Mkurugenzi wa Mkuranga akataliwa na madiwani, Kikao chavunjika mbele ya Naibu Waziri

nasema tena wamtoe wasimtoe sisi tushafaham mbunge wenu BADWEL ni mlafi hafai kanisani wala msikitini, yeye kumnyanyasa mumewe hilo sisi halituhusu hayo inawezekana ni makubaliano yao
 
nasema tena wamtoe wasimtoe sisi tushafaham mbunge wenu BADWEL ni mlafi hafai kanisani wala msikitini, yeye kumnyanyasa mumewe hilo sisi halituhusu hayo inawezekana ni makubaliano yao

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, namfaham vizuri Sipora Liana, ni mama chapakazi, jasiri na anaependa haki, si mpokea rushwa, amefanya kazi Moshi vijijini akaenda Monduli na sasa Mkuranga, ni Graduate wa SUA na kama anasoma sasa basi ni Shahada ya uzamili ambayo mtu hazuiliwi kusoma akiwa anafanya kazi - i mean open university.

Ni vema kuandika kitu ambacho mtu una uhakika nacho na si kusikia halafu ukakirusha hewani, afterall mwanadamu huwezi kumfurahisha kila mtu wapo watakaokubeza wapo watakaokuona unafaa.
 
Sipora liani sio mwadilifu kama sura yake inavyoonyesha, ila ni mbabe na asiyefuata utaratibu, na inakwenda mpaka nyumbani jinsi anavyo mnyanyasa mumewe...ni picha tosha kwamba hawezi uongozi.
Nahisi atakuwa na mtu anayelea huko tamisemi.
Shule yenyewe hana ndio sasa anasoma m asomo ya jioni.

Shule ipo fanya utafiti vizuri.
 
Sipora Liana ni mwanamke Mkurugenzi aliyevaa suali za wanaume mia moja. Hapendi upuuzi,anachapa kazi, si mlarushwa na ameleta maendeleo makubwa sana mkuranga. Mfano kwa kutumia mapato ya korosho amejenga soko na stand. Amenua boti mbili za kisasa kwa wakaazi wa kisiju pwani. Hospitali ya Wilaya ilikuwa haina Mortuary ila yeye kajenga.

Mifano mingine,ameondoa shule sita za matope na kujezijenga kwa kiwango cha matofali.Amejenga barabara za mkuranga mjini na vijijini. Mimi nina shamba kule mkuranga na kwa mara ya kwanza kwa muda mrefu huyu mama kasimamia kutengeneza barabara za vijijini,mimi nafika shambani na gari langu bila wasiwasi.

Sio kwamba kabla ya yeye kuwa mkurugenzi fedha zilikuwa hamna. Zilikuwepo ila kilichokuwa kinafanyika ni fedha kuchukuliwa kwa wazabuni halafu kazi haifanyiki. Mkurugenzi aliyekuwepo kabla yake alikuwa anagawana fedha hizo na madiwani. Na wakati huo haikuwa rahisi kujuwa kama huyu ni afisa au mfagizi. Mfagizi alikuwa na uwezo hata wa kukupa kazi ya uzabuni. Sasa alichofanya huyu mama ni kuleta law and order. "She brought sanity" in Mkuranga.

Anadhibiti manunuzi na matumizi ya Halmashauri(fiscal displine). Madiwani wanalipwa posho halali tu na hamna wanachopewa cha ziada kama walivyozoe huko zamani. Hivyo amewabana kwelikweli na kwa kufanya hivyo amejijengea maadui hasa wale wala rushwa,wababaishaji,wezi na wapenda vya bure.

Yeye ni graduate wa SUA na degree ya Uzamili to Open University. She is very sharp na halazi kazi mezani. Kama tungekuwa na wakurugenzi wengi kama Tanzania ingepaa
 
nasema tena wamtoe wasimtoe sisi tushafaham mbunge wenu BADWEL ni mlafi hafai kanisani wala msikitini, yeye kumnyanyasa mumewe hilo sisi halituhusu hayo inawezekana ni makubaliano yao
Na kufukuza watumishi je? Na udikteta? Habari ya Badwel ni nyingine isitumike kumsafisha mtu
 
Sipora Liana ni mwanamke Mkurugenzi aliyevaa suali za wanaume mia moja. Hapendi upuuzi,anachapa kazi, si mlarushwa na ameleta maendeleo makubwa sana mkuranga. Mfano kwa kutumia mapato ya korosho amejenga soko na stand. Amenua boti mbili za kisasa kwa wakaazi wa kisiju pwani. Hospitali ya Wilaya ilikuwa haina Mortuary ila yeye kajenga. Mifano mingine,ameondoa shule sita za matope na kujezijenga kwa kiwango cha matofali.Amejenga barabara za mkuranga mjini na vijijini....
Mkuu umemtendea haki sana Mama yule kwa kueleza ukweli. Wanabodi wanatakiwa wajue pia kwamba tunapozungumzia madhaifu hatumaanishi kwamba mazuri hayapo, yapo mengi kama ulivyoanisha hapo ila hata Mfalme Sulemani alijenga hekalu zuri sana ila kwa kuwafanya wananchi wake wa Israel kuwa Watumwa. Kweli unaweza kwenda mpaka Kizomla kilometa 45 Shambani kwako lakini upande wa pili inabidi ajirekebishe
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, namfaham vizuri Sipora Liana, ni mama chapakazi, jasiri na anaependa haki, si mpokea rushwa, amefanya kazi Moshi vijijini akaenda Monduli na sasa Mkuranga, ni Graduate wa SUA na kama anasoma sasa basi ni Shahada ya uzamili ambayo mtu hazuiliwi kusoma akiwa anafanya kazi - i mean open university. Ni vema kuandika kitu ambacho mtu una uhakika nacho na si kusikia halafu ukakirusha hewani, afterall mwanadamu huwezi kumfurahisha kila mtu wapo watakaokubeza wapo watakaokuona unafaa.
Mkuu kwenye utendaji wa kazi... Ni miongoni mwa watu wachache sana nchi hii wanaochapa kazi lakini kuna sehemu anapaswa kujirekebisha ili afanikiwe zaidi..Halazi kazi, yuko strict kwenye matumizi, kaziba mianya na hapokesi rushwa ndivyo wanvyosema wanaomfahamu vizuri lakini upande wa pili... Unajua wabongo pia kwa uvivu hatuwapendi watu wakweli..
 
Mkuu umemtendea haki sana Mama yule kwa kueleza ukweli. Wanabodi wanatakiwa wajue pia kwamba tunapozungumzia madhaifu hatumaanishi kwamba mazuri hayapo, yapo mengi kama ulivyoanisha hapo ila hata Mfalme Sulemani alijenga hekalu zuri sana ila kwa kuwafanya wananchi wake wa Israel kuwa Watumwa. Kweli unaweza kwenda mpaka Kizomla kilometa 45 Shambani kwako lakini upande wa pili inabidi ajirekebishe

Samahani Gerrad huo upande wa pili unoongelea ni upi? Funguka mkubwa
 
nasema tena wamtoe wasimtoe sisi tushafaham mbunge wenu BADWEL ni mlafi hafai kanisani wala msikitini, yeye kumnyanyasa mumewe hilo sisi halituhusu hayo inawezekana ni makubaliano yao

Wanasiasa wote lao moja! Mama alijitoa mhanga sasa wanamtoa yeye Mhanga. Hii iangaliwe kwa umakini vinginevyo vita dhidi ya ufisadi itaishia kusikika kwenye majukwaa na redioni tu.
 
wakazi wa Monduli wanamuelewa she is the hardworker!hata E.L alijaribu kumwita nyumbani kwake akamwambia aje ofisini kwa mkurugenzi kwa sababu hakuna ofisi nyumbani kwa m-bunge.so ma-snitch acheni wivu wa kike!
 
Isijekuwa hao madiwani wanatumika kumuangamiza huyo mkurugenzi kwa sababu ya kumkamatisha fedha ya moto mbunge Bedwel.
Ingawa inawezekana pia ni kweli kwamba anapwaya na madai ya madiwani ni genuine.

Wazo lako la kwanza ndo sahihi kabisa.
Madiwani wa hizi zinazoitwa halmashauri wanataka wizi, wizi, wizi basi!
Ukisikia kumetulia ujue Mkurugenzi anagawana pesa na hao madiwani ktk vikao. Huyu mama siku zote amesifika kwa kutotaka upuuzi.

Hebu angalia scenario hii. Madiwani walistahili kumusifu kwa kuweka wazi matumizi safi ya halmashauri bila rushwa na kukataa kumuhoga huyo mbunge *****. lakini eti wanagomea kikao kwa sababu afisa mmoja alihamishwa kama ilivyoelezwa kwenye thrd.

Hizi halmashauri hazifiki kokote kwa viwango hivi vya uelewa, bahati mbaya pwani yetu nayo elimu duni. Wapi utapata diwani mwenye kichwa kilichojaa. Ukiangalia kwa makini utakuta hao 7 waliobaki ktk kikao siyo marafiki wa Mkurugenzi bali elimu yao nafuu.

Jamani Katiba iweke kiwango cha chini cha elimu kuwa Diwani. Napendekeza F.VI
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Katika hali inayoashiria kwamba mambo si shwari ndani ya Chama cha mapinduzi Kikao cha Baraza la Halmashauri ya Wilaya Mkuranga leo kimevunjika majira ya saa 5.30 asubuhi muda mfupi nbaada ya kufunguliwa na Mwenyekiti wake.
Sababu za kuvunjika kikao hicho ni kuwepo kwa kundi kubwa la madiwani wasiokuwa na imani na Mkurugenzi wa halmashuri hiyo Bi. Sipora Liana. Itakumbukwa kuwa Mwezi April pia Kikao kilichoitishwa kwa dharura hakikumalizkia licha ya kuendelea mpaka saa 3 usiku.

Kiufupi Madiwani wengi walishamkataa huyu Mama muda mrefu mpaka kumlazimu aliyekuwa Waziri wa Tamisemi George Mkuchika kuingilia kati na kusuluhisha ugomvi huo lakini mgogoro uliibuka tena baada ya Mkurugenzi kumtuhumu Afisa Utumishi (Bw.Mbuba ambaye alihamishiwa ghafla wilaya ya Ngara) kwamba ameshirikiana na madiwani kuandikia barua ya isiyokuwa na jina wala sahihi na kuisambaza kwa madiwani wengine ili wamkatae Mama huyo.

Baada kufanya uchunguzi wa kutosha madiwani wakajiridhisha kwamba barua hiyo haikupita masjala kuu kwa hiyo hakukuwa na ushahidi kama hiyo barua haikuandikwa na yeye mwenyewe Mkurugenzi ili kupata sababu ya kumwondoa DHRO.

Ndipo ilipofika leo majira ya saa 5 hivi baada ya kikao kufunguliwa madiwani walitaka kujua hatima ya agenda ya kikao cha mwezi wa 4 ambapo taarifa zilipelekwa kwa Mwantumu Mahiza (Mkuu wa Mkoa wa Pwani) ili aunde tume jambo ambalo halikutekelzwa.

Baada ya kupata majibu ytasiyoridhisha Diwani mmoja baada ya mwingine wakaanzakuvua majoho na kutoka nje na mwisho wa siku walibaki madiwani 7 wafuasi wa Mwenyekiti, mkurugenzi mpamoja na Mbunge wake (Mh Adam Malima ambaye naye alikuwepo). Kwa utaratibu ni kuwa na kuwa na angalau nusu ya wajumbe ilibidi kikao kiahirishwe kwa kuwa walibaki ndani wajumbe 7 kati ya 25 walikuowepo/wanaotakiwa kuwepo.

Wanabodi ni lazima mkumbuke kuwa huyu ndio yule Mama aliyemkamatisha Mbunge na rushwa ya sijui Milioni 2?!!!! Mbunge wa Bahi Omar Badwell.

Nini kinaendelea baadae nitaendelea kuwajuza. Source Mimi Mwenyewe nilikuwepo kwenye tukio
Huyo msma Ipora ni Jembe, nani asiyejua njaa ya madiwani na kuendekeza rushwa.
Wao wakakae vijiweni wamwachie huho mama achape kazi.
 
Back
Top Bottom