa habari ambao pamoja na mambo mengine, walijipanga kumkabili kwa maswali.

  Dk Hoseah alicheza mchezo huo katika makao makuu ya Takukuru jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali kwa uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ambavyo alipewa yeye binafsi na rafiki yake wa Marekani, lakini akavifanya kuwa mali ya taasisi hiyo na kutoa msaada.

  Baada ya kuzungumzia msaada huo wa vifaa kwa kifupi, Mkurugenzi huyo alisimama na kuvikabidhi kwa Mpoki Ulisubisya wa Idara ya Usingizi na Wagonjwa Mahuti katika hospitali hiyo.

  Wakati wa makabidhiano hayo na tukio la kupiga picha, tayari baadhi ya waandishi walijiandaa kumchokonoa kuhusu uchunguzi wa wabunge kupokea posho mara mbili ambao hivi sasa umegubikwa taarifa za utata kwamba umesimama na nyingine zikisema unaendelea.

  Lakini, mara baada ya makabidhiano hayo, Dk Hosea aliwaambia wandishi wa habari kuwa "ninyi marafiki zetu itabidi tukae mwakani" kisha akavuta hatua mbili kuelekea mlango wa kutokea.

  Alipoelezwa kuwa waandishi walikuwa na maswali ambayo ni pamoja na kuhusu thamani ya vifaa hivyo na aina yake, alijibu: "jamani hata kukabidhi vifaa mnataka maswali, Mimi nimekuja kukabidhi vifaa tu basi," alisema huku akicheka kipindi ambacho tayari alikwishafunguliwa mlango na kuondoka.

  Mapema Dk Hosea, alisema msaada huo alipewa yeye binafsi na rafiki yake Dk Ngugi Kinyungu, kutoka Jimbo la Ilinois Marekani, lakini akaona si vema kuchukua na kuamua kuutoa kwa hospitali ili usaidie Watanzania wenye matatizo.
  "Nimeona bora vifaa hivi visaidie jamii ya Watanzania wenye shida mbalimbali katika Hospitali ya Taifa Muhimbili," alifafanua Dk Hoseah.

  Alifafanua kwamba, msaada huo ambao umetolewa na Takukuru si wa kwanza na kwamba tayari kuna misaada mbalimbali ya kibinadamu ilitolewa Mbeya, Hospitali ya Saratani ya Ocean Road, Kituo cha Don Bosco na Lushoto.
  Hii ni mara ya pili kwa Dk Hosea, kukwepa maswali ya waandishi wa habari tangu alipowashukia wabunge na kutia ngumu kwamba uchunguzi dhidi yao kuhusu tuhuma za kula posho mara mbili, utaendelea na hakuna aliye juu ya sheria.

  Mara ya kwanza ilikuwa Dodoma alikokuwa ameitwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ambako hata hivyo hakujibu maswali ya waandishi.

  Kwa upande wake, Dk Ulisubisya, alisema vifaa hivyo vya kisasa na ubora wa hali ya juu, vitatumika katika kutolea huduma na kufundishia. Dk Ulisubisya alifafanua kwamba, vifaa ni pamoja na vya kupeleka gazi kwa mtu anayefanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo, kuongezewa maji au dawa kwa wagonjwa wa ICU, upasuaji wa kichwa, kutoa damu iliyoganda mwilini, kuingiza hewa mwilini na kutoa uchafu kama usaha kwa mtu mwenye jipu kwenye mapafu.
   
 2. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Akimbie tu, lakini kunasiku atawatafuta yeye mwenyewe.
   
 3. KILITIME

  KILITIME JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2009
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  "Mapema Dk Hosea, alisema msaada huo alipewa yeye binafsi na rafiki yake Dk Ngugi Kinyungu, kutoka Jimbo la Ilinois Marekani, lakini akaona si vema kuchukua na kuamua kuutoa kwa hospitali ili usaidie Watanzania wenye matatizo."
  "Dk Hoseah alicheza mchezo huo katika makao makuu ya Takukuru jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali kwa uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ambavyo alipewa yeye binafsi na rafiki yake wa Marekani, lakini akavifanya kuwa mali ya taasisi hiyo na kutoa msaada."
  Dkt Hoseah amesema amepewa vifaa hivyo na rafiki yake huko Marekani, sasa sijaona amevifanyaje kuwa eti vimetolewa na Taasisi! Waandishi wa habari acheni kuchemka!
   
 4. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Vifaa vyenyewe mbona hamvitaji?

  Amandla......
   
 5. b

  ba mdogo Member

  #5
  Nov 24, 2009
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona sioni mahala ambapo kichwa cha habari kinaoana na kilichoandikwa? ametia aibu katika lipi?
   
Loading...