Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 749
- 1,797
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Dkt Maulid Madeni amemtumbua wadhifa wake Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya cha Ngarenaro,Dkt.Japhet Kivuyo na kuwa Mganga wa kawaida kwa kosa la kutoroka kazini na kwenda kula pasaka na kuwaacha solemba wagonjwa waliokuwa wakisubiri kutibiwa
Tayari dkt Madeni amemteua Dkt David Mng'anya kushika nafasi yake huku akiunda tume ya kuchunguza tukio hilo na tabibu wengine katika jiji la Arusha wenye tabia kama hiyo ya kutoroka kazini bila taarifa hasa siku za sikukuu.
Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa hatua hiyo imekuja kufuatia sauti iliyonaswa na kurushwa kwenye mitandao ya kijamii ,ambapo mkuu huyo wa kituo alisikika akibishana na viongozi wa Kamati ya siasa ya ccm kata ya Levolosi waliotembelea kituoni hapo wakitekeleza majukumu yao, akidai yupo kanisani na hawezi kurudi kazini kwa sababu ni kipindi cha sikukuu.
" Hatua ya kwanza tuliochukua ni kumvua uongozi ili iwe fundisho kwa tabibu wengine wenye Tabia kama hii ,wananchi wanapaswa kuhudumiwa muda wote kwa Massa 24 na si vinginevyo"Alisema Dkt Madeni
Dkt,Madeni aliwaomba radhi wananchi waliopatwa na adha hiyo ambao walikuwa katika kituo hicho cha afya wakihitaji Huduma ya matibabu.
"Kauli aliyoitoa si majibu ya kiuongozi yeye.kama kiongozi anapaswa kuwa kioo cha jamii ,kama ingetokea akaja mgonjwa mahututi na akafia pale nini kingetokea "