Mkurugenzi Tunduru aanza vitisho

Kama mnavyoweza kukumbuka wanajamii forums kuna taarifa iliandikwa ktk jukwaa hili kuhusu Watumishi wa Halmashauri ya willaya ya Tunduru kuwanyanyasa walimu wapya. Kwamba, walimu waliokuwa na tofauti kidogo katika majina yao walilipishwa Shs 82,000/ kwa ushirikiano kati ya ofisi ya Utumishi na Ofisi ya mwanasheria wa Halmashauri.

Badala ya Mkurugenzi kuwaita au kutafuta taarifa za siri kujua ukweli juu ya tuhuma husika yeye ameenda kinyume kwa kuwaita walimu anaowahisi hasa waliotoka ktk mikoa ya kaskazini. Amewaita leo ofisini kwake amewalazimisha wakiri kuwa either ni wao au wanawafahamu waliorushwa habari zille jamii forums.

Baada ya hapo amewapeleka Polisi kutoa maelezo, sijui ni maelezo gani. Kwa vyovyote vile inawezekana walimu wale hawahusiki wala pengine hawajui chochote kinachoendelea ktk mitandao ya jamii ukizingatia wako porini maeneo ambayo haina mawasiliano ya simu.

Huku jamii forums nataka nimjulishe Mkurugenzi huyu mlevi wa madaraka kuwa mtanzania yoyote mzalendo anayechukia uonevu, rushwa, dhuluma anaweza kutumia jukwaa hili kuifikishia serikali ujumbe. Mkurugenzi ndio ametuonesha kuwa habarii zile ni za ukweli na yeye ni mhusika na naujua mchezo wote wa watumishi wake.

Walimu wetu sasa hivi wako ndani polisi wananyanyaswa badala ya wala rushwa kukamatwa wamewageuzia wanyonge waliokopa hata nauli ya kufika Tunduru mjini ambayo inafika shs 20,000/. Mwalimu moja nasikia ana watoto wadogo sana amewaacha bila mtu wa kuwaaangalia nauli yenyewe amekopa lakini yuko polisi.

Mwanasheria aliyekuwa anachukua hizo pesa anajulikana kwa majina hata namba zake za simu zinajulikana ila Mkurugenzi amemkumbatia na kuwageuzia kibao innocent people kwa kuwabambikia kesi za uwongo na uzushi. Kama taarifa ni za uwongo kwanini awapeleke walimu polisi? Polisi ni kichaka cha kuficha uovu wao? Tuna taarifa wanaanda mpango wa kuwafukuza kazi juu kwa juu. Jamani jeshi letu la Polisi kwanini mtumiwe na watumishi wasio waaminifu kunyanyasa innocent people?

Rais wetu mpendwa mkono wako ni mrefu tunakupigia magoti umwagize waziri wa TAMISEMI mh. Ummy Mwalimu awanusuru watanzania wenzetu wanaonyanyaswa pale wilayani Tunduru kwa uonevu mkubwa. Huyu Mkurugenzi ni nani ktk nchi hii? Mbona Rais anasemwa anaandikwa, Waziri Mkuu anasemwa anaandikwa, mawaziri waandikwa wanalalamikiwa hawafanyi mchezo huu. Huyu mkurugenzi amejisahau amejifanya Mungu mtu, ananyanyasa binadamu wenzake tunaomba msaada wa Serikali kuu walimu wetu wanusurike.
@Julius Mtatiro Ina maana haoni Mambo haya au mpaka atumiwe watu wa kuchunguza kule Kama mwenzake Sabaya
 
View attachment 1870398
Anaitwa ndg Gasper Zahoro Balyomi. Habari zilizotufikia punde simu za dada moja mwalimu mpya hazipatikani mpaka sasa hivi mara ya mwisho alikuwa polisi saa 5 asubuhi. Dada mwenyewe ana watoto wadogo, Mungu wangu isije akawa amelazwa polisi. Sijui watoto wake itakuwaje kule porini. Nani amewpikia, watalala na nani? Namuombea Mungu awanusuru. Mama yetu Rais mnusuru mwananchi wako anayeonewa bila kosa lolote
Na miwani yake kama macho ya panzi
 
Serikali hii viongozi wengi wakubwa ni wanawake akiwemo waziri mhusika Ummy Mwalimu, Professor Ndalichako. Mwanamke mwenzenu yuko ndani polisi ana watoto wadogo mnataka walale nje na njaa? Kwanini msiwe na huruma? Huyu Mkurugenzi ni nani atese watumishi hivi? tena mgeni ambaye hajalipwa hata hela ya kujikimu. Tunduru ni Msumbiji? Naomba msaidie mama wa watu ajiunge na watoto wake. Pigeni simu Tunduru.
Asulubiwe Huyo kolo
 
Back
Top Bottom