Mkurugenzi wa Mkuranga akataliwa na madiwani, Kikao chavunjika mbele ya Naibu Waziri

SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,955
2,125
Katika hali inayoashiria kwamba mambo si shwari ndani ya Chama cha mapinduzi Kikao cha Baraza la Halmashauri ya Wilaya Mkuranga leo kimevunjika majira ya saa 5.30 asubuhi muda mfupi nbaada ya kufunguliwa na Mwenyekiti wake.
Sababu za kuvunjika kikao hicho ni kuwepo kwa kundi kubwa la madiwani wasiokuwa na imani na Mkurugenzi wa halmashuri hiyo Bi. Sipora Liana. Itakumbukwa kuwa Mwezi April pia Kikao kilichoitishwa kwa dharura hakikumalizkia licha ya kuendelea mpaka saa 3 usiku.

Kiufupi Madiwani wengi walishamkataa huyu Mama muda mrefu mpaka kumlazimu aliyekuwa Waziri wa Tamisemi George Mkuchika kuingilia kati na kusuluhisha ugomvi huo lakini mgogoro uliibuka tena baada ya Mkurugenzi kumtuhumu Afisa Utumishi (Bw.Mbuba ambaye alihamishiwa ghafla wilaya ya Ngara) kwamba ameshirikiana na madiwani kuandikia barua ya isiyokuwa na jina wala sahihi na kuisambaza kwa madiwani wengine ili wamkatae Mama huyo.

Baada kufanya uchunguzi wa kutosha madiwani wakajiridhisha kwamba barua hiyo haikupita masjala kuu kwa hiyo hakukuwa na ushahidi kama hiyo barua haikuandikwa na yeye mwenyewe Mkurugenzi ili kupata sababu ya kumwondoa DHRO.

Ndipo ilipofika leo majira ya saa 5 hivi baada ya kikao kufunguliwa madiwani walitaka kujua hatima ya agenda ya kikao cha mwezi wa 4 ambapo taarifa zilipelekwa kwa Mwantumu Mahiza (Mkuu wa Mkoa wa Pwani) ili aunde tume jambo ambalo halikutekelzwa.

Baada ya kupata majibu ytasiyoridhisha Diwani mmoja baada ya mwingine wakaanzakuvua majoho na kutoka nje na mwisho wa siku walibaki madiwani 7 wafuasi wa Mwenyekiti, mkurugenzi mpamoja na Mbunge wake (Mh Adam Malima ambaye naye alikuwepo). Kwa utaratibu ni kuwa na kuwa na angalau nusu ya wajumbe ilibidi kikao kiahirishwe kwa kuwa walibaki ndani wajumbe 7 kati ya 25 walikuowepo/wanaotakiwa kuwepo.

Wanabodi ni lazima mkumbuke kuwa huyu ndio yule Mama aliyemkamatisha Mbunge na rushwa ya sijui Milioni 2?!!!! Mbunge wa Bahi Omar Badwell.

Nini kinaendelea baadae nitaendelea kuwajuza. Source Mimi Mwenyewe nilikuwepo kwenye tukio
 
Isijekuwa hao madiwani wanatumika kumuangamiza huyo mkurugenzi kwa sababu ya kumkamatisha fedha ya moto mbunge Bedwel.
Ingawa inawezekana pia ni kweli kwamba anapwaya na madai ya madiwani ni genuine.
 
Inaelekea hawa madiwani wa Mkuaranga hawampendi huyu mama kwavile ni muadilifu na jasiri kuweza kumkamatisha yule mbunge wa Bahi mla rushwa!! Jinsi inavyoeelekea huyu Mkurugenzi haendekezi njaa za hawa madiwani hivyo wao kukosa upenyo wa kula na ndio kisa cha kumchukia; hawa ndio watendaji wanaostahili kulindwa na serikali isiyo dhaifu!!
 
Isijekuwa hao madiwani wanatumika kumuangamiza huyo mkurugenzi kwa sababu ya kumkamatisha fedha ya moto mbunge Bedwel.Ingawa inawezekana pia ni kweli kwamba anapwaya na madai ya madiwani ni genuine.
Inawezekana ingawa rekodi zinaonyesha ugomvi huu ulianza tangu 2010.
 
Sipora ni Jimbe la Kazi amethhibiti mianya ya rushwa Mkuranga na ufisadi unaofanywa na wafanyakazi wa halmashauri wakishirikiana na madiwini. kabla ya kufika Sipora Mkuranga magari Binafsi ya Baadhi ya madiwani akiwemo mwenyekiti yalikuwa yanawekewa mafuta kwa kutumia hela ya halmashauri. Nafikiri pia hela ya BADWEL inafanya kazi. Badwel atakuwa amehonga hao madiwani kama alivyohonga waandishi wa habari maana hata habari ya kesi yake haiandikwi tena kama kesi zingine. Kuna mtu wa usalama wa Taifa aliniambia Badwel na hela yake yote nani atamfunga?kesi hii itapigwa mpaka uchaguzi mwingine utakuja. Naomba huyo mama watuletee sisi watu wa Halmashauri ya Babati vijijini. Tunamhitaji atamawa liza mchwa kwenye halmashauri yetu. Hawa Ghasia chondchonde MLete Babati vijijini.
 
Haya sasa; mambo hapo ni MADIWANI NGUVU YA UMMA dhidi ya MKURUGENZI CHAGUO LA RAIS hiyo.
 
Kama ni mwadilifu kweli hayo yanayompata Ndiyo gharama yake. anatakiwa kuvumilia na kuzidisha uadilifu wake.
 
Amuombe na Mungu pia. In this world there are two waiz, either you ar with them or you are with God.
 
Sipora liani sio mwadilifu kama sura yake inavyoonyesha, ila ni mbabe na asiyefuata utaratibu, na inakwenda mpaka nyumbani jinsi anavyo mnyanyasa mumewe...ni picha tosha kwamba hawezi uongozi.
Nahisi atakuwa na mtu anayelea huko tamisemi.
Shule yenyewe hana ndio sasa anasoma m asomo ya jioni.
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Sipora ni Jimbe la Kazi amethhibiti mianya ya rushwa Mkuranga na ufisadi unaofanywa na wafanyakazi wa halmashauri wakishirikiana na madiwini. kabla ya kufika Sipora Mkuranga magari Binafsi ya Baadhi ya madiwani akiwemo mwenyekiti yalikuwa yanawekewa mafuta kwa kutumia hela ya halmashauri. Nafikiri pia hela ya BADWEL inafanya kazi. Badwel atakuwa amehonga hao madiwani kama alivyohonga waandishi wa habari maana hata habari ya kesi yake haiandikwi tena kama kesi zingine. Kuna mtu wa usalama wa Taifa aliniambia Badwel na hela yake yote nani atamfunga?kesi hii itapigwa mpaka uchaguzi mwingine utakuja. Naomba huyo mama watuletee sisi watu wa Halmashauri ya Babati vijijini. Tunamhitaji atamawa liza mchwa kwenye halmashauri yetu. Hawa Ghasia chondchonde MLete Babati vijijini.
Babati? Mbona kabla ya kuhamia Mkuranga alitokea Simanjiro ambako pia alishindana na madiwani? Any way inawezekana Badwel yupo kazini pia
 
Sipora liani sio mwadilifu kama sura yake inavyoonyesha, ila ni mbabe na asiyefuata utaratibu, na inakwenda mpaka nyumbani jinsi anavyo mnyanyasa mumewe...ni picha tosha kwamba hawezi uongozi.
Nahisi atakuwa na mtu anayelea huko tamisemi.
Shule yenyewe hana ndio sasa anasoma m asomo ya jioni.
Hili la kumnyanyasa Mumewe pia nilisikia, eti kwa vile Mume wake ni Mwalimu (Mkuu wa Shule).
 
Njaa za Madiwani ndio chanzo cha chuki,pia inaonekana hata mleta mada ni Kuadi(dalali) wa Mbunge wa Bahi Mh Omar Bad-well! Mleta mada anatupotosha na anataka tuamini kuwa Mh Bad-Well alikamatishwa rushwa,jambo ambalo si kweli Bad-well aliomba rushwa yeye mwenyewe kwa Mkurugenzi,ikumbukwe siku hiyo Bad-well alipo kamatwa alijikojolea pale pale Hotel ya Peacock hii iki leta picha kuwa kujikojolea ni kujutia kosa!
Mleta maada hapa JF tunaichukia rushwa na sio sehemu ya kusafisha wala rushwa! Kama umekula hela ya Bad-well umsafishe basi nenda kwenye magazeti na sio JF!
 
kama hawamtaki watumie sayansi asilia ya kufunga chura kwenye nguo na yai viza na kumwekea mlangoni atatimka mwenyewe,
au wale wajuzi wa mkuranga wa kuwanyoa walimu nywele usiku kwani hawapo? fanyeni kazi hiyo kumtoa
au kumlaza nje kila siku usiku kwa taaluma yenu ya Mkuranga..ujuzi mnao fanyieni kazi lol
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Njaa za Madiwani ndio chanzo cha chuki,pia inaonekana hata mleta mada ni Kuadi(dalali) wa Mbunge wa Bahi Mh Omar Bad-well! Mleta mada anatupotosha na anataka tuamini kuwa Mh Bad-Well alikamatishwa rushwa,jambo ambalo si kweli Bad-well aliomba rushwa yeye mwenyewe kwa Mkurugenzi,ikumbukwe siku hiyo Bad-well alipo kamatwa alijikojolea pale pale Hotel ya Peacock hii iki leta picha kuwa kujikojolea ni kujutia kosa!
Mleta maada hapa JF tunaichukia rushwa na sio sehemu ya kusafisha wala rushwa! Kama umekula hela ya Bad-well umsafishe basi nenda kwenye magazeti na sio JF!
Nataka Badwel afungwe miaka 20 ili CCM iadabishwe lakini pia nafurahi Madaiwani wa Mkuranga wanapogawanyika kwa sababu ni faida kwa kunguru. Kumbuka Mkuranga yote inaongozwa na nambari wani. Pia sikubaliani na tabia ya Mkurugenzi, namfahamu vizuri so usiniingize kwenye kutumika. Sijawahi wala sina mpango. By the way nimsema kwenye majibu yangu kuwa huyu DED alikataliwa kabla ya scandal ya Rushwa, usiwe mvivu hebu pekua kwenye mtandao andika tu "Mkurugenzi wa Mkuranga" au Sipora Liana" Mlengo wa Kati
 
Last edited by a moderator:
Huyu Mama sitamsahau katika maisha yangu, alinipa masaa ya kuondoka wilayani mwake Mkuranga wakati nimekwenda kufanya kazi ya shirika moja la kimataifa na kisha kufika ofisini kwake kujitambulisha. Nitakuja hapa kuwaeleza kilichonitokea lakini kiukweli huyu Mama hafai kwa uongozi hata kidogo.
 
Dikteta yule Mama
 
Yule mama ni zaidi ya mshenzi, na hastahili kupewa ofisi kubwa, hata mwanasheria wake pale anamnyenyekea kama Mungu.
Kumbe unamjua vizuri sana. Yule Mwansheria ndio anayempotosha yule Mama, anamshauri vibaya sana.
 
Back
Top Bottom