Mkurugenzi Mtendaji wa TBC, Dr. Ayoub Rioba apata ajali Kigoma, mtu mmoja afariki dunia

wastage of resources aisee, gari hiyo ya kwenda nayo vumbi kweli, hapo inauzwa milioni kama mia tatu, anatembelea mtu mmoja tu kwenda kweney mradi wa laki ngapi, ona sasa imedondoka na kuharibika, hapo tumetupa kwenye maji milioni mia tatu hapo. ndo maana watu walipendekeza uko kwenye mavumbu nendeni na magari ya kwenye vumbi. mnatia hasara tu na vifo kwa watu.
 
Kama Dereva ni wa hapa Dar kujikuta kwenye eneo kama hilo (Mgombe) wakati wa mvua kama alikuwa na mwendo mkali kubinuka ni lazima.
 
Wakati wa mvua Kama huu Kama unaenda kibondo, kasulu au Kigoma town bora ukifika Nyakanazi kodi dereva wa huko maana gari kugeuka ilipotoka ni dk kwa utelezi. Wazawa huwa wanatembea speed Kama kawaida [HASHTAG]#michomoko[/HASHTAG]
 
Hawa WACHUMIA Tumbo ambao walikuwa hawajazoe Kula NEEMA za nchi sasa wameanza kula wanakuwa kama Wamewehuka kila Siku Safari tu hadi Dereva anachoka hatimaye anapindua gari kwa USINGIZI.
 
Hizi gari Land Cruiser V8 zilizouzwa Tanzania usikute zina hitilafu fulani kwenye system!!!maana sio kawaida ingekuwa Marekani wangeshaagiza uchunguzi wa kina kuyachunguza hayo magari na kama kungekuwa na hitilafu yoyote wangelipwa fidia na gari zote aina hii zilizo mikononi mwa raia zingerudishwa kurekebishwa.

Ila hapa kwetu inatokea ajali wanakufa watu tunabaki kusema kazi ya Mungu kuangalia plan B ya tatizo hatutaki wala upeo huo hatuna.kingine hawa madreva wa kiserikali wanaendesha gari zao akikupita utasema anaeendesha ni mwendawazimu.wabadilike!
 
Mkurugenzi Mtendaji wa TBC, Dr. Ayoub Rioba amepata ajali ya gari katika eneo la Mgombe, Kigoma ambapo mtu mmoja amefariki dunia.

Taarifa hizo zimethibitishwa na Kamanda Wa Polisi Mkoa wa Kigoma, OtienoView attachment 720716

Nikiwa mwaka wangu wa pili Chuoni nakumbuka kuna Mzee wangu mmoja hivi na pia alikuwa ni Mwandishi wa Habari ' Mwandamizi ' kabisa nilipomuona tu nilizungumza nae mengi tu ya kuhusu ' Tasnia ' yetu na nikamuambia kuwa ningependa kuja kufanya Kazi Tizama Badilika Chukua Media nikimaliza Masomo yangu.

Huku nikitegemea angenijibu jibu tu la haraka nakumbuka Kwanza aliniangalia kwa huruma kisha akaniuliza nina Umri gani na tatu akaniambia kwamba nifanye Kazi katika Media zote ila nisije kuthubutu kufanya Kazi hapo Tizama Badilika Chukua Media kwani Watu wanapigana mno kama siyo sana ' Ndumba / Fusho / Ulozi / Uchawi / Ola Ola ' na kwamba wapo baadhi walioaga dunia kiajabu kiajabu tu na wapo ambao hadi sasa ' nyaya ' zao Ubongoni mwao zimeachana na ule ' waya ' mkubwa unaopeleka taarifa katika Chumba cha Uelewa na Ufahamu ' timilifu ' kilichopo katika Medulla Oblangata ya Mwanadamu.

Pole sana Mwalimu wangu wa Habari na Mawasiliano, Poti wangu kabisa na mmoja wa Watu ambao walinishawishi mno Mimi kupenda kuwa Mwana ' Tasnia ' Mzee Dr. Ayub Ryoba kwa Ajali hiyo na kunusurika. Pia pole kwa hao waliopoteza maisha ambapo mpaka sasa taarifa zinatukanganya wengine wanasema ni wawili na hapa tunaona ni mmoja. Nakuombea kwa Mwenyezi Mungu Wewe na hao Wenzako mliopata ' majeraha ' mpone haraka na hao Marehemu basi Roho zao zikae mahala pema peponi Amen.

Usisahau tu ' Poti ' wangu kwenda Nyumbani Tarime mara moja kusalimia kwani umeponea chupuchupu sana huko leo.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa TBC, Dr. Ayoub Rioba amepata ajali ya gari katika eneo la Mgombe, Kigoma ambapo mtu mmoja amefariki dunia.

Taarifa hizo zimethibitishwa na Kamanda Wa Polisi Mkoa wa Kigoma, OtienoView attachment 720716
300m zimekwenda tena. hivi kuna sababu gani kudrive all the way to kigoma? kwanini temesa wasiwe na pool cars kwa ajili ya vip. wapande saratoga hadi kigoma wakifika wapewe gari ya DAS.
 
Hizi gari Land Cruiser V8 zilizouzwa Tanzania usikute zina hitilafu fulani kwenye system!!!maana sio kawaida ingekuwa Marekani wangeshaagiza uchunguzi wa kina kuyachunguza hayo magari na kama kungekuwa na hitilafu yoyote wangelipwa fidia na gari zote aina hii zilizo mikononi mwa raia zingerudishwa kurekebishwa.

Ila hapa kwetu inatokea ajali wanakufa watu tunabaki kusema kazi ya Mungu kuangalia plan B ya tatizo hatutaki wala upeo huo hatuna.kingine hawa madreva wa kiserikali wanaendesha gari zao akikupita utasema anaeendesha ni mwendawazimu.wabadilike!
Ni ushamba tu hili v8 ndo lakupeleka kigoma na mvua hizi? Wangeazima gari la RAS au mkuu wa mkoa. Juzi tena ffu kalitupa gari kule arusha kisa tairi bandia
 
Tatizo la Kasulu ni barabara kuteleza hata kwa mvua ndogo ya dakika 10.
Kuna ajali nyingi za malori ya mizigo maeneo ya Kasulu nyingi ya ajali hizo zina sababishwa na Utelezi wa barabara pindi magari yanapopishana.
Cha msingi ni kuzitanua barabara hizo na kuondoa side slope kali zinazopelekea magari kuanguka hata kama yakiwa katika speed ndogo.
Mfano mmoja ni juzi tu, kuna Lori lilikuwa limebeba Ng'ombe likiwa linapanda kilima fulani hivi ilibidi utafutwe mchanga kuweka katika mapitio ya taili zake ili kuongeza friction forces kwani taili zilikuwa zinazunguka tu bila ya gari kusogea mbele.
 
Njia kama huijui jiepushe Na high speed....pia u mgenivwa njia uliza kwa watu wanaoijua wakupe pre caution
 
Ni ushamba tu hili v8 ndo lakupeleka kigoma na mvua hizi? Wangeazima gari la RAS au mkuu wa mkoa. Juzi tena ffu kalitupa gari kule arusha kisa tairi bandia

Wala siyo suala la kuazima. Pale Mkoani kunakuwa na magari mengi sana tu yame pack. Le Director ange board Bombardier mpaka Kg, then akapewa Landcrusier Hard top na dereva mwenyeji ampeleke huko Kasulu na Kibondo. Shida ya hawa jamaa zetu wanapenda sana 'kucheza na jukwaa'!

Poleni wafiwa na majeruhi Allah awafanyie wepesi mpate nafuu ya mapema.
 
Back
Top Bottom