Mkurugenzi Mtendaji wa TBC, Dr. Ayoub Rioba apata ajali Kigoma, mtu mmoja afariki dunia

Nakumbuka Barua Yake humu Jukwaani ya kumkejeli Lissu aliyekuwa Nairobi Hospital akiugulia Maumivu! Hii ilikuwa baada ya ahadi ya kishika Uchumba Cha Dola milioni 300(HEWA)iliyotolewa na Barrick! Aliongea mbovu Sana! Binadamu tusijisahau, Uhai na Uzima vyote Tumeazimwa, mwenye navyo anavichukua muda wowote akitaka! Naamni leo amechungulia, haamini Kama hajatumbukia humo, liwe fundisho!
 
Hivi mkurugenzi hakutakiwa kutumia SU kweli...?? Mbona naona STK, au siku hizi hakuna ulazima..??
 
Nikiwa mwaka wangu wa pili Chuoni nakumbuka kuna Mzee wangu mmoja hivi na pia alikuwa ni Mwandishi wa Habari ' Mwandamizi ' kabisa nilipomuona tu nilizungumza nae mengi tu ya kuhusu ' Tasnia ' yetu na nikamuambia kuwa ningependa kuja kufanya Kazi Tizama Badilika Chukua Media nikimaliza Masomo yangu.

Huku nikitegemea angenijibu jibu tu la haraka nakumbuka Kwanza aliniangalia kwa huruma kisha akaniuliza nina Umri gani na tatu akaniambia kwamba nifanye Kazi katika Media zote ila nisije kuthubutu kufanya Kazi hapo Tizama Badilika Chukua Media kwani Watu wanapigana mno kama siyo sana ' Ndumba / Fusho / Ulozi / Uchawi / Ola Ola ' na kwamba wapo baadhi walioaga dunia kiajabu kiajabu tu na wapo ambao hadi sasa ' nyaya ' zao Ubongoni mwao zimeachana na ule ' waya ' mkubwa unaopeleka taarifa katika Chumba cha Uelewa na Ufahamu ' timilifu ' kilichopo katika Medulla Oblangata ya Mwanadamu.

Pole sana Mwalimu wangu wa Habari na Mawasiliano, Poti wangu kabisa na mmoja wa Watu ambao walinishawishi mno Mimi kupenda kuwa Mwana ' Tasnia ' Mzee Dr. Ayub Ryoba kwa Ajali hiyo na kunusurika. Pia pole kwa hao waliopoteza maisha ambapo mpaka sasa taarifa zinatukanganya wengine wanasema ni wawili na hapa tunaona ni mmoja. Nakuombea kwa Mwenyezi Mungu Wewe na hao Wenzako mliopata ' majeraha ' mpone haraka na hao Marehemu basi Roho zao zikae mahala pema peponi Amen.

Usisahau tu ' Poti ' wangu kwenda Nyumbani Tarime mara moja kusalimia kwani umeponea chupuchupu sana huko leo.
tatizo letu la ndani ndo hili... poti poti.....tunaukabila usiozungumzwa...ajali na upoti vinakujaje hapa?
 
Tatizo la Kasulu ni barabara kuteleza hata kwa mvua ndogo ya dakika 10.
Kuna ajali nyingi za malori ya mizigo maeneo ya Kasulu nyingi ya ajali hizo zina sababishwa na Utelezi wa barabara pindi magari yanapopishana.
Cha msingi ni kuzitanua barabara hizo na kuondoa side slope kali zinazopelekea magari kuanguka hata kama yakiwa katika speed ndogo.
Mfano mmoja ni juzi tu, kuna Lori lilikuwa limebeba Ng'ombe likiwa linapanda kilima fulani hivi ilibidi utafutwe mchanga kuweka katika mapitio ya taili zake ili kuongeza friction forces kwani taili zilikuwa zinazunguka tu bila ya gari kusogea mbele.
Solution ni kuweka lami tu fashta, si lingine
 
Pole Dokta.Vipi hilo Puto litapigwa mnada?Serikali huwa haina muda wa kutengeneza magari ya namna hiyo na mbaya sana huwa haikatii bima magari yake (ST...SM,DFP..) .Ni muda muafaka sasa kwa Serikali kuliangalia hili la kukatia magari yake bima.Yaani VX la milioni 200 likipata ajali (write-off) na Kilometa mfano 1,000 ndiyo mwisho wake.Sina nia mbaya,nashauri tu.
 
Mambo ya Mungu haya,hata Idiamini Mungu alimpenda zaidi ingawa misukule walimpenda sana.
 
Pole mkurugenzi ingekuwa ni enzi zako ukiwa na akili zako timamu pale UDSM kabla haijapakwa rangi ya kijani wangekupa pole wengi sana kwa upendo na umuhimu wako

Mungu akuponye
Kwa majungu uloanza nayo sidhani kama hiyo pole ataisikia
 
Mugombe Kasulu hiyo, dongo jekunduuuuuu!! Huwa linawatesa sana vijana wa kutoka kwenye lami lazima gari uipige chini tu!!

Madereva wengi wa serikali wana mwendo wa kasi sana barabarani iwe mikoani au Dar es Salaam Magari ya mawaziri ndiyo zaidi kwa mwendo kasi...
 
Back
Top Bottom