Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini wa TAKUKURU anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha aandika barua kwa DPP kukiri makosa

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,298
2,000
Wakili wa utetezi katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kulthum Mansoor umedai kuwa wameandika barua kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kwa ajili ya kukiri makosa yake

D1EE55EB-1497-4C50-98C1-79A22DC07F81.gif


Mansoor anakabiliwa na mashtaka manane ya kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha Sh1.477 bilioni.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon kudai mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu kuwa bado upelelezi haujakamilika.

Wakili wa Utetezi, Elia Mwingira amedai kuwa wameandika barua kwenda kwa DPP kwa ajili ya kuomba msamaha na kukiri makosa, hivyo ni vyema kupata majibu kwa haraka ili mshtakiwa aweze kupata haki yake ya msingi.

"Tunaomba upande wa mashtaka kulifuatilia hili ili mteja wetu aweze kupata haki yake ya msingi," amedai Mwingira.

Baada ya maelezo hayo, Simon amedai kuwa suala hilo atalifuatilia kwa haraka na
Hakimu Mhina ameahirisha shauri hilo hadi Oktoba 16, 2019 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.
Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari 2013 na Mei 2018, mshtakiwa alighushi barua ya ofa ya Agosti 13, 2003 kwa madhumuni ya kuonyesha kuwa, barua hiyo imetolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo huku akijua kuwa si kweli.

Katika shtaka la pili, inadaiwa kati ya Januari 2012 na Mei 2017 huko maeneo ya Upanga ndani ya Wilaya ya Ilala, mshtakiwa kwa kudanganya, alijipatia Sh5.2 milioni kutoka kwa Alex Mavika ambaye ni mfanyakazi wa Takukuru, kama malipo ya kiwanja kilichopo Kijiji cha Ukuni wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Pia, inadaiwa kati ya tarehe hizo, Mansoor alijipatia Sh3 milioni kutoka kwa Wakati Katondo kama malipo ya kiwanja kilichopo maeneo ya Kijiji cha Ukuni wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Mshtakiwa huyo pia anadaiwa kuwa alijipatia Sh5milioni kutoka kwa Ofisa wa Takukuru, Gogo Migutah kama malipo ya kiwanja kilichopo eneo hilo.

Katika shtaka la tano, inadaiwa Mansoor alijipatia Sh7 milioni kutoka kwa Ekwabi Majungu ambaye pia ni ofisa wa Takukuru kama malipo ya kiwanja hicho.

Mansoor anadaiwa kati ya Januari 2012 na Mei 2017, maeneo ya Upanga jijini Dar es Salaam, akiwa Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini wa ofisi hiyo, alijipatia Sh7 milioni kutoka kwa John Sangwa kama malipo ya kiwanja cha eneo hilo.

Indaiwa kuwa mshtakiwa akiwa mwajiriwa wa Takukuru, alijipatia Sh5 milioni kutoka kwa Rose Shingela kwa ajili ya malipo hayo.

Katika mashtaka ya utakatishaji fedha, inadaiwa kati ya Januari 2013 na Mei 2018 huko maeneo ya Upanga, mshtakiwa alijipatia Sh1,477,243,000 wakati akijua kuwa fedha hizo ni haramu na ni zao la kosa tangulizi la kughushi.
 

Uwazitu

JF-Expert Member
Aug 19, 2019
1,415
2,000
Alipe tu mzigo wetu

HIZO ZITAKUWA ZA SERIKALI AU WATARUDISHIWA WENYEWE?

HUYU NAYE NI
MHUJUMU UCHUMI AU NI TAPELI?

HAYA NA NINYI MATAPELI NJOONI MLIPE PESA MLIZOTAPELI.

MLIPATA MITAJI BILA RIBA, KAMA HAMKUFANYIA BIASHARA NA KUPATA FAIDA, KIVYENU.
 

Anti-Hacker

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
806
1,000
haikusaidii lolote kuinua hali yako,( of course ya Jiwe na wanaomzunguka itaimarika) utaendelea na umasikini mpaka unaingia kaburini na kuwaachia/kuwarithisha kila moja anayekuhusu umasikini wako pamoja na kuwa watakili wote!

Mbona unakurupuka mi nimesema inanisaidia kitu....kuku maji wew
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom