Mkurugenzi wa Golden Shark Mining Ltd kizimbani kwa kutapeli na kutakatisha zaidi ya tsh bilioni 4

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
index.jpg
Mkurugenzi wa kampuni ya Golden Shark Mining Ltd, Cuthbert Kishululi amepandishwa katika kizimbani cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu likiwemo la kutakatisha zaidi ya USD milioni mbili, ambazo ni sawa na zaidi ya bilioni nne.

Kishululi (48) anayeishi Salasala jijini Dar es salam , wamesomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Respicious Mwijage wa mahakama hiyo.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa serikali, Pius Hilla amesema, January 4 mwaka 2013 jijini Dar wa Salaam, mshtakiwa kwa nia ya kudanganya alitengeneza nyaraka ya uongo ambayo ni cheti cha kumbukumbu kuonyesha kuwa hajawahi kufanya uhalifu ( Non- Criminal Certificate) cha 17 August 2015.

Imedaiwa kuwa, cheti hicho kilikuwa na nia ya kuonyesha kuwa, kimetolewa na Munusco United Nations Organization Stabilization Mission in the Democratic Republic of Congo kwenda kwa M/S Delicore Metals Company Ltd, huku akijua kuwa siyo kweli.

Hilla ameendelea kudai kuwa, kati ya Julai Mosi na Agosti 30 mwaka juzi,mshtakiwa kwa nia ya kudanganya, alijipatia USD 2,405,000, ambazo ni zaidi ya milioni nne, kutoka Holism Group Ltd kwa uongo baada ya kujifanya angewapatia kilo 500 za dhahabu kutoka kwenye kampuni hiyo ya Holism kupitia kampuni yake ya Golden Shark Mining Ltd.

Katika shtaka la tatu imdaiwa kuwa, kati ya Julai 22 na Agosti 27 mwaka juzi, mshtakiwa alitakatisha fedha hizo kwa kujihusisha kwenye muamala wa USD 2,405,000 na kuelekeza fedha hizo zipelekwe kwenye account namba 010095361111 iliyopo katika bank ya I and M bank kwa jina la Delicore Metals Kampuni.

Aidha imedaiwa kuwa, mshtakiwa alizitoa fedha hizo huku akijua kuwa ni zao la uhalifu wa kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.Hata hivyo, mshtakiwa amekana mashtaka yote, na amerudishwa rumande kwa kuwa shtaka la utakatishaji wa fedha halina dhamana.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika, imeahirishwa hadi Julai 14 ambapo upande wa mashtaka unatarajia kuongeza washtakiwa wengine katika kesi hiyo.
 
heeee
kulikoni tena na huu mfululizo wa hizi kesi za kutakatisha maana wiki ya pili mfululizo tunazisikia
ila pongezi nusu kwa taasisi husika maana nadhani tunao watakatishaji wengi kwenye mfumo ila hawagusi
hivi ANDREW CHENGE hana kesi ya kutakatisha kweli
[HASHTAG]#HappyBirthdayToMe[/HASHTAG]
 
Kushitaki ni rahisi sana, lakini kuwatia hatiani ni ngamia kupita tundu la Sindano. Je Serikali ipo vizuri na waendesha mashitaka kiasi cha kuwawezesha kuendesha kesi hizo kwa ufanisi. Isiwe kama PCCB, ipo vizuri kutoa takwimu za kesi walizofungua, lakini si takwimu za kesi walizoshinda.

Mfano kuachiwa kwa Kasusura ulikuwa ni uzembe wa waendesha mashitaka, hata kesi ya samaki wa Pombe ilikuwa ni uzembe tu, ushahidi ulikuwa vizuri ila kwa uzembe wakakosea taratibu. Kesi zote hizo wanaachiwa kwa technicality tu!!
 
Na bado vita ya uchumi ni kubwa sana so.movie itaendelea tu ngoja tuone magereza yatajaa sana na bado wale wengine wanakuja tu wa escrow kuna wabunge na mawaziri wastuuuuufuu yetu macho
 
heeee
kulikoni tena na huu mfululizo wa hizi kesi za kutakatisha maana wiki ya pili mfululizo tunazisikia
ila pongezi nusu kwa taasisi husika maana nadhani tunao watakatishaji wengi kwenye mfumo ila hawagusi
hivi ANDREW CHENGE hana kesi ya kutakatisha kweli
[HASHTAG]#HappyBirthdayToMe[/HASHTAG]
Yan hawa jamaa wa kwenye system wanakuwa wamekuweka kwenye target. Wanakukamua kama ng'ombe, wakishahakikisha umeishiwa maziwa ndio sasa wanakupeleka korokoroni...
 
Haki itapatikana. Hivi kama ulipiga mabilioni na unayo bado then unaona wenzio daily wanasombwa b4 the court bado upo Tz tu? Doing what?

Masikini ndio Binadamu Movable zaid kwa kuwa Hana cha kupoteza

Tajiri akimbie Nchi kizembe Zambe wakati Account zake Bank zinasoma Mabillion Ana Majumba, Mashamba na Vitega uchumi kadhaa?
 
Kushitaki ni rahisi sana, lakini kuwatia hatiani ni ngamia kupita tundu la Sindano. Je Serikali ipo vizuri na waendesha mashitaka kiasi cha kuwawezesha kuendesha kesi hizo kwa ufanisi. Isiwe kama PCCB, ipo vizuri kutoa takwimu za kesi walizofungua, lakini si takwimu za kesi walizoshinda.

Mfano kuachiwa kwa Kasungura ulikuwa ni uzembe wa waendesha mashitaka, hata kesi ya samaki wa Pombe ilikuwa ni uzembe tu, ushahidi ulikuwa vizuri ila kwa uzembe wakakosea taratibu. Kesi zote hizo wanaachiwa kwa technicality tu!!
Kwenye kesi ya samaki wa magufuli.kw mala ya kwanza serikali ilshinda.waka kata rufaa.ndipo rushwa ikatembea ikaonekana kesi imefunguliwa vibaya.na ikawa imetupwa. Wanaohongwa ni wale mawakili wa serikali.
 
Back
Top Bottom