Mkurugenzi Tunduru aanza vitisho

northener

Member
Sep 5, 2018
12
18
Kama mnavyoweza kukumbuka wanajamii forums kuna taarifa iliandikwa ktk jukwaa hili kuhusu Watumishi wa Halmashauri ya willaya ya Tunduru kuwanyanyasa walimu wapya. Kwamba, walimu waliokuwa na tofauti kidogo katika majina yao walilipishwa Shs 82,000/ kwa ushirikiano kati ya ofisi ya Utumishi na Ofisi ya mwanasheria wa Halmashauri.

Badala ya Mkurugenzi kuwaita au kutafuta taarifa za siri kujua ukweli juu ya tuhuma husika yeye ameenda kinyume kwa kuwaita walimu anaowahisi hasa waliotoka ktk mikoa ya kaskazini. Amewaita leo ofisini kwake amewalazimisha wakiri kuwa either ni wao au wanawafahamu waliorushwa habari zille jamii forums.

Baada ya hapo amewapeleka Polisi kutoa maelezo, sijui ni maelezo gani. Kwa vyovyote vile inawezekana walimu wale hawahusiki wala pengine hawajui chochote kinachoendelea ktk mitandao ya jamii ukizingatia wako porini maeneo ambayo haina mawasiliano ya simu.

Huku jamii forums nataka nimjulishe Mkurugenzi huyu mlevi wa madaraka kuwa mtanzania yoyote mzalendo anayechukia uonevu, rushwa, dhuluma anaweza kutumia jukwaa hili kuifikishia serikali ujumbe. Mkurugenzi ndio ametuonesha kuwa habarii zile ni za ukweli na yeye ni mhusika na naujua mchezo wote wa watumishi wake.

Walimu wetu sasa hivi wako ndani polisi wananyanyaswa badala ya wala rushwa kukamatwa wamewageuzia wanyonge waliokopa hata nauli ya kufika Tunduru mjini ambayo inafika shs 20,000/. Mwalimu moja nasikia ana watoto wadogo sana amewaacha bila mtu wa kuwaaangalia nauli yenyewe amekopa lakini yuko polisi.

Mwanasheria aliyekuwa anachukua hizo pesa anajulikana kwa majina hata namba zake za simu zinajulikana ila Mkurugenzi amemkumbatia na kuwageuzia kibao innocent people kwa kuwabambikia kesi za uwongo na uzushi. Kama taarifa ni za uwongo kwanini awapeleke walimu polisi? Polisi ni kichaka cha kuficha uovu wao? Tuna taarifa wanaanda mpango wa kuwafukuza kazi juu kwa juu. Jamani jeshi letu la Polisi kwanini mtumiwe na watumishi wasio waaminifu kunyanyasa innocent people?

Rais wetu mpendwa mkono wako ni mrefu tunakupigia magoti umwagize waziri wa TAMISEMI mh. Ummy Mwalimu awanusuru watanzania wenzetu wanaonyanyaswa pale wilayani Tunduru kwa uonevu mkubwa. Huyu Mkurugenzi ni nani ktk nchi hii? Mbona Rais anasemwa anaandikwa, Waziri Mkuu anasemwa anaandikwa, mawaziri waandikwa wanalalamikiwa hawafanyi mchezo huu. Huyu mkurugenzi amejisahau amejifanya Mungu mtu, ananyanyasa binadamu wenzake tunaomba msaada wa Serikali kuu walimu wetu wanusurike.
 
Tunduru! Nakosa neno sahihi kwenye kuchangia ila pole yao ndg zetu yote yanapita kwa sababu zake muumba mbingu na ardhi....

Swala la sulpha feki limefikia wap kama upo uko
 
Duu! nimeumia sana, hii habari niliandika mwenyewe nikiamini km ilivyo siku zote hili jukwaa inatumiwa na Serikali na wote wenye mapenzi mema kusaidia wanyonge na wanaonyanyaswa. Anyway, nawapa pole wote mliopatwa na majanga hayo ila Mungu yuko upande wetu Serikali itakuwa imesikia na naamini Serikali hii ni sikivu hasa mama yetu wa TAMISEMI Ummy Mwalimu.

Tunachoomba km kweli kuna mtu au watu wamewekwa ndani na Mkurugenzi watolewe bila masharti yoyote badala yake tuhuma yenyewe ifuatiliwe na wahusika wawajibishwe akiwemo Mkurugenzi mnyanyasaji na anayewatetea waovu walio chini yake.

Mkurugenzi huyu habari zake si geni humu jamii forums alishaandikwaga sana, nashangaa kwanini serikali haimfuatilii. Tunategemea kusikia watanzania wenzetu wamesaidiwa na hawatishiwi tena. Comrade Julius Mtatiro tusaidie wananchi wako.
 
Duu! nimeumia sana, hii habari niliandika mwenyewe nikiamini km ilivyo siku zote hili jukwaa inatumiwa na Serikali na wote wenye mapenzi mema kusaidia wanyonge na wanaonyanyaswa...
Huyo Mkurugenzi anaongozwa na mtazamo wa kizamani kama kukosolewa ni kuvunjiwa heshima na utu.

Poleni sana walimu kama mnatarajia msaada wa Ummy mtakua mmeangukia pua.
Mkurugenzi kwenye halmashauri yake ya Tanga jiji ni mwizi,mtoa rushwa na mbabe kama huyo mnae mlalamikia.

Chini ya Ummy TAMISEMI haitakua na jipya sana ikilinganishwa na ile ya Jaffo
 
Huko Tunduru si ndiko DC Mtatiro anaomba rushwa ili aachie ng’ombe zisitaifishwe

Tuwekee jina lake hapa tumlipue huyo dikteta UCHWARA.
1627393463842.png

Anaitwa ndg Gasper Zahoro Balyomi. Habari zilizotufikia punde simu za dada moja mwalimu mpya hazipatikani mpaka sasa hivi mara ya mwisho alikuwa polisi saa 5 asubuhi. Dada mwenyewe ana watoto wadogo, Mungu wangu isije akawa amelazwa polisi. Sijui watoto wake itakuwaje kule porini. Nani amewpikia, watalala na nani? Namuombea Mungu awanusuru. Mama yetu Rais mnusuru mwananchi wako anayeonewa bila kosa lolote
 
Angalia sura na pozi lake, anaonekana katili kweli. Huyu siyo ameiweka serikali ya mama mfukoni. Ila siamini liMkurugenzi tu la Halmashauri ya wilaya. Ila kuna mtu kule TAMISEMI atakuwa anampa kiburi siyo bure ndio maana hajali wala haogopi ukizingatia jiwe(JPM) hatunaye tena sijui km mama anaweza kututetea. Hivi wa hao polisi siyo binadamu? Ndugu yao angetendewa hivyo wangejisikiaje? Muachieni dada wa watu aende kwa watoto wake. Inaonekana wamenyanganya na simu asipate hata wa kumdhamini.

Ulaaniwe mkurugenzi na jopo lako lote Mungu anawaona na atawageuzia kibao kwa ushetani wenu huo.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Pesa zote wanazopiga lakini hawatosheki, hadi unaanza kuwanyanyasa watumishi wanaoanza kazi ambao ndio kwanza wananza maisha ya utumishi.
 
Serikali hii viongozi wengi wakubwa ni wanawake akiwemo waziri mhusika Ummy Mwalimu, Professor Ndalichako. Mwanamke mwenzenu yuko ndani polisi ana watoto wadogo mnataka walale nje na njaa? Kwanini msiwe na huruma? Huyu Mkurugenzi ni nani atese watumishi hivi? tena mgeni ambaye hajalipwa hata hela ya kujikimu. Tunduru ni Msumbiji? Naomba msaidie mama wa watu ajiunge na watoto wake. Pigeni simu Tunduru.
 
View attachment 1870398
Anaitwa ndg Gasper Zahoro Balyomi. Habari zilizotufikia punde simu za dada moja mwalimu mpya hazipatikani mpaka sasa hivi mara ya mwisho alikuwa polisi saa 5 asubuhi. Dada mwenyewe ana watoto wadogo, Mungu wangu isije akawa amelazwa polisi. Sijui watoto wake itakuwaje kule porini. Nani amewpikia, watalala na nani? Namuombea Mungu awanusuru. Mama yetu Rais mnusuru mwananchi wako anayeonewa bila kosa lolote
Mkuu huo uzi mwingime ukowapi?
Ambao umeanzisha malalamiko yote haya?

Upandishe hapa au hata PM. Kuna mtu anataka kuona kama anaweza kufanya jambo
 
Wakurugenzi Kama Hawa hawafai kabisa,sijui huwa vinatumika vigezo gani kupata wakurugenzi!Kuna mwingine huyu wa halmashauri ya wilaya ya RUNGWE-MBEYA-tunamtafutia ushahidi,uzi wake utakuja hapa soon!

Jamiiforum idumu milele maana humu ndiyo tunatemea nyongo zetu!
 
Wakurugenzi Kama Hawa hawafai kabisa,sijui huwa vinatumika vigezo gani kupata wakurugenzi!Kuna mwingine huyu wa halmashauri ya wilaya ya RUNGWE-MBEYA-tunamtafutia ushahidi,uzi wake utakuja hapa soon!

Jamiiforum idumu milele maana humu ndiyo tunatemea nyongo zetu!
wanapiga ndumba hatari yaan ndumba za hatariii,huwez jiamini hvhv lazma cheketu cheketu ihusike
 
Hakuna waandishi wampigie simu ahojiwe ili ajichanganye kama yule wa Temeke.Ila wizara ya Tamisemi inatakiwa waziri kama Awesso au Lukuvi
 
Back
Top Bottom