Mkurugenzi wa Sumry amkana ailyekuwa mbunge wa Mpanda Magharibi......

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
202,339
2,000
Mkurugenzi wa Sumry azungumza

Wednesday, 08 December 2010 19:27 newsroom
NA MWANDISHI WETU
MKURUGENZI wa Kampuni ya Mabasi ya Sumry, Hamuod Sumry, amefafanua kuwa hana uhusiano wa kibiashara wala kindugu na aliyekuwa Mbunge wa Mpanda Magharibi mkoani Rukwa, Abdallah Sumry, ambaye anatuhumiwa kwa wizi wa gari la serikali. Sumry alitoa ufafanuzi huo jana alipopiga simu kwenye chumba cha habari cha gazeti hili, kufafanua kuhusu habari zilizochapishwa na kumhusisha aliyekuwa mbunge wa zamani na tukio hilo.

ìSina undugu wala uhusiano wa kibiashara na huyo aliyeandikwa,î alisema mmiliki huyo wa mabasi yanayofanya safari katika maeneo mbalimbali nchini na kuwa kufafana huko kwa jina kumemsababishia usumbufu.
Gazeti hili toleo la juzi lilikuwa na habari kuwa aliyekuwa mbunge wa Mpanda Magharibi, anashikiliwa na polisi katika mkoa wa kipolisi wa Temeke kwa tuhuma za kukutwa na gari la wizi mali ya serikali. Ilidaiwa kuwa Sumry alikutwa na gari lenye namba za usajili STK 7080 mali ya Wizara ya Ujenzi na kuwa alikamatwa Jumamosi iliyopita mjini Dar es Salaam akiwa na gari hilo aina ya Land Cruiser, likiwa limengíolewa baadhi ya vipuri.
 

mams

JF-Expert Member
Jul 19, 2009
615
195
Jina lake laweza safishwa mahakamani. Inajulikana wazi kuwa ajina yanafanana, lakini kwa wanini watu waseme ndiye mmiliki wa magari bila kuwa na uhakika?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom