Mkurugenzi wa Bandari amesema kuwa DP World bado hawajaanza kazi na hakuna mfanyakazi aliyevunjiwa mkataba wake

Kuna hili la kuwa kutakuwa na watumishi watakaoamia DP WORLD na watakaobaki TPA. Je kama wafanyakazi wa TPA wote watagoma kwenda DP WORLD nini kitatokea kama DP WORLD akiajir watumishi wapya hawa waliobak TPA watakuwa watumishi hewa au watafanya kazi gani nyingine?
Mawazo ya kichawichawi
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mkurugenzi Mkuu wa bandari yetu ya Dar es salaam Ndugu Mrisho amekanusha taarifa za uzushi na uongo mkubwa ulioenezwa na watu kuwa wafanyakazi wa bandari ya Dar wamevunjiwa mkataba na DP World ambao wameleta wafanyakazi wao.amesema kuwa taarifa hizo ni za uongo na zenye kuleta taharuki tu katika jamii.

Amesema kuwa taarifa hizo ni za uongo kwa kuwa DP World bado hajaanza kazi au shughuli zake japo anatarajia kuanza kazi hivi karibuni na pia hakuna mfanyakazi ambaye atavunjiwa mkataba wake, ameeleza kuwa pia bandari inaendelea na kazi yake usiku na mchana huku wafanyakazi wakifanya kazi kwa shift na wala hakuna mgomo wa aina yoyote ile wa wafanyakazi wa bandari,Lakini pia amekanusha habari ya kuwa kuna upendeleo katika utoaji wa mizigo pale bandarini.amesema kuwa taarifa hizo nazo ni za uzushi na uongo kwa kuwa jambo hilo halipo hata kidogo na badala yake haki inatendeka vyema kwa watu wote..

Rai yangu ni kuwa serikali ianze kuwachukulia hatua kali sana vijana wa CHADEMA ambao wamekuwa mstari wa mbele kutoa na kuleta habari za uzushi ,uongo na uchonganishi kupitia mitandao ya kijamii.nasema hivi kwa kuwa hata habari hii imezushwa na vijana wa CHADEMA ambao wakati wote wamekuwa ni watu wenye kuleta habari za kuleta taharuki na sintofahamu katika jamii.

Tabia hii ikiachwa iendelee na kukomaa pasipo watu hawa kuchukuliwa hatua za kisheria italeta shida kubwa sana mbele ya safari,ipo siku watakuja wazue jambo litakalo tetemesha na kutikisa usalama wetu wa Taifa pamoja na utulivu katika Taifa hili .watafanya hivi kwa kujuwa kuwa hakuna hatua za aina zozote zile zitakazochukuliwa zidi yao ,mfano katika suala hilo walilozusha linaleta athari katika uchumi wetu kwa sababu linaleta taharuki na sintofahamu kwa Wafanyabiashara wanaotegemea na kuitumia bandari yetu.

Kutoa taarifa kuwa kuna upendeleo katika utoaji wa mizigo bandarini maana yake ni kuwapa hofu watumiaji wa bandari ambao wanaweza kuhama kuitumia bandari yetu katika kupitishia mizigo yao, na kuamua kutumia bandari za washindani wetu na hivyo kupunguza mapato yatokanayo na bandari na hivyo kupunguza mapato katika nchi. Jambo hili tunaweza kuliona dogo lakini katika jicho la tatu hili siyo la kulifumbia macho maana linauwezo wa kuathiri uchumi wetu.

Lakini pia watu hawa hasa vijana wa CHADEMA wanaweza kutumiwa na mahasimu wetu na washindani wetu kiuchumi au hata maadui zetu waliojificha kuwapa taarifa za uongo na uzushi ili wazitoe kupitia mitandao ya kijamii na hivyo kuleta taharuki,kuharibu mahusiano ya kidiplomasia,kuleta hali ya kutoaminiana,kuleta na kupandikiza chuki kwa watu,kuleta uhasama,visasi na vinyongo.

kwa hiyo ni muhimu sana serikali ianze kuwachukulia hatua kali sana za kisheria. uhuru una mipaka yake.uhuru pasipo mipaka ni fujo na hatari kwa usalama wa Taifa letu.ni lazima tufahamu upi ni uhuru wa mtu na wapi unaishia na upi ni wajibu wa mtu.ni lazima kila mtu ajuwe ana wajibu wa kuheshimu sheria zetu pasipo kutoa habari au taarifa zenye kuleta taharuki katika jamii pasipo ushahidi wa aina yoyote ile.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

Lucas, hivi mzee Mwashambwa, ana hata fununu tu kuwa huwa unafanya kazi hii ya uchawa? Yawezekana hana hata habari. Nina hakika kama angejua angekuwa tayari amewaita hata wazee wenzake wakukalishe chini kukurudi ili angalao uitafute hekima.

Naona kama umekwishalemaa. Hata unapokuwa na kitu cha kuandika, ambacho kinaweza kuwa cha kweli na muhimu, lazima ukiharibu kwa sababu ya uchawa.

Uutambue na kujivunia utu na ubinadamu wako. Hao unaoamua kujitoa akili na utu wako kwaajili yao ni wanadamu kama wewe. Huna sababu ya kujifanya duni kiasi hicho. Kumbuka mazoea hujenga tabia. Kujizoesha kuwa mtu wa hovyo mwishowe utakuwa kweli mtu hovyo.

Thamini utu wako.
 
Hii mada imekuzidi kimo cha upeo wa akili yako .kwa hiyo ingekuwa vyema ungesubiri mada zinazoendana na akili yako maana hii ni mzigo mkubwa kwako.
 
Ukweli ni kuwa huyu Lucas hana baba ndiyo maana anahangaika kama kuku anayetaka kutaga
 
Hii mada imekuzidi kimo cha upeo wa akili yako .kwa hiyo ingekuwa vyema ungesubiri mada zinazoendana na akili yako maana hii ni mzigo mkubwa kwako.

Kwa huu upuuzi unaouweka humu kila siku, wakitafutwa watu 5 wenye akili ndogo kabisa, upeo duni kupindukia, wasiojitambua, wanafiki na watafuta makombo ya watawala, wewe huwezi kukosekana.

You are mind crippled, good for nothing. Only that you posses human being features, our respect to you only rests on that, nothing else.
 
Mada hii imekuzidi akili yako ,kwa hiyo wewe subiri mada za kuendana na akili yako.hii waachie wenye akili kubwa au somaga tu maoni ya watu😀😀😀
 
Kupunguzwa kazi ni inevitable (Watapunguzwa tu) huwezi ukaongeza automation usipunguze manual labor
 
Tuna wasomi wajinga Sana.
Ukituhumiwa jibu tuhuma basi
Hatua za kuchukuliwa Sio kazi yako Kwa sababu haina maana ulivyojibu Ndio ukweli
Tatizo unachanganya siasa Kwenye kazi za taaluma. Haifai hata kidogo
Mkurugenzi Jenga kujiamini
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mkurugenzi Mkuu wa bandari yetu ya Dar es salaam Ndugu Mrisho amekanusha taarifa za uzushi na uongo mkubwa ulioenezwa na watu kuwa wafanyakazi wa bandari ya Dar wamevunjiwa mkataba na DP World ambao wameleta wafanyakazi wao.amesema kuwa taarifa hizo ni za uongo na zenye kuleta taharuki tu katika jamii.

Amesema kuwa taarifa hizo ni za uongo kwa kuwa DP World bado hajaanza kazi au shughuli zake japo anatarajia kuanza kazi hivi karibuni na pia hakuna mfanyakazi ambaye atavunjiwa mkataba wake, ameeleza kuwa pia bandari inaendelea na kazi yake usiku na mchana huku wafanyakazi wakifanya kazi kwa shift na wala hakuna mgomo wa aina yoyote ile wa wafanyakazi wa bandari,Lakini pia amekanusha habari ya kuwa kuna upendeleo katika utoaji wa mizigo pale bandarini.amesema kuwa taarifa hizo nazo ni za uzushi na uongo kwa kuwa jambo hilo halipo hata kidogo na badala yake haki inatendeka vyema kwa watu wote..

Rai yangu ni kuwa serikali ianze kuwachukulia hatua kali sana vijana wa CHADEMA ambao wamekuwa mstari wa mbele kutoa na kuleta habari za uzushi ,uongo na uchonganishi kupitia mitandao ya kijamii.nasema hivi kwa kuwa hata habari hii imezushwa na vijana wa CHADEMA ambao wakati wote wamekuwa ni watu wenye kuleta habari za kuleta taharuki na sintofahamu katika jamii.

Tabia hii ikiachwa iendelee na kukomaa pasipo watu hawa kuchukuliwa hatua za kisheria italeta shida kubwa sana mbele ya safari,ipo siku watakuja wazue jambo litakalo tetemesha na kutikisa usalama wetu wa Taifa pamoja na utulivu katika Taifa hili .watafanya hivi kwa kujuwa kuwa hakuna hatua za aina zozote zile zitakazochukuliwa zidi yao ,mfano katika suala hilo walilozusha linaleta athari katika uchumi wetu kwa sababu linaleta taharuki na sintofahamu kwa Wafanyabiashara wanaotegemea na kuitumia bandari yetu.

Kutoa taarifa kuwa kuna upendeleo katika utoaji wa mizigo bandarini maana yake ni kuwapa hofu watumiaji wa bandari ambao wanaweza kuhama kuitumia bandari yetu katika kupitishia mizigo yao, na kuamua kutumia bandari za washindani wetu na hivyo kupunguza mapato yatokanayo na bandari na hivyo kupunguza mapato katika nchi. Jambo hili tunaweza kuliona dogo lakini katika jicho la tatu hili siyo la kulifumbia macho maana linauwezo wa kuathiri uchumi wetu.

Lakini pia watu hawa hasa vijana wa CHADEMA wanaweza kutumiwa na mahasimu wetu na washindani wetu kiuchumi au hata maadui zetu waliojificha kuwapa taarifa za uongo na uzushi ili wazitoe kupitia mitandao ya kijamii na hivyo kuleta taharuki,kuharibu mahusiano ya kidiplomasia,kuleta hali ya kutoaminiana,kuleta na kupandikiza chuki kwa watu,kuleta uhasama,visasi na vinyongo.

kwa hiyo ni muhimu sana serikali ianze kuwachukulia hatua kali sana za kisheria. uhuru una mipaka yake.uhuru pasipo mipaka ni fujo na hatari kwa usalama wa Taifa letu.ni lazima tufahamu upi ni uhuru wa mtu na wapi unaishia na upi ni wajibu wa mtu.ni lazima kila mtu ajuwe ana wajibu wa kuheshimu sheria zetu pasipo kutoa habari au taarifa zenye kuleta taharuki katika jamii pasipo ushahidi wa aina yoyote ile.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
Sasa kuna haja gani kuwapa DP uongozi wa bandari yetu. Hii mipango ya kizandiki ndio inatukwamisha kama nchi. Uroho wa vigogo wanatuaminisha hatuwezi chochote. Sisi tuwekeze halafu tuwalete wajanja kwa mgongo wa dubai kuja kuvuna faida huku hawawekezi kitu. Jamani huu ni ufala au ujinga😭😭
 
Back
Top Bottom